SIMIYU: Watu zaidi ya 22 wapoteza Maisha kwa kufukiwa na kifusi baada ya Mgodi kutitia Wilayani Bariadi

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,309
5,464
Ndugu zangu kuna taarifa nimezipata kuwa inadaiwa kuna Mgodi umetitia kutokana na mvua zinazoendelea Wilayani Bariadi Mkoani Simiyu na Watu kadhaa kufukiwa.

Mgodi upo Kijiji kinaitwa Ikinabushu, details za jina na kilichotokea zaidi bado sijazipata.

Mliopo karibu na Bariadi tupeni taarifa zaidi.

======

WATU ZAIDI YA 10 WAHOFIWA KUPOTEZA MAISHA
SIMIYU: Tukio la kutitia kwa kifusi katika Mgodi wa Dhahabu wa Ikinabushu uliopo Wilayani Bariadi linadaiwa kusababisha watu zaidi ya 10 kupoteza maisha na wengine kujeruhiwa.

Kamanda wa Polisi Mkoa, Mkuu wa Mkoa na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama na viongozi wengine wa Wilaya na Mkoa wote wapo eneo la tukio.

Hali hiyo imetokea wakati mvua zikiendelea kunyesha kwa wingi Mkoani #Simiyu. Taarifa zaidi zitafuata.

=====

UPDATES

Zoezi la kufukua miili ya wachimbaji waliofukiwa na kifusi katika mgodi wa IKINABUSHU uliopo kijiji cha Ikinabushu Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu imefikia 22 hadi kufikia usiku wa Jumamosi January 13.

Mkuu wa Wilaya Bariadi Simon Simalenga amethibitisha idadi hiyo Usiku huu wakati akizungumza na #CloudsDigital
 
Mvua ni nyingi,
Ilikua suala la kuchukua tahadhari tuu,
Hili mbona linajulikana, mda mwingine hata Maji yanaingia kwenye mashimo.
 
Pole sana kwa wafiwa ila kipindi kama hichi cha mvua tahadhali ni muhimu sana kwa wachimbaji vinginevyo kifo unakiona nje nje
 
Machimboni ni kama jeshi la ziada, aisee maisha Kule sio kabisa Kuna watu wamejichoka sana, ila nachopenda Kule Kila mtu anamuheshimu mwenzake na kumuona mpambanaji, ujinga ujinga wa kuleteana ubabe ni mara chache sana kuona
 
kazi ambayo nilisema siwezi kufanya hata niwe nimefika mwisho ni hii ya kuingia huko chini ya ardhi pamoja na kazi za kwenya maji mfano uvuvi na nk.

najua kufa nitakufa tu ila kufa huku najiona hapana

pole sana kwa Wafiwa
Wewe hujawahi pambana wewe mwanaume usiseme hivyo ukifukishwa duniani kupambana tu, yumkini huajwahi lala polisi wewe ama kwenda kwa sangoma chonganishi kama sivyo basi uwe unasali sana dua ibada
 
Wewe hujawahi pambana wewe mwanaume usiseme hivyo ukifukishwa duniani kupambana tu, yumkini huajwahi lala polisi wewe ama kwenda kwa sangoma chonganishi kama sivyo basi uwe unasali sana dua ibada
acha Polisi mi nimeshakaa jela tofauti tofauti mikoa tofauti na kuhusu kwa Sangoma nilishaogea makaburini sana tu ila mgodini chini ya ardhi siendi na kwenya maji siendi sio kwamba nitaishi milele ila kufa huku najiona hapana 🙌
 
1000007113.jpg
 
Nishawahi ingia uko chini Nyarugusu.

Napenda kusema KULE SIO KUZURI
 
Pole yao wafiwa na nchi kwa ujumla
Ila kwa biashara hizi na kazi kama ya kuingia chini wakati wa mvua hivi bora serikali ingekuwa inasitisha uchimbaji wa hivyo
Serikali ina wajibu kuwalinda Raia kama hivi
Kweli ndio ajira zao lakini ni hatari sana kwa wakati huu
 
nadhani kati ya kazi unayokiona kifo kama hii ya machimbo kwa sababu wakati wowote mambo yanakuharibikia, yaani ni sawa na tumbo la kuhara
Kuna sehemu inaitwa Mererani, wanachimba Tanzanite. Kuna jamaa aliniambia wachimba wenye lifespan yao inapunga kwa sababu ya lile vumbi. Vumbi la ile sehemu ni baya sana, liko kama majivu, ukichanganya na moshi wa baruti wanazotumia kulipua miamba, ni hatari. Magonjwa ya mapafu kujaa maji ni mengi.
 
Back
Top Bottom