The Palm Beach
JF-Expert Member
- Dec 30, 2015
- 810
- 1,667
Kumbe "mlihamasishwa" tu?Sisi viongozi wa Dini wa Mkoa wa Kilimanjaro tumeshangazwa na ujumbe unaosambazwa mitandaoni kwamba tutahusika na mapokezi ya Kiongozi wa Kisiasa .
Tunatambua kwamba ujumbe huo ni wa Wanasiasa na wala haujatoka kwetu sisi viongozi wa Dini. Sisi kama viongozi wenu wa Dini tunaendelea kujikita kwenye masuala ya Kiroho na kuliombea Taifa letu pasipo kujihusisha na Siasa na mapokezi ya Kisiasa.
Tunaomba Wananchi na waumini wote wapuuzie uhamasishaji huo unaolenga kutumia jina la Viongozi wa Dini kwa matakwa binafsi ya Kisiasa. Mwenyezi Mungu aibariki nchi yetu na kutujalia Neema zake.
Imetolewa na Umoja wa Viongozi wa Dini Mkoa wa Kilimanjaro.
18/03/2022.
Sasa shida yako ni nini? Maana kuhamasishwa ni kitu kimoja. Kwenda au kutokwenda ni kitu kingine kabisa. Inabaki kubwa ni utashi wako. Sasa ishu ya kujipashika nafsi ya "sisi viongozi wa dini" inatoka wapi tena?
Mimi nadhani wewe una tatizo la political insecurity kiasi cha kuamua kujivika gauni la "ukiongozi wa dini" ili u - express insecurity yako unanimously
Huo ni UJINGA na UPUMBAVU kaka/dada yangu!!
Acha hizo. Jiamini na tenda wema na haki utafurahia maisha. Be yourself!!