Viongozi wetu na Kingereza

Jamaa katisha. Nimefurahi aliposema, "all people they supposed to be accoutable"
 
Mkuu kidogo ungenikata mbavu zangu. Naona hii itakuwa kali ya kufungia mwezi. Ni kweli kwa mazingira ya Osterbay kuna ulazima wa kuweka Tangazo kwa kiingereza sababu wapo wageni wengi. Lakini siamini kwamba alikosekana kabisa mtu wa kuipitia hiyo barua kabla ya kubandikwa. Hii ndivyo tunavyotaka tuonekane machoni kwa wageni!!.
 
Mmmmmh!

Huyu naye!! Ila na sisi wa-TZ kwa kushobokea Kiingereza bwana! Hapo ukute ameamua kuliweka kimya kimya bila kushirikisha wengine ili watu pale Kitaa wamwone yuko juu, yaani Mwenyekiti wa mtaa wetu hapa Oyster bay anashuka Kiinglishi ni mwisho wa maneno!!!

Ona sasa alivyoishia aibu. Aibu yake, Aibu ya CCM
 
Kumbe wa mtaa! Mbona kajitahidi sana,watu na masters zao lakini bado ni "somebody gas" chezea kingereza wewe...
 
Kuna haja ya watanzania kukubaliana namna ya kuwapata viongozi wenye uelewa lakini pia wenye kufahamu lugha gani watumie kwa njia ya mawasiliano hembu angalieni viongozi wenu wa CCm wanavyowasiliana kwa lugha ya kingereza
 
Turudi nyuma kidogo, hivi tukiambiwa baadhi yetu humu JF tuirekebishe hiyo barua, ni wangapi watathubutu? Mushi amethubutu, ameweza na anasonga mbele. Ujumbe umefika kwa walengwa.
 
kwanini wasiwe wanaandika kiswahili? ukiwa france ivory coast na kwengineko wanaandika kifaransa kama hujui lugha utajiju...
 
Nyie mchekeni, atakuja kuwa Mbunge wenu huko Kilimanjaro. Anaitwa Mushi!

Si bora ya huyu aingie bungeni , umewahi ona mbuge Lusinde au Majimarefu wanapokuwa kwenye kamati za bunge halafu kukawa na bahati mbaya ya kukutana na Mzungu??? utawaona wanajisogeza nyuma taaraaatiiiibu ... mpaka wapate usawa wa mwishoooo kabisa na kuwaachia wenzao wanaopandisha slang wakae mbele hapo ndipo nyoyo zao hupata amani
 
Angetumia lugha ya Taifa angeeleweka zaidi. Sasa watu wataishia kustruggle na kiingereza chake badala ya ujume uliomo kwenye barua
 
duh hii nimeikubali...

attachment.php
 

Attachments

  • kingereza_page1_image1.jpg
    kingereza_page1_image1.jpg
    483.9 KB · Views: 978
Back
Top Bottom