Visa gani pombe ilikufanyia hutasahau?

Visa gani pombe ilikufanyia hutasahau?

Kule sawa

Kule sawa hapa sio[emoji6] Alafu last week ulizingua but it was ok with me. Smirnoff nilikuwa nazipenda ila sasa kwa pombe kali napiga Magic moment of any taste kama nikiikuta hapo mahali. Haiumizi kichwa wala haikupi hang over wala haiumizi kichwa.
Hivi smirnoff beer bado ipo kweli?
We lazima utakua una matukio sana kama unapiga magic moment

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Nikiri na niweke wazi, pombe sio mbaya endapo ukiitumia kwa nidham, ila ikitumika kwa upuuzi ni batili kabisa, Alhamisi iliopita nimeenda kutoa mshahara wa magu nikasema wacha nichukue laki mbili tu inatosha kwa matumizi, wife alikua safarini.
Sasa nilikua na deni la miez miwili nilikunywa urabu sehem moja ninayoaminika sana 36k, nilipolipia ndio nikaanza urabu kiasi chote cha pesa mfukoni nilichokua nacho nikakimaliza kwa mda mfupi tu kwani nilijikuta nimearika marafiki kama wanne na niliwahakikishia kula na kunywa.
Kutoka apo kichwa imewaka kila mashine ATM nilioiona nilitoa hela na kuwanunulia pombe whuni, ata nisiowajua so mpka kufika jumamosi jion ninetumia 700k , kilichoniokoa ni kufuatwa na wife baada ya kifika toka safari, na kukuta siko home, alipopiga simu nilimtajia kiwanja nilichopo. Niko ndani leo siku ya tatu nimeomba ruhusa kazini kila nikijitafakari najiona sina amani ya moyo na mie kipato changu sio cha kutumia pesa hio bila kujutia. Nineweka mkakati wa kuacha pombe na ninaomba kuanzia hapa wenye nia wenzangu tuunde group la kupeana mikakati na mabadiliko ya kweli mim naiona pombe basi
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Hapa kama ninakiri!

Kitendo kilichonifanya kuacha kunywa pombe ni tukio la aibu nililolifanya miaka 30 iliyopita, lakini hadi leo bado linanibungua kichwa kwa aibu ile!

Miaka hiyo nilikuwa ninaishi 'kotaz' nyumba zenye kufanana kuanzia sura, rangi na mpaka mazingira ya nje.

Kimbembe kilipoanzia ni pale nilipotoka safari na kukuta 'ugeni' wa rafiki yangu wa siku nyingi kanitembelea hapo nyumbani.

Mahali gani pazuri pa kumpeleka 'outing' huyu ndugu akasuuze roho yake, hakuna pengine ni bar tu!

Sa9 alasiri tayari tupo kwenye meza ndefu tunakunywa, baada kama ya saa1 na nusu nikamuona mgeni wangu 'keshanitaimu' kalewa tayari mimi bado mkavu na bia hazinibambi, nikaona kama ananisanifu, sasa nifanyeje kufukia mashimo?

Wakati natafakari cha kufanya, nikaona mgeni wangu yupo chakari kabisa, nikaitisha tax ikampeleka nyumbani, mi nikabaki bar.

Bia zilivyoendelea kudunda nikaona niagize pombe kali nimix ili kupata ulabu kwa kasi, kumbe ninajitengenezea sumu!

Nikachukua viroba viwili vya 'power' (pombe ilikuwa inaingizwa toka Zambia)nikavimiminia kwenye chupa ya bia na kuanza kuifakamia.

Kumbukumbu zangu ndiyo zilipokomea hapo, yaliyofuata ni simulizi tu nilizokuja kusimuliwa bila mimi kukumbuka hata1.

Inaonekana ilipofika sa1 niliondoka bar kwa miguu kuelekea nyumbani, maana hapakuwa mbali sana.

