Viongozi wetu na Kingereza

someni hapo kuanzia "........ORDER, if your refuse to be accountable or stop the censer officer to do the job of counting people............." = usipowajibika kwa jamaa au kuzuia ofisa wa sensa kufanya kazi yake ya kuhesabu watu.... Jamani hapo shida yenu ni nini, jamaa amekosea nini?
 
"Censer".

Kutojua kiingereza si shida, after all huyu ni Mwenyekiti wa serikali za mitaa kitu ambacho almost mtu yeyote anaweza kuwa.

Kulazimisha kuandika Kiingereza wakati unaweza kuandika Kiswahili, kutojua kwamba hujui Kiingereza kiasi cha kuji expose hivi, kutojali au kutokuwa na akili za kuwapa wanaojua wafanye "proofreading" kunaonyesha kutokuwa na werevu wala maarifa.
 
Aisee kwakweli inachekesha sana! inafaa jukwaa la Burudani,lakini message imefika bwana,hata hivyo siyo lugha yetu ya mama. Angalizo siku nyingine ajitahidi kupeleka kwa wajuzi au wakubwa wake wanaojua vizuri lugha hiyo ili waipitie!

umesikiliza bunge la Kenya,utadhani wanaigiza lafudhi yao,pi kuna events hata grammer ni issue, msikilize waziri mkuu Raila anvyoongea kam ulimi umewekwa gundi.Nao wanchekesha hamana mfano.T
 
In a nutshell: Huyu jamaa katafsiri kiswahili kwenda Kiingereza ndugu zangu lugha za watu hizi tuwe makini na hasa unapokuwa na kanafasi. Mungu atuponye sisi watu wake, na hii ndio aliyosema Mh. Peter Msigwa watu wa kiwango kimoja cha elimu, uelewa hawawezi kusaidiana bali wanahitaji aliye juu kiuelewa maarifa nk. Sasa unaandika censer badala ya censors, Residance badala ya Residence, Beural badala ya Bureau, Accountable badala ya counted, Censer officer badala ya censors officilas. It is very interesting!!!!
 
...he or she must be countable to this censer! Mungu jalia.....kaniacha hoi! Hapo katunisha msuli hadi kaweka saini! Mungu saidia elimu yetu!
 
"Remember the Government of Republic Union of Tanzania announce on 26.08.2012 is the day of
counting people [censer] for all living visitors in Tanzania"

Cha msingi ujumbe umefika.......CCM Oyeeee......
 
nilikuwa naangalia bunge la kenya n akujaribu angalia kam akweli tupo tofauti sana.Duh nao ni vichekesho.Ila niclichoweza gundua pia ni kuwa wapo wabunge wachache wenye kiingereza kizuri nc akinachopelek ujumbe bila kushanganya.

katika vichekesho vyao vya lugh ya watu kama vile wakoseavyo kiswahili walinimaliza kwa Mbunge mmoja kulalama kuwa wakimbiaji wao walikuwa wamevaa nguo za kike.Raila akachomekea kuwa kama jamaa hakulalamika sio shinda,kwani alipambana hadi kupata medali kwa kwa kenya.Hii ndio nchi ya waoenda suti bwana halafu kuna wasiojua kuvaa au kuwavaliasha wenzao.
 
Hii kitu enzi zangu za shule ya msingi tulikuwa tunaita BANDUA BANDIKA.

Kwanza kabisa unaandika barua yangu nzuri kwa lugha ya kiswahili mpaka unaridhika nayo kimpangilio.

Baada ya kunywa kahawa kidogo, sasa unaanza kazi ya Bandua Bandika.
Palipo na neno la kiswahili unalibandua neno la kiswahili na badala yake una bandika neno la kiingilishi vile.

Hapo majambo yote yanakuwa poa kama ilivyo barua ya mwenyekiti wa mtaa ( CCM).
 
Du aisee si angendika kiswahili tu? Ahaa kwa vile kule oysbey wazungu wengi ndio maana akajikakamua. Sasa si angetafuta japo mtu anaekijua? Du kali.
 
Du aisee si angendika kiswahili tu? Ahaa kwa vile kule oysbey wazungu wengi ndio maana akajikakamua. Sasa si angetafuta japo mtu anaekijua? Du kali.

Mtu kama huyu sina hata uhakika kama angeandika Kiswahili kungekuwa na afadhali.

Inawezekana Kiswahili akapunguza makosa tu, lakini akaburuza vilevile.
 
Du aisee si angendika kiswahili tu? Ahaa kwa vile kule oysbey wazungu wengi ndio maana akajikakamua. Sasa si angetafuta japo mtu anaekijua? Du kali.
 
Angejiandikia tu kiswahili, hao wageni wangetafuta wakalimali, mbona tulienda nchi zao hawatuingeleshi kiswahili bwana.....inabidi tujivunie lugha yetu, labda kama unatafuta wateja hapo ntakuelewa.
 
Back
Top Bottom