Ushauri kwa watawala kuhusu matumizi yasiyo ya lazima sana

koryo1952

JF-Expert Member
Mar 7, 2023
380
763
Kila kukicha tunashauri tubane matumizi katika kila eneo, sasa mimi nikiwa mwanchi wa kawaida kabisa nashauri yafuatayo kwa Watawala kuhusu kupunguza matumizi makubwa ya Serikali.

(1) Wananchi tumeshuhudia misafara mikubwa ya magari ya umma yakisindikiza misafara ya Viongozi Wakuu mfano Mhe. Rais, Makamu wa Rais, Mhe. Waziri Mkuu, Wahe. Mawaziri, Mhe. Makonda na wengineo.

Utakuta katika msafara moja magari siyo chini ya 40. Msafara huu unatumia mafuta, posho, chakula, malazi n.k. Ukilinganisha msafara wa siku moja, gharama yake inaweza kujenga

Kituo kimoja cha Afya. Sisi ni nchi maskini kwa nini Watawala wakachukua uamuzi mgumu kuwa katika msafara moja kuwe na angalau magari yasiyozidi kumi.

Ushauri wangu kwa Watawala tupunguze matumizi ambayo siyo ya lazima.
 
mambo yasiyo ya lazima ni pamoja na shughuli za uzinduzi.Tanzania bado tunajitafuta kiuchumi lakini tuna mbwembwe kuzidi nchi tajiri.

uzinduzi ni nyingi kuliko maendeleo na zinduzi zote zinatafuna pesa na kufunga barabara kupisha kiongozi wa kondoo anaenda kuzindua.
 
Kila kukicha tunashauri tubane matumizi katika kila eneo, sasa mimi nikiwa mwanchi wa kawaida kabisa nashauri yafuatayo kwa Watawala kuhusu kupunguza matumizi makubwa ya Serikali.
(1) Wananchi tumeshuhudia misafara mikubwa ya magari ya umma yakisindikiza misafara ya Viongozi Wakuu mfano Mhe. Rais, Makamu wa Rais, Mhe. Waziri Mkuu, Wahe. Mawziri, Mhe. Makonda na wengineo. Utakuta katika msafara moja magari siyo chini ya 40. Msafara huu unatumia mafuta, posho, chakula, malazi n.k. Ukilinganisha msafara wa siku moja, gharama yake inaweza kujenga
Kituo kimoja cha Afya. Sisi ni nchi maskini kwa nini Watawala wakachukua uamuzi mgumu kuwa katika msafara moja kuwe na angalau magari yasiyozidi kumi.
Ushauri wangu kwa Watawala tupunguze matumizi ambayo siyo ya lazima.
haowezekani waziri mkuu yupo mkoa au wilaya fulani kisha wakuu wa idara na vuongozi waandamizi wa eneo husika wasiwepo kwenye msafara wake. Ikitokea kuna jambo waziri mkua anataka kujua nani atalitolea maelezo au kulifafanua....
na ndio kazi zenyewe hizo...

labada ungeshauri eneo jengine..
 
Screenshot_20240416-065933.jpg
 
Back
Top Bottom