Visa gani pombe ilikufanyia hutasahau?

Visa gani pombe ilikufanyia hutasahau?

As a matter of fact gambe is nice, almradi uwe na discipline nayo.......displine, kama hiyo ya kwako unaweza kukaa mwaka na nusu bila kuonja..hahahahah. Hiyo Ni beyond discipline kwa kweli.
Ukiindekeza tu umeisha asee
 
Hahahaha......Huyu mzee atakuwa alikuwa anaheshimika sana, isingekuwa rahisi kuongelea maisha yake binafsi. Public figure!
Na atabaki kuwa the public fugure vizazi na vizazi kama vile Yuda anavyowakilisha usaliti. Sipati picha kama Yuda angekuwa anakunywa pombe kisirisiri hali ingekuwaje😂😂
 
Visa vyangu ni lukuki, miaka ya 2000 nilisafiri toka mkoa niliokuwepo nikaenda Mkoa wa mara (Musoma mjini). Rafiki yangu wa karibu sana alikuwa anafunga ndoa, sherehe ikafanyika pale Musoma hotel. Nilikunywa pombe nazinduka nimelala ufukweni mwa ziwa victoria tena asubuhi kabisa vitu vyangu vyote ninavyo. Usiku baada ya sherehe wamenitafuta wakashindwa kujua nilikokwenda. Nikarudi nilikofikia bila kuwasimulia kilichonikuta
[emoji1][emoji1][emoji1] hapo pombe inasema kichwani uko lodge lala nyumban utaenda asubuhi
 
Sio mwanachu huyo. Ni mdangaji fulani tu yuko Kigoma. Hiyo boti anayoongelea ilikua iko ziwa Tanganyika.
Aisee ningeshangaa...mwanachuo kabisa tena analipwa 3.7M hajui hata namna Offer inavyoandikwa
 
Pumbav kabisa. Chuoni sikwenda kujifunza kuandika majina ya nchi. Hata hivo umeelewa. Halafu shika adabu yako nina kazi nzuri na ninalipwa 3.7mil mm sio level yako
Naona mshahara umepanda ghafla
 
Gambe inanipa fedhea Sana mtaani ..yani nikilewa nakua na furaha Sana mixer kurap ,kuongea Sana ,kesho yake balaaa hangover , uzuni moyoni, najiona mkosaji Sana , nikipishana na mtu tu akanisalimia kwa kunichangamkia najua tayari hapo anakupunga chenga zaku za ulevi
 
Ngoja niweke mkasa wangu mwingine ulitokea 2004, Jamaa zangu walitoka mgodini wana hela ya maana wamekuja na mshikaji wao watupambanishe kunywa pombe wanajua mimi kichwa ngumu kwenye bia. Nikawapa masharti kuwa nakunywa bia na si pombe kali. Wakaleta kreti moja ya Tusker na jamaa akapewa yakwake hiyo ni saa mbili asubuhi tumeshakula ugali kwa supu ya samaki. Kufika saa saba nimemaliza kreti jamaa kachemsha. Nikaaga nikaenda kulala, nakuja kushtuka kesho yake mchana majirani wanabomoa mlango wakijua nimekufa. Walichungulia dirishani wanaona mtu kalala chini wakajua nishaenda kwa Sir God. Niliugua siku 3 sijiwezi kabisa.
[emoji849][emoji849][emoji849][emoji849]
 
Back
Top Bottom