Visa gani pombe ilikufanyia hutasahau?

Visa gani pombe ilikufanyia hutasahau?

Wiki ya tatu naenda ya nne sasa sijagusa. Najiona mtu tofauti sana, siku 3 za mwanzo zilikuwa ni mtihani kweli kweli kidogo nirudi kupiga maji. Sijui nitamaintain kwa muda gani ila nimedhamiria iwe jumla.
Mkuu hiyo ni hatua kubwa sana. Leo jioni twende tukajipongeze samaki samaki
 
Wiki ya tatu naenda ya nne sasa sijagusa. Najiona mtu tofauti sana, siku 3 za mwanzo zilikuwa ni mtihani kweli kweli kidogo nirudi kupiga maji. Sijui nitamaintain kwa muda gani ila nimedhamiria iwe jumla.
Amen Amen nategemea updates zaidi

Hata kama hutaacha kabisa lakini ukipiga mara moja ukazima ukatulia miezi au mwezi si mbaya

Sio sawa na kuzima daily unapoteza vingi, Afya, Heshima na pesa

Unazungumzia kutetema mikono naelewa unachozungumza niliwahi kufikia stage hiyo, bahati mbaya kazi yangu ni ya kuandika sana, ikija kazi nakosa amani, nazunguka zunguka tu huku na huko mradi hiyo kazi afanye mwingine mimi siwezi kabisa

Kuna dada nilimuonyesha huu uzi akaanza kunishuhudia jinsi mwanaume wake anateswa na uraibu wa pombe kwa kweli mpaka nilidhani ni wewe ila kuna vitu ni tofauti kidogo

Huyo mwenzio(mwanaume wa huyo dada) nafikiri anakuzidi parefu sana ikiwa umeshaandika yote hapa

Yeye alipelekwa mpaka sober alipotoka tu akarudishwa nyumbani na mkokoteni ameokotwa siku hiyo hiyo

Bidada amekata tamaa ameachana nae na anadhani kwa jamaa alipofikia hana muda anafariki

Mungu atakusaidia mkuu uraibu wa aina yoyote ni mbaya sana unatesa mhusika mpaka watu wa karibu
 
Shukrani mkuu, nitajitahidi sana kwani majanga niliyopitia ni mengi mno. Nina mikasa kibao sijaiweka humu na muda huu niliokaa bila kugusa nakumbuka nyuma na ninasikitika sana na sitaki niendelee kukumbuka. Nilipoteza vingi kama ulivyotaja hapo. Naukumbuka msemo mmoja toka kitabu kimoja cha J.H. Chase usemao "If you live for the past, you bring sorrow to yourself" wacha niyasahau tu maisha yasonge mbele.
 
Kwamba ungeenda?[emoji3][emoji3]
Hata huku niliko nakaa na washikaji seemu za starehe na wanakunywa na ninawanunulia pia. Mimi sasa ni Pepsi na Grand malta tu. Nimeona nisijifiche bali niwe mazingira niliyozoea.
 
Siku ingine nilifakamia sana pombe mchanganyiko nilikuwa na binamu yangu wakati tunaondoka tupo ndani ya daladala mimi tu ndo nilikuwa muongeaji watu wote vicheko. Tuliposhuka nikawa naenda njia ambayo sio binamu yangu akaniita.

Tulipofika nyumbani nikasema ngoja nikanywe ya mwisho wakati narudi nikapotea tena nyumbani nikashtuka kuwa nimepotea nyumba baada ya kuona sifunguliwi mlango.
Mlevi hapotei njia ya nyumbani
 
Shukrani mkuu, nitajitahidi sana kwani majanga niliyopitia ni mengi mno. Nina mikasa kibao sijaiweka humu na muda huu niliokaa bila kugusa nakumbuka nyuma na ninasikitika sana na sitaki niendelee kukumbuka. Nilipoteza vingi kama ulivyotaja hapo. Naukumbuka msemo mmoja toka kitabu kimoja cha J.H. Chase usemao "If you live for the past, you bring sorrow to yourself" wacha niyasahau tu maisha yasonge mbele.
Wala usikae kufikiria ya nyuma hatuishi muda uliopita maisha lazima yaendelee

Lakini sikushauri sana kupendelea kukaa baa maana bado hujaimarika kiimani

Usiogope eti nani atasema unamtenga au unajifanya kubadilika(mimi nilikuwa naambiwa anajifanya ameacha atarudi tu/anatutenga anatuona walevi wakati yeye alikuwa mlevi tu) kwa sababu hatuishi maisha ya watu wengine

Ulipopata majanga yalikusibu wewe peke yako pia na mustakabali wako ni wako peke yako
 
Hapo umenena, ni kujaribu kutengeneza marafiki wapya wenye mwelekeo wangu na pia kupunguza kuwa maeneo hayo. Kuna wakati wanavunja moyo sana kwa kauli zao za kejeli.
 
Pombe haiachwi kirahisi rahisi hivyo [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Mwambie huyo mwamba, anadhani pombe ni kama soda kuwa hata ukikaa mwaka huwezi imis, pombe siyo mchezo kuiacha kunataka ujitoe kweli na urudi kwa Mungu. Toka miaka hiyo unaipiga alafu leo uamke na kuipa taraka kirahisi rahisi tu, hapo ni mtakuja tu
 
Mwaka 2008, Nilikuwa Mbeya Tukuyu Kikazi, Nilikuwa nimetokea Mbeya Mjini ambapo Kuna baridi, Dose yangu ilikuwa Tusker Kumi,
View attachment 1614054

Kwenda Tukuyu Nikaendelea na dose ileile bila kugundua kuwa Hali ya hewa ya Tukuyu Ni Tofauti na Mbeya Mjini. Na Pombe. Hukolea kwenye Joto, Tukuyu Kuna Joto.

