Vipi update za mazungumzo na Accacia

Vipi update za mazungumzo na Accacia

Naskia yanaendelea vzri; kutokana na fedha waliokubali kulipa tutanunuliwa Range sio noah tena
 
Shida yetu ni kukosa subira. 'Wanaume' wamejitolea kuzileta Noah kabisa ndio maana kuna ukimya. Hebu 'bwageni mioyo', muda huu pambana upate leseni ili siku ya uzinduzi usiseme tumekutenga, maana tutapiga bonge la show tukiperuuuuuuuuz juu ya 'furahi ova' yetu.

Timaaaaaam?
Nilivyosikia tu Noah nilitoa na ka- hela kangu kwenda kusoma Driving. Sasa hivi nipo final stage.

Yaani nina hamu ya kuendesha gari. Ila ikishindikana hata Bajaji poa.
 
Muulizeni Tundu Lissu sindiyo Msemaji wenu mnamtaka serikali ya nini wakati Lissu mnaye hukohuko
 
Nilivyosikia tu Noah nilitoa na ka- hela kangu kwenda kusoma Driving. Sasa hivi nipo final stage.

Yaani nina hamu ya kuendesha gari. Ila ikishindikana hata Bajaji poa.
Tutazindua pamoja na fulai wova, tulia mwanangu. Mgaagaa na wali hali upwa mkavu
 
Aisifuye mvua imemmnyea. Tuliwasifia wanaume, wametugonga, wametutelekeza na gu-mimba gwetu. Watatupeleka mahakamani na tutalipa mamilioni ya dola. Baba jesca unaangamiza taifa kwa maamuzi yako ya pupa
Wametutelekeza na Gu Mimba Gwetu hii imenichekesha saana Hahahahahaaaaaaaaa!!!! kwa hiyo wanaojidai wana uchungu waende Leba sasa!!!!!!😀😀😀😀😀😀😀😀😀😀🙄🙄🙄🙄😡😡😡😡😡😡🙁🙁🙁🙁😳😳😳😳!!!
 
Ukumbi wanaokutana kujadiliana unajulikana,
huo ukumbi una wafuta vumbi,wavagiaji na mawatcham,

hotel wanazofikia hao wazungu haziwezi kuwa siri kwa mtu anaetafuta,
pale airport ambapo ndo entry point panafahamika,
huko kote hakuna member wa jf wa kuleta update tukajua kama bado kuna mkutano ama la?.
 
Sina chanzo chochote cha taarifa za ndani kati ya serikali na acacia . Ila nadiriki kusema mazungumzo hayo yalishakwisha kitambo kwa kutumia akili za kuzaliwa tu. Hebu tujiulize machache haya harafu tuamue mazungumzo yanaendelea au yashakwisha kitambo.

Tangu mazungumzo hayo yaanze ni takribani mwezi sasa. Je mtanzania mwenzangu una amini unaweza kukaa na mzungu mwezi mzima kujadili jambo moja kama hili la mchanga??? Kwa ninavyowafaham wazungu wanajali sana muda kuliko chochote kile . Siamin hata kidogo kwamba bado wanazungumza na serikali yetu. Kwan hayo mazungumzo ni ya kuuziana nchi ? Mazunguzo ya nani yuko sahihi kati ya ACACIA na serikali ndio ichukue muda wote huo?? Thubutu!! Mazungumzo yalisha isha, ila naona tumepigwa za usso sasa tunajipanga tutatokaje mbele za wananchi.!! Mzungu kwake masaa 24 ya kuacha kaz moja harafu afanye kaz ya ziada jua kaz ya siku tatu itafanywa kwa siku moja. Tukae bongo na wazungu wale mwez et kujadiliana nani yuko sahihi?? Mnipige mniue hakuna kitu kama hicho.

Kinachoweza kutokea ni labda walikaa siku mbili tatu kila mmoja akaenda zake kuandaa maamuz ya oficce yake than wamepanga kuja kukutana siku ya kutoa taarifa. Lakn hili la kusema mazungumzo yanaendelea tutakua tunaota.

