Kuna baadhi ya Viongozi wa Dini Wanataka kumdhoofisha na kumpa hofu Rais Samia

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,311
9,740
Ndugu zangu Watanzania,

Huo ndio ukweli ambao upo wazi kwa yeyote mwenye akili Timamu na mwenye kupima kauli ,matendo,maneno,Historia ya Baadhi ya viongozi wa Dini katika awamu Tofauti tofauti na kwa marais tofauti Tofauti katika ukosoaji na uotaji wa matamko na nyaraka na kile kinachoitwa misimamo binafsi au ya kitaasisi.

Kuna Baadhi ya viongozi wa Dini Wanataka kutumia Dini au uongozi wao au makoti ya Dini kwa makusudi na malengo maalumu, kwa ajenda maalumu ,kwa dhamira maalumu ,kwa Hesabu maalumu ,kwa mipango maalumu,kwa mikakati maalumu kutaka kumdhoofisha Rais samia kiutendaji na kumpa Hofu isiyo ya msingi.

Inapofikia hatua kiongozi wa Dini anatamka maneno kuwa Taasisi aliyopo au anayoongoza au kuisimamia ni kubwa yenye mizizi mpaka ngazi ya kaya. maana yake au mantiki ya maneno au kauli hiyo ni kuwa anataka kumwambia au kutuma ujumbe kwa Rais wetu na serikali yake kuwa yeye ni mkubwa kuliko serikali,yeye yupo juu ya serikali na Rais,yeye ana hadhi kubwa kuliko Rais,yeye anapaswa kusikilizwa kuliko mtu yeyote,yeye ni mmiliki wa mawazo na akili za watanzania na yeye ndio sauti ya watanzania na kwamba asipo sikilizwa yeye basi lolote atakalo linaweza kufanyika au yeye ndiye mwenye kauli ya mwisho inayopaswa kutekelezwa na kufuatwa na serikali.

Hii ni hujuma kwa mh Rais na serikali yetu,Hii ni dharau kwa mh Rais na serikali yetu,ni kutaka kumpa Hofu mh Rais na ni kutaka kumdhoofisha Rais wetu.Kuna Baadhi ya viongozi wa Dini wanataka misimamo yao Binafsi na mitizamo yao hasi au kule kutomuunga mkono mh Rais wanataka kulivalisha kanisa zima na waumini wote kuifuata na kuiamini misimamo yao.Hii siyo sawa na haiwezi kuwa sawa. Kwa kuwa hawajaja kwetu waumini kutuomba maoni yetu na mawazo yetu au mitizamo yetu.Hakuna kura iliyoitishwa au kutoa nafasi ya kutoa mawazo au mitizamo kwa waumini juu ya suala la Bandari na masuala yoyote yale ndani ya jamii yetu.

Kinachotokea na kuendelea kwa sasa ni kwa baadhi ya viongozi wa Dini kuchomekea misimamo yao Binafsi ,mapenzi yao na kuyaweka katika Taswira ya kuonekana ndio msimamo wa Taasisi nzima na kanisa zima,jambo ambalo siyo la kweli na halina ukweli wowote ndani yake. Kwa kuwa sisi waumini tunashangaa na kufedheheshwa na hatua ya baadhi ya viongozi wetu kutumia Dini kama kichaka cha kutaka kuidhoofisha serikali yetu kwa ajenda zao binafsi na kutujumuisha katika misimamo yao binafsi kuwa ni yetu.

Sisi waumini tunachosema ni kuwa Dini na viongozi wetu wa Dini watambue heshima kubwa waliyonayo katika jamii kiimani na kiroho,lakini heshima hiyo haiwezi kuendelezwa na kupewa au kutolewa ikiwa wataonyesha upendeleo,mapenzi binafsi kwa viongozi au watu au Tofauti ya kidini ya kiongozi anayekuwepo madarakani .Tutawapinga kwa nguvu zetu zote bila kujali vyeo vyao.Tutawapinga kwa kuwa watakuwa wamekwenda kinyume na maadili na kile tunachotarajia kupata na kukiona kutoka kwao.

Hata zisomwe nyaraka ngapi makanisani na kwa muda gani bado hatutakubali kuona Rais wetu anahujumiwa na kudhoofishwa kiutendaji.sisi waumini akili zetu hatubebewi wala kushikiwa na viongozi wa Dini,kinachotuongoza ni Biblia na neno la Mungu kutoka ndani ya Biblia na lenye kurejea vifungu vya Biblia na siyo matamko au kauli au maneno yasiyo na vifungu wala rejea kutoka ndani ya Biblia isiyo eleweka msingi wake,mitizamo ya mtu binafsi haiwezi kuwa msimamo wa kanisa zima na waumini wote,kwa kuwa viongozi wa Dini hawana hati miliki kwetu waumini.

Rai yangu kwa viongozi wote wa Dini ni kuwaasa kutokuleta mitafaruko ndani ya jamii yetu,wasitake kulipasua Taifa letu kwa kuleta hisia za Udini,wasitumike hovyo wala kutumika na watu wenye maslahi binafsi,wazichunge na kuzishibisha Roho za waumini kwa neno litokalo katika biblia na siyo maneno kutokana na mitizamo au mapenzi binafsi,wasitupe misimamo yao binafsi kuwa misimamo ya kanisa wakati hakuna tulipokaa tukatoa mawazo yetu.

