Viongozi BAKWATA - Simiyu wadaiwa kusimamishana kwa muda usiojulikana kisa matumizi mabaya ya madaraka

BigTall

JF-Expert Member
Mar 9, 2022
422
1,049
Viongozi sita wakiwemo Mashekh wawili wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Wilaya za Meatu na Bariadi mkoani Simiyu, wanadaiwa kusimamishwa uongozi wao kwa muda usiojulikana kutokana na tuhuma mbalimbali wanazodaiwa kutuhumiwa.

Imedaiwa kuwa viongozi hao walisimamishwa na Mkutano Mkuu wa BAKWATA Mkoa, ulioketi Juni 10, 2023, mjini Bariadi ukiongozwa na Sheikh wa Mkoa Mohamud Karokola.

Taarifa za ndani zinaeleza kuwa viongozi waliosimamishwa ni Sheikh Mkuu wa Wilaya ya Meatu Issa Nyangenyange, Katibu Bakwata Wilaya Meatu pamoja na Mwenyekiti wa Halmashauri kuu ya Bakwata Wilaya ya Meatu.

Wengine ni Sheikh Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Juma Athuman, Katibu wa BAKWATA Wilaya ya Bariadi na Mwenyekiti wa Halmashauri kuu Bakwata Bariadi.

Taarifa zinaeleza viongozi hao wanatuhumiwa kusababisha migogoro ya mara kwa mara kwenye Wilaya zao, matumizi mabaya ya madaraka, kufukuza viongozi wenzao bila ya kufuata taratibu.

Tuhuma nyingine kukaidi na kudharau maamuzi na maagizo ya viongozi wao wa juu, pamoja na kuingilia shughuli za kiutendaji bila ya kufuata utaratibu.

Hata hivyo licha ya Mkutano Mkuu huo kuwasimamisha viongozi hao, iliundwa kamati maalumu yenye wajumbe watano kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa tuhuma zinazowakabili viongozi hao kama zina ukweli au hapana.

“ Wajumbe tuliazimia wasimamishwe kwanza uongozi viongozi hao, maana tuhuma dhidi yao zimekuwa nyingi, na tuliunda tume ichunguze ukweli wa tuhuma hizo, kama zina ukweli hatua zaidi zichukuliwe, kama hakuna ukweli wataendelea na majukumu yao,” alisema Mmoja wa wajumbe ambaye hakutaka jina lake litajwe.

Tumemtafuta mmoja wa viongozi wanaotuhumiwa Sheikh Issa Nyangenyange, ambaye amesema kuwa tuhuma hizo hazina ukweli huku akitaka tume iliyoundwa ifanye kazi kwanza ili kubaini ukweli uko wapi.

“ Hizo tuhuma hazia ukweli, kama wewe ni mwandishi na unataka kuandika ukweli, tusubilie kwanza hiyo tume ifanye kazi yake, tusiandike kwa sasa ili kuchafua viongozi, tusubilie tume tujue ukweli uko wapi” amesema Sheikh Nyangenyange.

Alipotafutwa Katibu wa Bakwata Mkoa Dotto Mayombi kutaka kupata ufafanuzi juu ya taarifa hizo, alisema kuwa yeye siyo msemaji wa taasisi na badala yake atafutwe Sheikh Mkuu wa Mkoa.

Tulimtafuta Sheikh wa Mkoa Mohamud Kalokora, kuelekeza jambo hilo ambapo amesema kuwa kwa sasa hayuko tayari kuliongea… “ Hilo jambo liache kama lilivyo, siko tayari kuliongelea kwa sasa”.
 
Back
Top Bottom