Mufti Mkuu amtengua Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Simiyu kwa kukiuka maagizo ya Mkutano Mkuu wa BAKWATA

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,460

Mufti Mkuu wa Tanzania Abubakar Zuber Bin Ally amemsimamisha Sheikh wa Mkoa wa Simiyu, Mahamoud Salum Kalokola kutokana na kukiuka maamuzi halali na maagizo ya mkutano Mkuu ya Baraza Kuu la Waislamu (BAKWATA) Mkoa uliofanyika Juni 10, 2023.

Baada ya maamuzi hayo Khadhi wa Mkoa wa Simiyu, Issa Kwezi Kidai amekaimishwa kuwa Kaimu Sheikh wa Mkoa wa Simiyu.

Katibu Mkuu wa BAKWATA Taifa, Alhaji Nuhu Jabir Mruma amesema maamuzi hayo yametolewa Agosti 5, 2023, ambapo pia amewasimamisha kazi Sheikh wa Wilaya ya Bariadi, Juma Athumani na Sheikh wa Wilaya ya Meatu, Isa Nyangenyange.

Akizungumza baada ya kukaimishwa, Issa Kwezi Kidai amesema “Nashukuru kwa uteuzi huu, sina budi kupokea uteuzi huu na kwa kipindi ambacho nitakaimu ninaahidi kushirikiana na viongozi wa BAKWATA kuanzia ngazi ya msikiti, kata, wilaya, mkoa na Taifa.”
 
Kazi kubwa ya masheikh wa bakwata ni kuisifia serikali na kuomba dua kwenye mkutano ya siasa za ccm
 
Back
Top Bottom