Amani yetu inapaswa kulindwa kwa nguvu zote,hisia za kidini zikipandikizwa na kumea katika mioyo ya watanzania litakuwa ni jambo la hatari sana katika umoja na mshikamano wa Taifa letu.Tusiangalie faida au matamanio ya kimadaraka ya muda mfupi au kutaka kumfanikisha au kumsaidia au kumsafishia njia fulani atwae uongozi na madaraka na kushindwa kuona athari za muda mrefu zinazoweza kulikumba Taifa na kuatamia katika mioyo ya watanzania.

Tusilete na kutaka kuchochea fikira za kidini,tusilete mitizamo hiyo.Tukifikia hatua hiyo itapelekea watu wafikie hatua ya kutaka na kufuatilia kila uteuzi utakapofanyika kuangalia aliyeteuliwa katika nafasi fulani ni wa dini gani? Ana swali au kusali wapi? Ndugu Viongozi wangu na wetu wa Dini Mnataka kupanda mbegu gani kwenye mioyo ya watanzania? Mnataka kulipeleka wapi Taifa letu? Mnataka kutufundisha nini watanzania? Mnataka tuelewe nini watanzania? Mnataka tuamini nini? Tuishi vipi? Tuseme nini? Mnataka nini juu ya serikali yetu na Rais wetu?

Hapana hapana hapana hapana Watanzania hatupo tayari kuona Rais wetu akidhoofishwa na kuhujumiwa kiutendaji,maana tutakaoathirika ni sisi watanzania wanyonge . Tupo na Rais wetu na tunamtizama kwa matumaini makubwa na tuna matarajio makubwa kutoka kwenye uongozi na serikali yake na tusingependa kuona yeyote wa cheo chochote wa Dini yoyote wa Dhehebu lolote wa chama chochote akimhujumu au kumdhoofisha Rais wetu na serikali yetu,maana itakuwa ni hujuma kwetu watanzania na Taifa letu kwa ujumla.

Kazi iendelee mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel mwashambwa,kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
 

Attachments

  • 6DE6DCC6-D8B1-4FE5-B2E0-71CB7A9BDB4A.png
    6DE6DCC6-D8B1-4FE5-B2E0-71CB7A9BDB4A.png
    84.3 KB · Views: 2
  • IMG_2047.MP4
    1.2 MB
Ndugu zangu watanzania,

Huo ndio ukweli ambao upo wazi kwa yeyote mwenye akili Timamu na mwenye kupima kauli ,matendo,maneno,Historia ya Baadhi ya viongozi wa Dini katika awamu Tofauti tofauti na kwa marais tofauti Tofauti katika ukosoaji na uotaji wa matamko na nyaraka na kile kinachoitwa misimamo binafsi au ya kitaasisi.
Wewe Homeboy Lucus hata sisi ni Chawa wa Mama Wewe ila mimi na watanzania zaidi 80% Yanao jielewa hatutaki mkataba wa kuuza bandari zaidi zetu. Achana kuwa kibaraka wa Kuuza urithi wetu,
 
Mkataba mbovu ndugu, hauna maslahi ya nchi mnaung'ang'ania wanini jamani kuweni wazalendo kutoa maneno machafu namnahiyo kwataasisi ya dini. Mjinga mkubwa wewe Huna uzalendo na inchi unachowaza ni vyeo tu si maslahi ya nchi.
Taasisi inaongozwa na nani? Inasimamiwa na nani? Kwani wanaoongoza siyo watu? Siyo watanzania? Kwani wao hawakosolewi? Hawakosei? Ni malaika? Ni wakamilifu?
 
Ndugu zangu Watanzania,

Huo ndio ukweli ambao upo wazi kwa yeyote mwenye akili Timamu na mwenye kupima kauli ,matendo,maneno,Historia ya Baadhi ya viongozi wa Dini katika awamu Tofauti tofauti na kwa marais tofauti Tofauti katika ukosoaji na uotaji wa matamko na nyaraka na kile kinachoitwa misimamo binafsi au ya kitaasisi.


0742-676627.
Bull💩💩💩
 
Ndugu zangu Watanzania,

Huo ndio ukweli ambao upo wazi kwa yeyote mwenye akili Timamu na mwenye kupima kauli ,matendo,maneno,Historia ya Baadhi ya viongozi wa Dini katika awamu Tofauti tofauti na kwa marais tofauti Tofauti katika ukosoaji na uotaji wa matamko na nyaraka na kile kinachoitwa misimamo binafsi au ya kitaasisi.


0742-676627.
Hivi wewe ndo mkulu mwenyewe nini? Maana siamini kama kuna any binadamu ‘independent’ mwenye mawazo yako mkuu!
 
Wewe Homeboy Lucus hata sisi ni Chawa wa Mama Wewe ila mimi na watanzania zaidi 80% Yanao jielewa hatutaki mkataba wa kuuza bandari zaidi zetu. Achana kuwa kibaraka wa Kuuza urithi wetu,
Inatakiwa uweke ushahidi wa kinyaraka wa namna urithi wetu wa athiri ulivyouzwa na kiasa cha bei kilicho kubakiwa,malipo yaliponyikia ,tarehe ya malipo,benki zilikowekwa pesa ,malipo yaliyolipwa mpaka sasa ,watia saini wa mauziano hayo na sahihi zao pamoja na nyaraka za mauziano hayo.
 
Back
Top Bottom