Visa gani pombe ilikufanyia hutasahau?

Visa gani pombe ilikufanyia hutasahau?

Mpwa. Dawa ya hangover Ni maji hasa ya uvuguvugu saa kumi mpaka kumi na moja ALFAJIRI. Hakikisha unakunywa glass nne au tano. Drink the water on an empty stomach for best results and thank me later.
Infact hata Kama unaamka ukiwa huko fresh kwasababu ya uchafu ulio jikandamiza kwenye utumbo mkubwa, that is the remedy.
Asante, japo kuamka alfajiri yote hiyo kupasha maji na kunywa pia ni changamoto
 
Maji weka kwenye chupa ya chai . Kama una water dispenser mambo mswano kabisa. Chukua maji ya kawaida changanya na Yale ya Moto.
Kuhusu kuamka asubuhi sana. Nunua vile vi Tecno vya 18,000 vina alarm ya kuamsha hata tembo.
Ninacho cha itel aiseee ni kero
 
Kuna pombe hio inaitwa 211 kule ughaibuni nilikunywa kopo mbili halafu nilikwenda club. Yaani nilikuwa najiona kama Superman mikono kama ndege inayotaka kuruka. Nikaingia club nikamchapa mzungu flani nikatolewa nje nikaanza kuwatukana mabausa sijui kilitokea nini ila niliishia hospital wiki 2 na miezi 6 home.😂😂

View attachment 1576989


Ndukiiiii 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
Alcohol 8.1℅, siyo mbaya kwa kuamkia asubuhi.
 
Kuanzia mwaka 2013 mpaka sasa nimepoteza washkaji watatu wakaribu....tunasema ni mipango ya Mungu lakini sababu ni Pombe na washkaji wote tunajua ni Pombe...wamefariki wakiwa bwiii..acha waliolemaa kwa Pombe.
Nipo likizo ya bila malipo tangu mwanzoni mwa mwezi October nikilitafakari hili.
 
Pombe bwana...

Sitasahau ilivyonilaza kwenye ngazi...


Ila nimeachana nayo kabisa.
 
Kipindi Niko chuo kikuu Cha Dar es Salaam miaka Ile. Tulikua tunakwenda kunywa wanzuki au mbege maeneo ya Riverside. Siku hiyo tulipata boom vzr Basi tukaona tukapate mbili tatu. Tukafika pale zilipo hostel za mabibo enzi hizo hazijajengwa kulikua na vibanda vya pombe za ovyo. Tukaanza kugida wanzuki. Wenzangu wakachoka wakaniacha na li barmeid Fulani umri umesogea. Kufika saa nne hivi nikaanza kuliona Ni beautiful Fulani. Basi nikalikokota Hadi hall one tower block kwa wale mliopitia shule za ukweli. Tukapanda mpaka kwa room na kufanya majambooz. Asubuhi naamka kwenda kukojoa nikaona ndala za yule mmama zilikua zimetoboka pale anapokanyagia na zimekarabatiwa na waya. Kumcheki kichwani ametia Ile kalkit ya muonekano Kama nywele zimetiwa maji au mafuta mengi. Kumbuka wanafunzi wameshaanza kukaa pale chini karibu na ofisi ya hall manager, wengine wanapiga stori wakitokea kafeteria kupata chai. Mimi Niko juu gorofani na msukule wangu unao dai lazima nimpeleke kituo Cha Basi. Madem wa chuo nao wapo pale stendi wanasubiri daladala. Mimi bado Nina msukule wangu anadai anataka kuwahi kutengeneza pombe mabibo. Aloo.
Nilimlaumu shetani na kazi zake zote. Nitampitishaje yule msukule mbele ya ma brazamen?
Hii iliendelea wapi??
 
Kuanzia mwaka 2013 mpaka sasa nimepoteza washkaji watatu wakaribu....tunasema ni mipango ya Mungu lakini sababu ni Pombe na washkaji wote tunajua ni Pombe...wamefariki wakiwa bwiii..acha waliolemaa kwa Pombe.
Nipo likizo ya bila malipo tangu mwanzoni mwa mwezi October nikilitafakari hili.
Walikuwa wanadrive?
 
Kuanzia mwaka 2013 mpaka sasa nimepoteza washkaji watatu wakaribu....tunasema ni mipango ya Mungu lakini sababu ni Pombe na washkaji wote tunajua ni Pombe...wamefariki wakiwa bwiii..acha waliolemaa kwa Pombe.
Nipo likizo ya bila malipo tangu mwanzoni mwa mwezi October nikilitafakari hili.
Ilikuwaje mkuu
 
Hii iliendelea wapi??
Mkuu we acha tu. Hebu jaribu kufikiria kipindi hicho Niko 24/25 smart, learned, nasindikiza mmama mchafu muuza wanzuki mbele ya mademu wa chuo kikuu ambao ndio saizi yangu halafu najua habari hii itamfikia Demu wangu wa chuo ambae ni matawi. Hebu fikiria mabest wake wakimfikishia hiyo taarifa....
 
