Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 18,320
- 33,940
Kuratibu na kulinda misafara ya viongozi si jambo jepesi kama watu wengi wanavyodhani. Kuwa na mazingira wezeshi ya kulinda misafara hiyo pia si jambo la Polimi lai!!
Naona watu wengi pamoja na wanasiasa wenyewe wanachanganya kati ya kuwa na misafara mirefu na muda unaotumika kupitisha misafara kutokana na uhitaji wa huyo aliyemo kwenye msafara husika.
Leo mnataka misafara ilindwe kisiasa kuwafurahisha wanaosubirishwa bila ya kuangalia chanzo cha kusubirishwa huko. Kwa mfano misafara ya Dar toka Ikulu mpaka uwanja ndege hutumia kati ya Dakika 7 mpaka 10 kwa muda wa kawaida ama dakika 10 hadi 12 kama kuna dosari za mwendo na mpangiilio wa magari.
Lakini kama msafara huo huo toka Uwanja wa ndege kwenda Ikulu ukiwa na Mgeni unaweza kuchukua mpaka dakika 30. Sasa waliomo kwenye msafara siyo waliomo kwenye vituo (Point) vya kuongozea magari yapitayo msafara unapopita. Na Mwelekeo wa gari haudhibitiwi toka kwenye Pointi bali kule linakoelekea.
Kwa mfano kwenye Point tata ya Gerezani, wale wanaotaka Magari yazuiuwe dakika 10 kabla ya msafara kupita wanaelewa wanachokisema? Kwa mfano Magari yaruhusiwe kuelekea njia ya Kurasini, na ya kurasini yaruhusiwe kuelekea Posta. Nani atakuwa anasimamia mwendo kasi wa magari hayo??
Maana watu wanadhani kwamba ni kitu rahisi kuwafanya madereva wote wa Magari wafikirie kwa kufanana kwamba wanatakiwa waharakishe ili msafara upite. Matokeo yake kukiwa na kukwama basi lawama tena watatupiwa watu wa Usalama barabarani.
Wanasiasa wanaowalaumu Polisi leo ndiyo hao hao huwa wanawalaumu misafara inapoingiliwa. Na mikoani ndiyo Karipio huwa kubwa sana na Ma -RPC huwa kwenye changamoto kubwa sana kwenye kusimamia misafara hiyo.