Akili inaniambia hata kama Accacia/Barrick wakikubali kulipa haitatangazwa hadharani kama wamekubali walikosea na wamelipa kiasi gani. Hiyo itafanyika kwasababu ya kuwalinda wawekezaji wasipate misukosuko ktk soko la hisa la London. Taarifa itakuwa "Tumeshafikia makubaliano ambayo yanafaida pande zote na sasa tunaangalia zaidi namna ya kuongeza ufanisi katika uwekezaji wetu ili pande zote zipate faida zaidi. Maelezo ya ziada kuhusu makubaliano yetu yatabaki kuwa siri baina yetu. Ahsanteni sana." Mwisho wa kunukuu.