Nina visa lukuki vya pombe kwa miaka 25 niliyokunywa pombe. Niliwahi kuzuiliwa kupanda ndege mara mbili kwa sababu ya kuwa chakali, mara ya kwanza ilikwa fast jet ya kwenda mbeya na mara ya pili ilkuwa nchi moja ya ughaibuni, yaani nikiwa airport nasubiri kupanda ndege nikasikia kiu, nikaenda kwenye yale maduka yao nikanunua pombe kali kwa dola 14, nikaingia chooni nikaikata yote. Kilichofuata ni kuzuiliwa kupanda ndege hadi kesho yake.
Mzee vipi umefanikiwa kuacha?
 
Jamani pombe we acha tu.
Kule kijijini Kuna pombe inaitwa dengerua au boha. Hii pombe Ni very potent. Wengi wanainywea bar/vilabuni lakini wale watu matawi wa kijijini kama walimu, daktari, nesi na mchungaji huwa Wanaagiza na kuzama ndani ya nyumba ya mwalimu mmoja na kuanza kukata kiu.

Kuna siku moja shetani alitembelea kile Kijiji na kwa bahati mbaya team matawi walikua wanakata kiu Kama kawaida. Walikuweko walimu watatu, nesi wa Kijiji na mchungaji nae alikwenda kugida akiamini Hawa watamtunzia Siri.
Wakati wanaendelea kukata kiu shetani akamnongoneza mchungaji kwamba aondoke na yule nesi wakapumzike kwenye migomba kwa dharula. Nesi nae hakupenda kumpunja mchungaji starehe aliyoipenda pamoja na utu uzima wake.
Walivyokua wanatumia sign language na kukonyezana walidhani wale wengine hawaoni. Giza lilipoingia wakaona umefika muda muafaka.

Mara nesi akaaga anatoka, dakika mbili nyingi mchungaji nae akajifanya ametosheka. Nesi kwake Kuna watoto mchungaji nae kwake Kuna mke , watoto na kijukuu kimoja hivo wakaamua waende green lodge a.k.a kwenye migomba kupeana uroda.
Mchungaji alivua nguo zote ili zisichafuke kwenye zoezi Hilo ovu otherwise wife atastuka. Nesi nae kaamua kuvua zote ili zisiingie udongo. Wakaanza kupeana mahaba, kumbe mwalimu mmoja alikua anamuwania yule nesi sasa kitendo Cha nesi kuchukuliwa kirahisi rahisi na mchungaji kilimuudhi sana hivyo akaona awakomeshe once and for all. Yeye aliwafuatia nyuma tartiib na walipokua kwenye mchakato wa starehe yule mwalimu mkware akachukua nguo zao zote Hadi boxer ya mchungaji na kufuli na sidiria za nesi na pombe ikamtuma kuzipeleka LIVE kwa mke wa mchungaji. Alipofika alimwambia mama mchungaji mumeo Ni mzinzi Kama huamini nguo zake hizi hapa na za huyo kimada wake.

Kile kitendo Cha nguo zao kuchukuliwa mchungaji hakukiona maana alikua anakaribia kufika Mawenzi lakini nesi aliona. Kabla hata mchungaji hajafika Mawenzi vizuri nesi alimwambia mwalimu Fulani amechukua nguo zao na kuondoka zazo. Ile habari ulikifanya kitendea uroda Cha mchungaji kusinyaa chap Kama Kobe anavyoingiza kichwa kwenye kasa lake.
Kwanza kabisa waliondoka pale vile vile wakiwa uchi lakini hakuna aliyemtamani mwenzake Tena. Mchungaji pombe zilinitoka na alikua anamuona nesi Kama Dada yake mkubwa.

Mchungaji hakurudi nyumbani siku Ile ilhali akiwa uchi, nesi alizubaa na usiku wa manane akarudi kwake na kuapa hatarudia pombe Tena akirudia afe.

Mchungaji haikueleweka Ila saa mbili asubuhi kesho yake akiwa na nguo zisizokua zake na zilizombana sana alionekana kwa mkuu wa Jimbo na barua ya kujiuzulu uchungaji bila sababu za msingi.

Huku nyumbani nesi nae Hana raha maana nguo zake pamoja na chupi na sidiria viko kwa mbaya wake.
Ukitaka kumuumiza mwanamke wa kipare kisaikolojia chukua chupi yake ambayo haijafuliwa halafu tokomea nayo. Sasa huyu chupi iko kwa mbaya wake ataanzaje? Sio chupi tu na khanga na gauni na sidiria.
Ina maana mke wa mchungaji alikua amemuweka nesi anapomtaka.
Itaendelea...........
 
Back
Top Bottom