Vipi kuhusu suala la Machinga; bado utaratibu unazingatiwa na je, kuna miundombinu wezeshi?

At Calvary

JF-Expert Member
Aug 22, 2018
4,513
3,554
Habari zenu wakuu. Bila shaka mnafanya vyema katika ujenzi wa taifa.
Tuwe wazalendo, tupendane.

Haya moja kwa moja kwenye mada. Kuhusiana na machinga. Hapo mwanzoni mwa utawala wa Samia sakata la machinga lilichukua taswira pana. Kukatokea movement kibao na matamko ya kutosha toka kwa waandamizi mbali mbali.

Ila kwa sasa kadri siku zinaenda inaonekana kuwa serikali imeshafeli kulishughulikia suala big time. Sababu maeneo mengi ni business as usual. Na haya yote ni kwa sababu ya kukurupuka na kutaka kuridhishana ilhali hakuna mipango endelevu. Ndio maana mpaka sasa kuna maeneo machinga wameanza kurudi.

Hili jambo lilipaswa kwanza kuwa na longterm plan. Naona i short imewashinda sijui pesa hakuna, tukakope tena tukajenge masoko basi.

Anyway hizo ni stori. Na piah nina shida ya uwasilishaji hoja. Kama umenielewa akhsante.

Sasa karibu kwa mchango wako. Je mkoani kwako hali ya machinga ikoje? Did the issue has been resolved. Au wameanza kurudi nyuma? Na wale walopongeza kuhusu hatua zilizochuliwa, je bado mambo yanaendelea kama mwanzo?

Na mwisho ni kipi kifanyike kuwa na suluhu ya kudumu juu ya suala hili la machinga?

Jumapili njema.

At Calvary
 
Honestly hili ni zoezi la kuwatajirisha wahuni wachache na kuwaumiza watu wengi zaidi. Masikini kwa masikini ndio wanaumizana wakati wanaowatuma wakiendelea kujipimia kadiri wawezavyo kama walivyoruhusiwa. Nasema hivi kwa sababu pesa ya kuhonga tangu tuanze kusumbuana na hawa wahuni si chini ya laki moja. Just imagine wengine wametoa ngapi!?

Huku "kupangana" kama alivyodai anayewatuma ni kiini macho. Mimi nauza tai, mikanda na wallet pale Posta nikakae kule ghorofani machinga complex au Kisutu sokoni nitamuuzia nani!? Ndio maana sasa hivi nauza nikiwa nimeshika vitu vyangu mkononi na bado ridhiki napata. Kuliko kule machinga walikotaka kuniua njaa.

Suluhisho watenge maeneo huko huko kwenye maeneo yenye mikusanyiko na sio kujifanya kuwapeleka watu maeneo ya kuwamasikinisha kwa kudai kuwa unawasaidia. Huo ni uongo. Mathalani pale Posta walipovunja Billcanas si pamekaa wazi miaka sasa, panashindikana vipi kupatengeneza kwa ajili ya machinga wa Posta badala ya sijui huko jangwani!? Njaa haijawahi kuwa kitu kizuri waelewe hivyo. Hata wao wanarogana kwa sababu ya vyeo. Hivi si walidai mabanda ndiyo shida, sasa mabanda yameshabomolewa shida ni nini!?
 
Nadhani ushikishwaji ni mdogo. Zaidi ni mabavu yanatumika na ni kuwaumiza watu wa hali ya chini.

Hivo vikao wanakaa na tayari wanajua cha kufanya ndio chanzo mambo yanakuwa hayatekelezeki.

Nadhani ingekuwa bora wangesikilizwa kwanza machinga mapendekezo yao ndio wayafanyie kazi kuliko huu ubabe unaondelea.

Kwani hakuna namna huko mjini wakaweka miundombinu wezeshi.?
 
Na tatizo lingine ni huyu mtu anajiita Makala. Huyu siku zote ana chuki na machinga. Hajawahi kuwaza namna ya kuwasaidia yenye tija pande zote. Hata kule Mbeya alisumbua sana. Yeye ni mtu anayeamini katika kukimbizana tu, yaani mabavu.
 
Duh, kazi ipo
 
Back
Top Bottom