Visa gani pombe ilikufanyia hutasahau?

Visa gani pombe ilikufanyia hutasahau?

Hahah hakuna mbadala mzee baba ila tu siku hizi nimekua nachukia sana hangover(nadhani nimeanza kuzeeka sasa) maana natakiwa saa 11 asubuhi niwe nimeshaamka nimekaa mbele ya PC nafanya kazi,so nikiwa na hangover kazi haziendi ipasavyo.

Inshort siku hizi pombe zinanichosha ila siwezi kuacha ng'o,hahah
Una mishemishe gani mr
 
kisa cha kwanza nilikuwa na bro tukaenda ukweni kwake alikuwa anataka kuvuta jiko lake basi kabla ya kufika akaona tupandishe ujasiri na beer Kibo sa 2x2,Kufika ukweni tukapata tunangojewa kwa shangwe shughuli ikaenda vizuri tu
tukaendelea kujirudishia shukrani pale ukweni ilipofika maji ya shingo kwakuwa sikuwa mzoefu wa unywaji nikarudisha chenji pale ukweni kwa bro kwakweli hili liliniumiza sana leo na kesho
Kisa kingine ni kunywa na kesho yake sina memory yoyote kujua nilikula wapi,nilikunywa nini na home nimerud vp naamka najikuta home tu lakini sijui nilirudi vp imetokea kama tatu,nikaona itakuja niletea maafa nikaamua kupumzika ni mwaka saa
NOTE; kama ni mnywaji usinywe ukweni kabisa wakuu wakwe wanaweza kukujazia meza na ikawa kipimo cha kukupa binti yao bana😀
Ukweni ulikunywa/ulifakamia bia...
Hiyo kuzima na kupoteza memories ulikunywa pombe Kali.
Drink responsibly mkuu, pombe so mbaya Bali ubaya huja pale unapotaka kujifanya mbabe kwenye pombe na yenyewe haipendi dharau😆😆
 
Karibu na Pale Buguruni sokoni, kuna bar Fulani Ina guest house. Gesti yenyewe ni zile za Kiswahili chumba kulia chumba kushoto corridor Kati halafu bafu vyoo na vyumba vya short time kule uwani. Ile gesti ilikua na vyumba vinne kulia na vinne kushoto. Basi bwana tumeyapiga maji na bibie fulani Kisha tukaamua tuchukue chumba kabisa mule mule.

Tukaendelea na maji ya mende mpaka bar inatungwa tukaingia chumbani. Punde si punde mkojo wa bia huo. Nikatoka nikaenda chooni kule uwani kumbe na mteja mwingine nae alikua chooni. Mimi ilikua ndogo tu chap nikarudi yeye ilikua kubwa nikamuacha anaendelea kujikamua. Sasa nikasahau mlango wangu nikaingia kwake huku taa imezimwa lkn unaona kwamba kitanda ni kile neti ni ile na demu wake alikua uchi wa mnyama amekaa mkao wakuliwa kitandani (si unajua wanawake zetu wakilewa) wakati naendelea kuweka neti vizuri niingie njema ikaingia huku akihisi nataka niendelee na demu wake.

Alooh. Mpaka kuja kuikomvinsi Ile njemba kwamba nilikosea chumba ilikua muda sana na aliniomba niende nae chumba changu akahakikishe kwamba na Mimi ninae demu wangu. Pombe zilinitoka hata sijui zilienda wapi.....
 
Karibu na Pale Buguruni sokoni Kuna bar Fulani Ina guest house. Gesti yenyewe Ni zile za kiswahili chumba kulia chumba kushoto corridor Kati halafu bafu vyoo na vyumba vya short time kule uwani. Ile gesti ilikua na vyumba vinne kulia na vinne kushoto. Basi bwana tumeyapiga maji na bibie Fulani Kisha tukaamua tuchukue chumba kabisa mule mule. Tukaendelea na maji ya mende mpaka bar inatungwa tukaingia chumbani. Punde si punde mkojo wa bia huo. Nikatoka nikaenda chooni kule uwani kumbe na mteja mwingine nae alikua chooni. Mimi ilikua ndogo tu chap nikarudi yeye ilikua kubwa nikamuacha anaendelea kujikamua. Sasa nikasahau mlango wangu nikaingia kwake huku taa imezimwa lkn unaona kwamba kitanda Ni kile neti Ni ile na demu wake alikua uchi wa mnyama amekaa mkao wakuliwa kitandani (si unajua wanawake zetu wakilewa) wakati naendelea kuweka neti vizuri niingie njema ikaingia huku akihisi nataka niendelee na demu wake. Alooh. Mpaka kuja kuikomvinsi Ile njemba kwamba nilikosea chumba ilikua muda sana na aliniomba niende nae chumba changu akahakikishe kwamba na Mimi ninae demu wangu. Pombe zilinitoka hata sijui zilienda wapi.....
We ni kama vile ulifumaniwa ujue[emoji1787][emoji1787]

