Hii ya ukweni bora wewe mkuu ulikuwa umempeleka tu bro wako mimi yalinikuta makubwa,
Hii ilinitokea mwaka june 2014 siku ya kwanza kabisa nilipoenda kutambulishwa ukweni na ilikuwa ni kwenye sikukuu ya midsummer (kwa wanaoishi au walioishi Sweden watakuwa wanaifahamu sikukuu hii maana ni sikukuu kubwa sana sweden)
Familia ilikutana nje ya mji ambako ndio kuna summer house, ikiwa ni kusherehekea sikukuu hii pamoja na kutambulishwa kwangu kwenye familia, Tulifika eneo la tukio kwenye saa nne asubuhi na ilikuwa ni mbali kidogo na tunapoishi
Basi tukaanza mdogo mdogo na bia huku tunapiga stori za hapa na pale
Chakula kikaiva tukala, baada ya chakula ikawa toti za tequilla tukanywa kadhaa kila mtu, mwingine akasema ni lazima nionjeshwe Absolut maana ndio pombe yao wanayojivunia nayo nikapewa toti mbili tatu, kufika kwenye saa kumi na mbili jioni nyumba ikachangamka sana maana karibia familia yote ilikuwa imelewa, na stori za hapa na pale zikiendelea
Baada ya chakula cha usiku shemeji yangu akaamua kuleta box la red wine la lita 5, nalo likafunguliwa tukaanza kunywa,
Kiukweli mi sio mnywaji kiviile sasa haya mambo ya kuchanganya pombe yakaanza kunipa shida, nikamwambia mume wangu awaambie ndugu zake kuwa mi sitaweza kuendelea maana nimelewa sana hivyo naenda kulala, kweli akawataarifu, tukainuka ili anipeleke room nikalale dah hata sijafika mlangoni nikarudisha chenji ya hela yote[emoji24][emoji24][emoji24]
Kesho yake nikaamka sasa nataka nikaoge si ndio nakutana na nguo zina matapishi ndio nikakumbuka kuwa jana yake nilirudisha chenji, nikaona acha niende kusafisha chap nikakuta pameshasafishwa, ikabidi kumuasha mme wangu ili kumuuliza kama ni yeye ndio aliepiga mop kumbe nae hata hana kumbukumbu ya kilichotokea,
Niliamka bado nna pombe kichwani ila baada ya yeye kuonekana hakumbuki kilichoendelea baada ya mimi kutapika pombe zote ziliniisha
Sema nashukuru wakwe zangu na familia yote hawakuichukulia hiyo kama big deal ila hata hivyo siku zote zilizofuata ambazo nilikuwa hapo nilikunywa kwa umakini mkubwa sana mpaka sikukuu ilipoisha nikarudi zangu kwangu bila kufanya tukio lolote la kutia aibu!!!
Sent from my SM-A207F using
JamiiForums mobile app