Nakumbuka tukiwa chuo mshkaji wangu akaniambia tukastue akili kijijini ,tukapiga mbege chubuku mbili+konyagi kubwa sasa tukawa tumeishiwa ikabidi tuwe tunapiga debe watu waingie kwenye hice, gari ikajaa tukamzidi konda akili akatulia kama abiria wengine huku sisi tumedandia mlangoni tunazinguana na mshkaji wangu watu kwenye gari nikucheka tuu ,tukafika tunaposhuka tukaondoka konda anaseme nyie wahuni nyie nlijua tuu Hamna nauli,hapo tunalekea kwa jamaa wa masters alituambia tukachinje mbuzi kufika tukalianzisha tungi tena tukachinja tukachoma nikakomaa nikachkua kichwa cha mbuzi nkasepa nacho hiyo ni mida ya saa tano usiku geto ni mbali kidogo kuulizia bodaboda ni elfu 7,nikaona ujinga huu bora niende mdogomdogo huwezi amini nilifika mahali nikasikia mbwa wanabweka mbaya kabisa kugeuka nyuma mbwa kama mia hivi wanataka ile kichwa ya mbuzi mbaya zaidi hamna hata jabali ikabidi nivurumishe ile kichwa chini vumbi likatimka nkaona mbwa wanakimbia na Mimi nikawatolea uchovu nikaanza kuwatimua hapo fungi limekata kufika homu mikono imechubuka kesho yake nkamwambia dogo kuna kichwa ya ndafu kwenye mfuko set supu dogo ananiambia umekiokota wapi mbona kina vumbi hivi kweli kucheki utafkiri mzoga ikabidi kiundwe Kibishi ,baada yakumweleza kilichonisibu......ila kuacha siwezi huwa nainjoi haya matukio sana