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Kesho yake pia nilikunywa ila kwa adabu zote na nilihakikisha hilo tukio halijirudii tena
Ila kuacha kabisa bado sijafikiria kabisa labda kupumzika tu kwa muda[emoji1787][emoji1787]

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
Haha kupumzika sawa. Hongera kwa kuwa na adabu juu ya pombe, ndivyo pombe inavyotaka.
 
Karibu na Pale Buguruni sokoni Kuna bar Fulani Ina guest house. Gesti yenyewe Ni zile za kiswahili chumba kulia chumba kushoto corridor Kati halafu bafu vyoo na vyumba vya short time kule uwani. Ile gesti ilikua na vyumba vinne kulia na vinne kushoto. Basi bwana tumeyapiga maji na bibie Fulani Kisha tukaamua tuchukue chumba kabisa mule mule. Tukaendelea na maji ya mende mpaka bar inatungwa tukaingia chumbani. Punde si punde mkojo wa bia huo. Nikatoka nikaenda chooni kule uwani kumbe na mteja mwingine nae alikua chooni. Mimi ilikua ndogo tu chap nikarudi yeye ilikua kubwa nikamuacha anaendelea kujikamua. Sasa nikasahau mlango wangu nikaingia kwake huku taa imezimwa lkn unaona kwamba kitanda Ni kile neti Ni ile na demu wake alikua uchi wa mnyama amekaa mkao wakuliwa kitandani (si unajua wanawake zetu wakilewa) wakati naendelea kuweka neti vizuri niingie njema ikaingia huku akihisi nataka niendelee na demu wake. Alooh. Mpaka kuja kuikomvinsi Ile njemba kwamba nilikosea chumba ilikua muda sana na aliniomba niende nae chumba changu akahakikishe kwamba na Mimi ninae demu wangu. Pombe zilinitoka hata sijui zilienda wapi.....
Hahaha nimecheka aisee😂😂😂
 
Ukweni ulikunywa/ulifakamia bia...
Hiyo kuzima na kupoteza memories ulikunywa pombe Kali.
Drink responsibly mkuu, pombe so mbaya Bali ubaya huja pale unapotaka kujifanya mbabe kwenye pombe na yenyewe haipendi dharau😆😆
zahma haiji kwa kupanga mkuu jambo la aibu humpata mtu bila kutegemea😀😀
 
Changamoto ni hiyo, family iko mbali na kituo changu cha kazi. Nikienda likizo hata unywaji wangu unakuwa wa kawaida sana. Nikirudi job inakuwa balaa. Ila so far hata nikiona pombe naona kawaida tu na siitamani. Nataka niamie makazi mapya kuepuka group langu la walevi.
Bora kubadilisha makazi maana kama ni hivyo huwezi leta mama maeneo hayo akajua chama atachoma sana mkuu
 
Mwaka 2000 nmeemda kijijini,
Nikaenda kijiji cha jirani jioni kumuaga demu/classmate wangu, pia nikitoka hapo nkamuage bibi angu maana kesho yake nilikua narudi dar, wakati nimekaa pale kwa rafiki angu (anauza duka lina vinywaji pia) napata 2 za kuzugia akaja rafiki yangu nae tulisoma wote balaa likaanzia hapo, ndani ya masaa 3 nimetia nyavuni safari 11, sababu nilikunywa haraka sikuziskia mida hiyo nkaaga saa 1 usiku,
Kutoka hapo hadi kwa bibi kama km3 hadi home km10 naa,
Nlafanikiwa kufika kwa bibi ili nimuage nkaambiwa hayupo kaenda kwenu, fasta nkawahi home, nilishtuka tu nipo mazingira ya home sijui hata nilifikaje maana sikumbuki hata nilipita njia gani.
Kufika home bibi wamekaa na mama jikoni wananisubiri nkashikilia frem ya mlango wa jiko ili nisianguke huku najifanya niko sawa, baaada ya salamu nkajifanya kuna kitu nafata nyumba kubwa nkawaza hapa lazima bibi asindikizwe adi kwake na hali hii sijui iltakuaje,
Akili ikanijia nikajitapishe nkafanya hivyo ndio ikawa salama yangu maana hali ilikua inazidi kubadilika kila mara.
 
Ulimsindikiza???
 
