Hapa kama ninakiri!
Kitendo kilichonifanya kuacha kunywa pombe ni tukio la aibu nililolifanya miaka 30 iliyopita, lakini hadi leo bado linanibungua kichwa kwa aibu ile!
Miaka hiyo nilikuwa ninaishi 'kotaz' nyumba zenye kufanana kuanzia sura, rangi na mpaka mazingira ya nje.
Kimbembe kilipoanzia ni pale nilipotoka safari na kukuta 'ugeni' wa rafiki yangu wa siku nyingi kanitembelea hapo nyumbani.
Mahali gani pazuri pa kumpeleka 'outing' huyu ndugu akasuuze roho yake, hakuna pengine ni bar tu!
Sa9 alasiri tayari tupo kwenye meza ndefu tunakunywa, baada kama ya saa1 na nusu nikamuona mgeni wangu 'keshanitaimu' kalewa tayari mimi bado mkavu na bia hazinibambi, nikaona kama ananisanifu, sasa nifanyeje kufukia mashimo?
Wakati natafakari cha kufanya, nikaona mgeni wangu yupo chakari kabisa, nikaitisha tax ikampeleka nyumbani, mi nikabaki bar.
Bia zilivyoendelea kudunda nikaona niagize pombe kali nimix ili kupata ulabu kwa kasi, kumbe ninajitengenezea sumu!
Nikachukua viroba viwili vya 'power' (pombe ilikuwa inaingizwa toka Zambia)nikavimiminia kwenye chupa ya bia na kuanza kuifakamia.
Kumbukumbu zangu ndiyo zilipokomea hapo, yaliyofuata ni simulizi tu nilizokuja kusimuliwa bila mimi kukumbuka hata1.
Inaonekana ilipofika sa1 niliondoka bar kwa miguu kuelekea nyumbani, maana hapakuwa mbali sana.
Nilipofika, kwa kuwa nyumba zinafanana sana, nikakosea nikaingia nyumba kama yangu,lakini line ya mbele kabla sijafika kwangu.
Nilipofika nikaingia ndani na kupitiliza moja kwa moja chumbani kulala, wakati wenye nyumba wapo nje wanaongea!
Walipoingia wakakuta nimelala kitandani kwao na tayari 'shaharibu'.
Wakaenda kwa ghadhabu kumueleza 'wife' aje kunichukua, akakuta siamshiki wala sibebeki.
Njia iliyotumika kunitoa pale na kunipeleka kwangu pamoja na aibu yote niliyoifanya ndani ya nyumba hiyo na kwa familia hiyo, niliporudiwa fahamu na kusimuliwa, nilitamani dunia ipasuke inimeze!
Kwa unyenyekevu mkubwa, nikaiomba radhi familia hiyo na tangia hapo nikaacha pombe moja kwa moja mpaka takapokufa.
.
Sent using
Jamii Forums mobile app