Mzee Mzima Nikavesha Kama kawaida, mpaka saa tano FULANI hivi, Sasa kimbembe Nikasahau Guest, Nikaenda kugonga Nyumba ambayo Inaangaliana na Guest Huku Povu likinitoka kwanini wafunge na Mimi bado sijarudi.

Ebwana mlango ulifunguliwa na Mbaba mmoja akiwa na njemba tatu (Watoto wake) Nilichezea vitasa vyakutosha kila nikiweka Gurd wapi.

Niliokolewa na Staff wenzangu Baada ya kuhisi kuwa sijarudi na wanasikia kelele za sauti yangu.

Asee hiyo ilikuwa moja Ila Pombe kuacha bado nafikiria.
Aisee[emoji2][emoji2][emoji2]

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Juzi juzi tu hapa nimepanda daladala sayansi kijitonyama na jamaa amelewa saa 6 mchana jua kali,
tumetoka pale tunaelekea mwenge tumefika adi mataa pale mwenge anamwambia konda amuache sayansi na wakati alipopandia gari ndo sayansi[emoji23][emoji23]
Hahahahahaha

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Wiki ya tatu naenda ya nne sasa sijagusa. Najiona mtu tofauti sana, siku 3 za mwanzo zilikuwa ni mtihani kweli kweli kidogo nirudi kupiga maji. Sijui nitamaintain kwa muda gani ila nimedhamiria iwe jumla.
Hii kitu ni mtakuja mkuu, jamaa yangu aliweza kuacha kwa mwaka, aliporejea ilikuwa ni balaa zaidi ya alivyokuwa mwanzo, ila kama unasali pia basi uwezo wa kumantain ni mkubwa japo siyo rahisi hata kidgo
 
Hapa kama ninakiri!

Kitendo kilichonifanya kuacha kunywa pombe ni tukio la aibu nililolifanya miaka 30 iliyopita, lakini hadi leo bado linanibungua kichwa kwa aibu ile!

Miaka hiyo nilikuwa ninaishi 'kotaz' nyumba zenye kufanana kuanzia sura, rangi na mpaka mazingira ya nje.

Kimbembe kilipoanzia ni pale nilipotoka safari na kukuta 'ugeni' wa rafiki yangu wa siku nyingi kanitembelea hapo nyumbani.

Mahali gani pazuri pa kumpeleka 'outing' huyu ndugu akasuuze roho yake, hakuna pengine ni bar tu!

Sa9 alasiri tayari tupo kwenye meza ndefu tunakunywa, baada kama ya saa1 na nusu nikamuona mgeni wangu 'keshanitaimu' kalewa tayari mimi bado mkavu na bia hazinibambi, nikaona kama ananisanifu, sasa nifanyeje kufukia mashimo?

Wakati natafakari cha kufanya, nikaona mgeni wangu yupo chakari kabisa, nikaitisha tax ikampeleka nyumbani, mi nikabaki bar.

Bia zilivyoendelea kudunda nikaona niagize pombe kali nimix ili kupata ulabu kwa kasi, kumbe ninajitengenezea sumu!

Nikachukua viroba viwili vya 'power' (pombe ilikuwa inaingizwa toka Zambia)nikavimiminia kwenye chupa ya bia na kuanza kuifakamia.

Kumbukumbu zangu ndiyo zilipokomea hapo, yaliyofuata ni simulizi tu nilizokuja kusimuliwa bila mimi kukumbuka hata1.

Inaonekana ilipofika sa1 niliondoka bar kwa miguu kuelekea nyumbani, maana hapakuwa mbali sana.

Nilipofika, kwa kuwa nyumba zinafanana sana, nikakosea nikaingia nyumba kama yangu,lakini line ya mbele kabla sijafika kwangu.

Nilipofika nikaingia ndani na kupitiliza moja kwa moja chumbani kulala, wakati wenye nyumba wapo nje wanaongea!

Walipoingia wakakuta nimelala kitandani kwao na tayari 'shaharibu'.

Wakaenda kwa ghadhabu kumueleza 'wife' aje kunichukua, akakuta siamshiki wala sibebeki.

Njia iliyotumika kunitoa pale na kunipeleka kwangu pamoja na aibu yote niliyoifanya ndani ya nyumba hiyo na kwa familia hiyo, niliporudiwa fahamu na kusimuliwa, nilitamani dunia ipasuke inimeze!

Kwa unyenyekevu mkubwa, nikaiomba radhi familia hiyo na tangia hapo nikaacha pombe moja kwa moja mpaka takapokufa.
.

Sent using Jamii Forums mobile app
Dah kweli pombe sio chai

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Hii kitu ni mtakuja mkuu, jamaa yangu aliweza kuacha kwa mwaka, aliporejea ilikuwa ni balaa zaidi ya alivyokuwa mwanzo, ila kama unasali pia basi uwezo wa kumantain ni mkubwa japo siyo rahisi hata kidgo
Nimewahi kuacha mara kadhaa na nikarudi, safari wacha tena nijaribu mkuu. Nitakapoishia hapo hapo.
 
dah! aisee nimesoma comments zote toka mwanzo mpaka uzi ulipofikia sasa, cha umuhimu ni kuwapa pole tu wahanga wa uraibu huu, mungu awasimamie muweze kuacha ..
 
Back
Top Bottom