Hapa kama ninakiri!

Kitendo kilichonifanya kuacha kunywa pombe ni tukio la aibu nililolifanya miaka 30 iliyopita, lakini hadi leo bado linanibungua kichwa kwa aibu ile!

Miaka hiyo nilikuwa ninaishi 'kotaz' nyumba zenye kufanana kuanzia sura, rangi na mpaka mazingira ya nje.

Kimbembe kilipoanzia ni pale nilipotoka safari na kukuta 'ugeni' wa rafiki yangu wa siku nyingi kanitembelea hapo nyumbani.

Mahali gani pazuri pa kumpeleka 'outing' huyu ndugu akasuuze roho yake, hakuna pengine ni bar tu!

Sa9 alasiri tayari tupo kwenye meza ndefu tunakunywa, baada kama ya saa1 na nusu nikamuona mgeni wangu 'keshanitaimu' kalewa tayari mimi bado mkavu na bia hazinibambi, nikaona kama ananisanifu, sasa nifanyeje kufukia mashimo?

Wakati natafakari cha kufanya, nikaona mgeni wangu yupo chakari kabisa, nikaitisha tax ikampeleka nyumbani, mi nikabaki bar.

Bia zilivyoendelea kudunda nikaona niagize pombe kali nimix ili kupata ulabu kwa kasi, kumbe ninajitengenezea sumu!

Nikachukua viroba viwili vya 'power' (pombe ilikuwa inaingizwa toka Zambia)nikavimiminia kwenye chupa ya bia na kuanza kuifakamia.

Kumbukumbu zangu ndiyo zilipokomea hapo, yaliyofuata ni simulizi tu nilizokuja kusimuliwa bila mimi kukumbuka hata1.

Inaonekana ilipofika sa1 niliondoka bar kwa miguu kuelekea nyumbani, maana hapakuwa mbali sana.

Nilipofika, kwa kuwa nyumba zinafanana sana, nikakosea nikaingia nyumba kama yangu,lakini line ya mbele kabla sijafika kwangu.

Nilipofika nikaingia ndani na kupitiliza moja kwa moja chumbani kulala, wakati wenye nyumba wapo nje wanaongea!

Walipoingia wakakuta nimelala kitandani kwao na tayari 'shaharibu'.

Wakaenda kwa ghadhabu kumueleza 'wife' aje kunichukua, akakuta siamshiki wala sibebeki.

Njia iliyotumika kunitoa pale na kunipeleka kwangu pamoja na aibu yote niliyoifanya ndani ya nyumba hiyo na kwa familia hiyo, niliporudiwa fahamu na kusimuliwa, nilitamani dunia ipasuke inimeze!

Kwa unyenyekevu mkubwa, nikaiomba radhi familia hiyo na tangia hapo nikaacha pombe moja kwa moja mpaka takapokufa.
.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hahahahaaa itakua Mbeya hii....kota za wapi hizi mkuu
 
Ukweni ulikunywa/ulifakamia bia...
Hiyo kuzima na kupoteza memories ulikunywa pombe Kali.
Drink responsibly mkuu, pombe so mbaya Bali ubaya huja pale unapotaka kujifanya mbabe kwenye pombe na yenyewe haipendi dharau😆😆
Hakika mkuu pombe haitaki dharau, pombe inataka iheshimiwe 😂😂
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] noma sana
Enzi zile tuko sekondari wakati ule shule za sekondari Ni adimu Kama kumuona paka akijamiiana. Kule Mbeya tukifunga shule tulikua tunajitenga na vijana wengine. Basi Xmas moja tukaamua tuchange tununue pombe kwa ajili ya sikukuu ili tunywe na mademu wetu wanaosoma sekondari kumbuka tulikua hatujichanganyi na ma loko. Hela ilichangwa na pombe ikanunuliwa siku ya mkesha kusubiri sikukuu kesho yake. Pombe Ile kimpumu ambayo bado ilikua kwenye process ya kuiva tukaihifadhi kwenye gheto la mwenzetu mmoja mnyakyusa wa tukuyu Kisha kila mtu akaenda kwao kulala. Yule mnyakyusa akaona atapunjika akisubiri mpaka timu ikikamilika hivyo anywe kidogo. Basi bwana, glasi moja huanzisha nyingine halafu mnajua pombe ambayo haijaiva vizuri inavyowafanya watu wasio wazoefu wa pombe. Dogo alikunywa akalewa akapoteza network kuanzia 24/12 mpaka 26/12.
Ameamka Xmas imeisha na demu wake kachukuliwa na mtu mwingine.
 
Back
Top Bottom