Nilipofika, kwa kuwa nyumba zinafanana sana, nikakosea nikaingia nyumba kama yangu,lakini line ya mbele kabla sijafika kwangu.

Nilipofika nikaingia ndani na kupitiliza moja kwa moja chumbani kulala, wakati wenye nyumba wapo nje wanaongea!

Walipoingia wakakuta nimelala kitandani kwao na tayari 'shaharibu'.

Wakaenda kwa ghadhabu kumueleza 'wife' aje kunichukua, akakuta siamshiki wala sibebeki.

Njia iliyotumika kunitoa pale na kunipeleka kwangu pamoja na aibu yote niliyoifanya ndani ya nyumba hiyo na kwa familia hiyo, niliporudiwa fahamu na kusimuliwa, nilitamani dunia ipasuke inimeze!

Kwa unyenyekevu mkubwa, nikaiomba radhi familia hiyo na tangia hapo nikaacha pombe moja kwa moja mpaka takapokufa.
.


Sent using Jamii Forums mobile app
Kaka. Hii funga kazi......
 
dah! aisee nimesoma comments zote toka mwanzo mpaka uzi ulipofikia sasa, cha umuhimu ni kuwapa pole tu wahanga wa uraibu huu, mungu awasimamie muweze kuacha ..
Kuacha bila health complications and doctors' consultations ni ngumu, wengi wanapumzika alafu baadae wanarudi tena chamani 😊
 
Hii kitu ni mtakuja mkuu, jamaa yangu aliweza kuacha kwa mwaka, aliporejea ilikuwa ni balaa zaidi ya alivyokuwa mwanzo, ila kama unasali pia basi uwezo wa kumantain ni mkubwa japo siyo rahisi hata kidgo
Usimkatishe, tuliofanikiwa kupiga chini hatukuwa wanywaji tulikuwa walevi

Mwaka wa tano huu, mwaka jana nikagusa siku moja kwa kuwa sijakunywa muda mrefu nikalewa sana nikapiga chini tena

Kwahiyo nimefanikiwa kuichezea navyotaka sio yenyewe kunichezea

Hata kama hataacha mazima hatakuwa mnywaji wa kutupwa

Ili afanikiwe ni lazima awe anakumbuka majanga yake kila anapopata hamu
 
Enzi zile tuko sekondari wakati ule shule za sekondari ni adimu Kama kumuona paka akijamiiana. Kule Mbeya tukifunga shule tulikua tunajitenga na vijana wengine. Basi Xmas moja tukaamua tuchange tununue pombe kwa ajili ya sikukuu ili tunywe na mademu wetu wanaosoma sekondari, kumbuka tulikua hatujichanganyi na ma loko.

Hela ilichangwa na pombe ikanunuliwa siku ya mkesha kusubiri sikukuu kesho yake. Pombe Ile kimpumu ambayo bado ilikua kwenye process ya kuiva tukaihifadhi kwenye gheto la mwenzetu mmoja Mnyakyusa wa Tukuyu Kisha kila mtu akaenda kwao kulala. Yule mnyakyusa akaona atapunjika akisubiri mpaka timu ikikamilika hivyo anywe kidogo. Basi bwana, glasi moja huanzisha nyingine halafu mnajua pombe ambayo haijaiva vizuri inavyowafanya watu wasio wazoefu wa pombe. Dogo alikunywa akalewa akapoteza network kuanzia 24/12 mpaka 26/12.

Ameamka Xmas imeisha na demu wake kachukuliwa na mtu mwingine.
 
