Vipi update za mazungumzo na Accacia

Vipi update za mazungumzo na Accacia

nkulikwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2015
Posts
721
Reaction score
813
Hakuna ambaye amenusu kama zile billions zinatalipwa na wanaume au la! Mwenye update atuambe!

=================
Sina chanzo chochote cha taarifa za ndani kati ya serikali na acacia . Ila nadiriki kusema mazungumzo hayo yalishakwisha kitambo kwa kutumia akili za kuzaliwa tu. Hebu tujiulize machache haya harafu tuamue mazungumzo yanaendelea au yashakwisha kitambo.

Tangu mazungumzo hayo yaanze ni takribani mwezi sasa. Je mtanzania mwenzangu una amini unaweza kukaa na mzungu mwezi mzima kujadili jambo moja kama hili la mchanga??? Kwa ninavyowafaham wazungu wanajali sana muda kuliko chochote kile . Siamin hata kidogo kwamba bado wanazungumza na serikali yetu. Kwan hayo mazungumzo ni ya kuuziana nchi ? Mazunguzo ya nani yuko sahihi kati ya ACACIA na serikali ndio ichukue muda wote huo?? Thubutu!! Mazungumzo yalisha isha, ila naona tumepigwa za usso sasa tunajipanga tutatokaje mbele za wananchi.!! Mzungu kwake masaa 24 ya kuacha kaz moja harafu afanye kaz ya ziada jua kaz ya siku tatu itafanywa kwa siku moja. Tukae bongo na wazungu wale mwez et kujadiliana nani yuko sahihi?? Mnipige mniue hakuna kitu kama hicho.

Kinachoweza kutokea ni labda walikaa siku mbili tatu kila mmoja akaenda zake kuandaa maamuz ya oficce yake than wamepanga kuja kukutana siku ya kutoa taarifa. Lakn hili la kusema mazungumzo yanaendelea tutakua tunaota.

Kingine cha kutia shaka. Iweje ACACIA wapeleke notice ya kukusudia kutushitak kama mazungumzo yanaendelea?? Si watakua wanafanya maamuz wakati kikao kinaendelea jambo ambalo litatia litahatarisha mazungumzo kukatika?? Kuna uwezekano mkubwa tumeshindana nao kwa kukaa meza moja kwa zile jeuri zetu . Sasa wameamua kutuonyesha njia sahihi ya kutuonyesha hawatanii kwamba hawatoi hata mia isipokua wao ndio wanatudai.

Mwisho;

je wewe mdanganyika mwenzangu una amini mazunguzo yanaendelea???
 
Nipo hapa nasubiri Noah yangu kwa hamu yote ila cha kuhudhunisha hata mrejesho wa stori wakati wanakunywa chai sijasikia
 
Akili inaniambia hata kama Accacia/Barrick wakikubali kulipa haitatangazwa hadharani kama wamekubali walikosea na wamelipa kiasi gani. Hiyo itafanyika kwasababu ya kuwalinda wawekezaji wasipate misukosuko ktk soko la hisa la London. Taarifa itakuwa "Tumeshafikia makubaliano ambayo yanafaida pande zote na sasa tunaangalia zaidi namna ya kuongeza ufanisi katika uwekezaji wetu ili pande zote zipate faida zaidi. Maelezo ya ziada kuhusu makubaliano yetu yatabaki kuwa siri baina yetu. Ahsanteni sana." Mwisho wa kunukuu.
 
Agiza 'Faru John' nitumie bill
 
Swadakta...
 
Mazungumzo yatakwama tu Mtu mpo kwenye majadiliano halafu unawaita wenzako Wezi suluhu itapatikana vipi hapo
 
Hakana cha kujadili, Acacia ni wezi, wametuibia trilioni 108 na kodi trilioni 425, utajadiliana mtu kama huyu? Kwa mujibu wa ripoti za wataalamu wetu wa madini na fedha
No nikupiga assets zake pingu
 
Back
Top Bottom