Visa gani pombe ilikufanyia hutasahau?

Visa gani pombe ilikufanyia hutasahau?

"Hata kama ni maisha yako, ndo unywe bia na chapati ??" - haji manara
 
Sita sahau siku hiyo nimekunywa pombe badala ya kwenda Lumumba aisee nikaelekea pale ufipa tena nakumbuka nilimkuta mwenyekiti wao na makamu wake.

Ila kwa bahati nzuri sijui mbaya nao walikuwa washazitwika tani yao.
🤣🤣🤣🤣
 
Nikiwa nimepanga Temeke, majirani zangu walikuwa wakishakunywa pombe zao dah! Unajua tena nyumba ya kupanga lakini wao wakishalewa unakuta mtu kwa kisingizio cha pombe anaingia chooni na kuharisha na kueneza chooni kote, kibaya zaidi hata kujitawaza hakumbuki na wala kusafisha kule alikotapakaza kinyesi hakumbuki, then najikuta labda usiku wa manane ndio nimebanwa haja, mtu unaingia toilet unakuta kuko nyang'anyang'a. Yaani ile hakufai kabisa halafu kinyesi kishakauka [emoji2817][emoji2817][emoji2817]
Walevi muda mwingine mnaboa bana!!
Hii sio pombe, niujinga
 
Hawa

Aliwahi kutokea muuaji mmoja wa bunduki pale Tarime, Hawa jamaa zangu wakawa miongoni wa waliopigwa risasi na kufariki.
Njemba inaitwa KENONKE. Yule jamaa alikuwa anaua kisha hachukui hata mia mbovu
 
Mojawapo aliharibikiwa na gari usiku akampigia mwenzake akamsaidie. Mdunguaji akapita nao, na waliwahi kufanya kazi sehemu miaka ya nyuma
Hii ilifanya watu wasisafiri usiku. Jamaa alipita kama anawasaidia, akawaua. Fundi alikuwa uvunguni mwa gari na ndiye aliyeelezea kisa chote maana kwa bahati yeye hakuonekana.
 
Amini kwamba kama wewe ni msafi hata ukilewa hauwezi kufanya upuuzi huo, na iwapo utajijua kuwa ukilewa unafanya mambo ya ajabu lazima utajizuia kwasababu ya aibu
Na ndio maana pombe ni haramu hakuna usafi ndani ya pombe! Pombe ni mama wa maasi.
 
Nashukuru Mungu situmii ulabu japo nishapitia mazingira yanayoshawishi matumizi ya pombe. Majuzi kuna dada flani rafiki yangu alinipa nionje kidogo, funda moja la imagi lilinishinda kumeza, nikabaki kuburudika na twist passion yangu😂😂😂😂😂
 
Hukuna mganga wala tiba ya kuacha pombe,Nimeenda sana kwa waganga na dawa nimekunywa za kuacha,..wapi, naandika sahivi nimegonga lite mbili'

Kama ulivyoanza kunywa hujaenda kwa mganga uanze kunywa, ndio inavyotakiwa uache.

Period
 
Na walifanya kazi pamoja mgodi wa Nyamongo, SAM nilisoma naye kitambo alikuwa mshikaji wangu sana na ndio walioweka pambano la pombe.
 
Back
Top Bottom