Nikinywa naaanza kulia
Hahaha umenikumbusha rafiki yangu mmoja hivi yaani kama mmekaa nae hakikisheni bia ya nne hafikishi maana ataanza kwanza kuimba nyimbo za kihindi za miaka 1980's atakumbuka movies zake zile zenye kugusa hisia sasa akianza kulia hapo hakuna wakumzuia. Tunachofanyaga ni kumnyamazisha, akigoma huwa tunateleza mmoja mmoja na kumuacha peke yake na maneno yake ya kulaumu watu wenye pesa wanavyonyanyasa masikini.
Neno lake kubwa "The world is not fair na The law is blind"
Nimekukumbuka Mr. The law is blind😉😊
 
Hii kitu ni mtakuja mkuu, jamaa yangu aliweza kuacha kwa mwaka, aliporejea ilikuwa ni balaa zaidi ya alivyokuwa mwanzo, ila kama unasali pia basi uwezo wa kumantain ni mkubwa japo siyo rahisi hata kidgo
Mimi nawafahamu watu wengi tu(marafiki/ndg) waliikua ni wao na pombe lkn waliacha ndani ya siku 1 tu na mpk sasa wengine wana miaka zaidiya 10 na hawajawahi kuigusa tena na wala sio walokole wala nini.

Mimi binafsi ninapiga maji sana tu lkn nikiamua nakaa hata miezi 4 pombe sigusi na bar naenda fresh tu.
 
Mimi nawafahamu watu wengi tu(marafiki/ndg) waliikua ni wao na pombe lkn waliacha ndani ya siku 1 tu na mpk sasa wengine wana miaka zaidiya 10 na hawajawahi kuigusa tena na wala sio walokole wala nini.

Mimi binafsi ninapiga maji sana tu lkn nikiamua nakaa hata miezi 4 pombe sigusi na bar naenda fresh tu.
Hongera kwakuwa na hiyo nguvu ya maamuzi juu ya pombe. Au kuna mbadala mzee baba?
 
Mkuu huu uzi umenifanya naelekea kukata mwezi bila kugusa hata tone moja la pombe, yaani naamka kichwa hiko sawa napiga kazi zangu poa kabisa. Wiki ya mwisho kabla sijaacha nilikwenda kuhudhuria semina mahali fulani nimechoka mbaya kwa pombe za jana yake. Muda wa chai najipanga foleni nachukua kikombe cha maziwa n supu kushika tu robo ya maziwa ikaishia chini. Natetema mikono balaa, muda wa kusaini posho nikashindwa hata kutia saini nikachoronga tu nikasepa. Tangu nimeacha ( kama nitaweza kweli ku maintain) najiona kama nimezaliwa upya. Nilikuw nikiangalia TV naogopa naona kama wale watangazaji wananikodolea macho. Hata kijiko tu kikidondoka nashtuka balaa. Naushukuru huu uzi ulinitia moyo sana haswa comments za wadau.
utatoboa tu maintain hivyo hivyo pole pole na kingine kama una family basi tumia muda mwingi hapo unapotoka kwenye mitikasi yako
nunua hata ka playstation wakati huo kaimu wako anaanda hata chai utamaliza kabisa
 
emoji3.png
emoji3.png
emoji3.png
😀
 
kisa cha kwanza nilikuwa na bro tukaenda ukweni kwake alikuwa anataka kuvuta jiko lake basi kabla ya kufika akaona tupandishe ujasiri na beer Kibo sa 2x2,Kufika ukweni tukapata tunangojewa kwa shangwe shughuli ikaenda vizuri tu
tukaendelea kujirudishia shukrani pale ukweni ilipofika maji ya shingo kwakuwa sikuwa mzoefu wa unywaji nikarudisha chenji pale ukweni kwa bro kwakweli hili liliniumiza sana leo na kesho
Kisa kingine ni kunywa na kesho yake sina memory yoyote kujua nilikula wapi,nilikunywa nini na home nimerud vp naamka najikuta home tu lakini sijui nilirudi vp imetokea kama tatu,nikaona itakuja niletea maafa nikaamua kupumzika ni mwaka saa
NOTE; kama ni mnywaji usinywe ukweni kabisa wakuu wakwe wanaweza kukujazia meza na ikawa kipimo cha kukupa binti yao bana😀
 
Back
Top Bottom