Kingine cha kutia shaka. Iweje ACACIA wapeleke notice ya kukusudia kutushitak kama mazungumzo yanaendelea?? Si watakua wanafanya maamuz wakati kikao kinaendelea jambo ambalo litatia litahatarisha mazungumzo kukatika?? Kuna uwezekano mkubwa tumeshindana nao kwa kukaa meza moja kwa zile jeuri zetu . Sasa wameamua kutuonyesha njia sahihi ya kutuonyesha hawatanii kwamba hawatoi hata mia isipokua wao ndio wanatudai.

Mwisho;

je wewe mdanganyika mwenzangu una amini mazunguzo yanaendelea???

Tutapata kutoka kwa Tundu Lissu, wakili wao!!
 
Nawauliza wanao miliki JF, kwahiyo haya ndio maoni, na ndio faida za uhuru wa maoni kwa nchi yetu..
 
Kabla ya kuanza mazungumzo Serikali ililazimisha wajumbe wote walilazimishwa kuapa na kusaini confidentility agreement ili kusiwepo mtu yeyote wa kutoa taarifa mpaka pande zote mbili zitakaporidhia.

Kwa hiyo serikali ikitaka kusitolewe taarifa yoyote hata kwa miaka mitatu au kumi hakuna wa kuhoji na Acacia wakitoa taarifa ya majadiliano hayo kwa mtu yeyote watakuwa wamekiuka sheria ya kiapo.

Kwa nini serikali alitaka jambo hili liwe siri kwa raia wote? Mwenye akili atajua maana inahitaji akili ufahamu wa kawaida.

Mazungumzo yalikwisha wiki jana.
 
Ni takribani mwezi mzima tangu barick na serikali waanze mazungumzo, ndani mwezi huu wote serikali ipo haisemi kinachoendelea kwenye mazungumzo.
Swali la kujiuliza mazungumzo gani hayo yanafanywa mwezi mzima, hivi kweli wale jamaa wa Barrick hawana kazi za kufanya wakae mwezi mzima kujadili makinikia.

Binafsi naamini kuwa mazungumzo yale Tanzania tumeambulia patupu, naamini wale barick wameisha ondoka inatafutwa njia ya kutudanganya wadanganyika, wazungu wanajali sana hawawezi kukaa muda kujadili jambo hilo tu la makinikia
Serikali iseme kama tumeshindwa tujue.
 
Ni takribani mwezi mzima tangu barick na serikali waanze mazungumzo, ndani mwezi huu wote serikali ipo haisemi kinachoendelea kwenye mazungumzo.
Swali la kujiuliza mazungumzo gani hayo yanafanywa mwezi mzima, hivi kweli wale jamaa wa Barrick hawana kazi za kufanya wakae mwezi mzima kujadili makinikia.

Binafsi naamini kuwa mazungumzo yale Tanzania tumeambulia naamini wale barick wameisha ondoka inatafutwa njia ya kutudanganya wadanganyika, wazungu wanajali sana hawawezi kukaa muda kujadili jambo hilo tu la makinikia
Serikali iseme kama tumeshindwa tujue.
Kwani yalikuwa ni mashindano?
 
Mimi natamani hayo mazungumzo yazae matunda.

Natamani wasifikie kwenye zero. Kwamba angalau tupate hata dola 5B itusaidie kujenga Stigler's Gorge ya megawati 2100, na standard gauge ya kwenda mwanza.

Nchi yetu ni masikini. Tuitakie mema hata kama alieko madarakani hatumpendi, yeye ataondoka ila nchi yetu itaendelea kuwepo.

Nchi ni maskini sana, ikitokea tukakosa hizo hela hajakosa Magufuli, tumekosa watanzania, maana hizo hela zitainufaisha zaidi Tanzania kuliko Magufuli, hata kama ni kula hatakula zote.

Mimi binafsi naomba tupate angalau dola 5B tu ziboost bajeti yetu.
 
Back
Top Bottom