Yuko jamaa yangu mtu msomi vizuri tu tatizo anatokea kwenye kabila lenye misifa. Siku moja nilimkaribisha kinywaji pale 92 Sinza. Wakongwe mnapakumbuka miaka Ile palikua na gesti pia.
Tulianza vizuri tu Mara akaja mchekopuko wangu na rafiki yake(sasa hv mke wa mtu Tena mheshimiwa) baasi mie nikamchukua mchepuko wangu chobingo na kumpa laki na kumwambia pombe anunue yeye ili kulinda heshma yake kwa rafiki yake. Basi mchepuko wangu akaawaita wa jikoni na kuagiza mchemsho, mbuzi choma na kuku Kisha akalipa kabisa kumuonyesha jamaa yangu kuwa anazo. Kisha mvua ya bia ikaanza. Bwana misifa kila akitaka kuagiza ili kujitutumua mchepuko wangu anakua Kesha agiza bia. Sasa pale tuko wanne Mimi, mchepuko, misifa na rafiki wa mchepuko. Misifa akaona rafiki wa mchepuko Ni halali yake yaani alijimilikisha bila kutongoza kumbe anajipalilia Moto. Baada ya kula nyama nyingi, michemsho na mikuku mchepuko akasema twende kwake tukapate mbili mbili Kisha tuachane kila mtu aende kwake. Misifa hakupenda kuachwa nyuma alihisi labda anaweza kupata chance ya kununua bia ili amu impress rafiki wa mchepuko. Kufika nyumbani kwa mchepuko jirani kabisa na shule ya Mugabe mchepuko akawa amempa signal mama mwenye glossary ya jirani kwamba alete mvua ya bia. Zilipofika kabla misifa hajaingiza mkono mfukoni mchepuko akalipa kabisa. Basi kazi ikawa Ni moja tu. Kugida bia huku kila mtu amekaa sanjari kabisa na mwenza wake, Mimi na mchepuko na misifa na rafiki wa mchepuko, misifa alikua anajua lazima amvue nguo yule rafiki wa mchepuko. Punde si punde misifa akapitiwa na usingizi wa pombe na kulala kidogo kwenye Kochi. Rafiki wa mchepuko alivyoona jamaa amechoka nae huyoo akaondoka kwenda kwake huku misifa anakoroma kwenye Kochi ilhali ana mke aliyemuoa toka Kanda ya ziwa majuzi juzi tu. Mimi na mchepuko tukaingia chumbani na kujipunzisha huku kwenye Kochi misifa anangorota Kama trekta linalopukuchua mahindi. Kufika asubuhi nikamstua misifa aache ujinga, aamke awahi kwa mkewe mbichi mwenye miguu ya bia na lafudhi ya kamachumu.
Misifa kustuka akagundua amelala kwenye Kochi, rafiki wa mchepuko hakumpata na hakulala kwake. Kutoka pale misifa alipotoka kufika barabarani akaona gari ya polisi enzi zile tunayaita tetracycline. Akawaambia wale maaskari wajifanye wamemkamata halafu wampeleke kwake na wampige hata makofi mawili halafu wasachi nyumbani kwake Kama vile amefanya uhalifu fulani. Basi misifa akawakatia pochi polisi na kuwaambia wakifika home atawaongeza mbele ya mkewe. Polisi wetu wape dili la pesa na utajua wamepitia ccp Moshi. Misifa akapigwwa pingu na kupelekwa kwake muda huo yapata saa tatu asubuhi kumbuka enzi zile hakuna simu. Polisi wale kufika nyumbani kwa misifa wakamteremsha kwenye gari na kumwambia akawaonyeshe hiyo Mali ya magendo ilipo, mmoja akamlima Kofi mbili za keleb, misifa akajitetea Hana Mali ya magendo na polisi wakasachi uongo na kweli, Toto la kamachumu lilivyoona mumuwe aka misifa anazidi kudhalilika mbele ya majira akamuita polisi mmoja chocho na kumpa mlungula ili wamwache misifa. Basi pingu zikafunguliwa na misifa akaingia ndani na polisi kuondoka huku wakitabasamu na kijino pembe.
Itaendelea.......