Vincent Nyerere ampa Mkapa vidonge stahiki

Nadhani hii itakuwa ni mara ya mwisho kwa Mkapa kushiriki kwenye siasa.

Nimefurahi kusema ukweli, ingawaje sikubaliani na assertion ya Vincent, lakini thanks God finally huyu Mkapa aliyefanya biashara ikulu anakuwa exposed.

Huyu mtu anapata moral authority ya kufanya kampeni?
Matatizo mengi tuliyonayo sasa yametokana na ufisadi wa utawala wake.

And by the way, anaweza kukataa kwenye hili, lakini jee nani alimuua Kombe yule wa usalama wa taifa?
 
Mkuu,

Mimi nilienda kumwona Mwalimu na pia wawakilishi mbalimbali wa Watanzania walikuwa wanaenda kumwona kila siku.

Unachoandika hapa ni majungu na inatakiwa uone hata aibu kuingiza majungu kwa ajili tu ya siasa za maji taka.

Hata madaktari waliokuwa wanamtibu mwalimu walisamehe malipo yao kama heshima zao kwa mwalimu na watanzania.

kwa taarifa yako kwa UK ni sheria, mgonjwa yeyote akikutwa na kitu chochote ambacho kinaonekana huenda kuna mkono wa mtu, huita polisi hapo hapo. Hiyo ni sheria na hakuna daktari anayeweza kupuuza.

Kama kulikuwa na mkono wa mtu kwenye ugonjwa wa Nyerere na madaktari wake walijua, HAIWEZEKANI, narudia HAIWEZEKANI wanyamaze kimya.

Hizi story mtawadanganya watu ambao hawajui jinsi sheria za UK zinavyofanya kazi.

na ndio Maana walituuzia Rada Mbovu?
 
Tena wadai genes za kina Nyerere zina chembechembe za CCM, hivyo kitendo cha Vincent kujiuunga Chadema ni uthibitisho dili ilichezwa hivyo kudai anayepinga DNA ifanyike kuthibitisha not only ni mtoto wa nje bali pia wa kusingiziwa!.

Kwa hiyo hata Makongoro alipokuwa Mbunge wa Arusha Mjini kupitia Upinzani (NCCR-Mageuzi) naye ni mtoto wa nje?
 
kumbe humu jf tnachangia kiushabiki sana!mathalani mkapa angekataa kumpeleka mwl nyerere kutibiwa nje ya nchi watu kama vicent wangesema kama alvyoropoka,pili mm mwenyewe nina mzee,na mara nyingi wazee wetu huwa wabishi kwa hyo mwl nyerere aliapply hyo tabia ya wazee,halfu nyie wanajf kwl kwa akili alyokuwa nayo nyerere unaweza kusema eti alilazimishwa,huu ni ujinga na upuuzi kabisa,tjipange kuchambua mambo vzuri,

Mkuu haya unayoyaongea hapa una uhakika nayo au unadhania tu na kutanguliza kejeri kwa wana JF!!?
Please usilolijua angalia kwa macho!!!
Rejea post yangu page2
 
Chadema inawapasa kutoa sera za kusaidia maisha ya wananchi V.Nyerere analeta siasa za maji taka..achana na Mkapa tuambiane sera za kuwasaidia Wana-Arumeru

Kwa hiyo Mkapa wa CCM kusema Mwal Nyerere hakuwahi kumtajia kwamba kuna mtoto anaitwa Vincent Nyerere ndio sera za CCM?

Ukweli ni wazi kwamba Nyerere alipinga sana suala la kubinafsisha kila siku. Na hata alikataa NBC kubinafsishwa, akisema kama mabenki ya nje wanasema NBC ni kubwa sana hawewazi kuwekeza ikiwapo waondoke. Nyerere alikataa kubinafsisha hata akasema kuna siku mtakuja kubinafsisha hata magereza. Aliwauliza watu kwamba hivi mtanzania anaweza kwenda Uingereza hata aikiwa na hela akakubaliwa kupewa ardhi au shirika la UK? Na tunajua Mkapa alisimamia kwa kila nguvu kubinafsisha kila kitu. Mfano mzuri ni suala la kubinafsisha NBC, akafikia hata kukosana na wabunge waliopinga. Sasa itaingia akilini kwa kila mtu kwamba Mkapa alimwona Nyerere kama kikwazo kikubwa katika uraisi wake - hivyo si wazo la mbali kwamba inawezekana kabisa alidiriki kum"Mwakyembe".

Ubinafsishaji wa aina ya Mkapa ulimuudhi Nyerere kupita kiasi, na ikawa wazi Nyerere asingekubali Mkapa kuendelea kuwa raisi awamu ya pili.

Na kila mtu anajua baada ya kifo cha Nyerere Mkapa alibadilika isivyo kawaida!!! Akawa fisadi wa kutupwa.

Mkapa alifikia hatua ya "kuzawadiwa" hoteli kule Afrika kusini na Kampuni aliyoisaidia kupata shirika kubwa sana la umma hapa Tanzania, na akamuomba Mandela awe mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa hiyo hoteli Mandela akamtolea nje kwa maneno ya kejeli sana.

Nyie hamumfahamu Mkapa nawaambia mie. Yaani afadhali hata Mwinyi ambaye tunamsamehe kwa kuwa maovu mengi yaliyofanyika ikulu akiwa raisi yeye alikuwa akishinizwa kwa kuwa alikuwa "weak character" . Lakini sio Mkapa. Mkapa alihusika yeye mwenyewe moja kwa moja.

Kwanza Mkapa anamsema Vincent juu ya uzao wake kwa ukoo wa Nyerere, yeye je? Mkapa anataka tuseme ya "watoto" wake kweli? Aibu tupu zimejaa tukianza kwenda nyanja hizo. Tutasema na yale yasiyosemeka kwa utaratibu wa desturi zetu - ohooo!!! Msione kina Cameron wanasema tuhalalishe mambo fulani. Wanajua mengi.
 
Wanasiasa ni watu wa ajabu sana,Chadema inawapasa kutoa sera za kusaidia maisha ya wananchi V.Nyerere analeta siasa za maji taka..achana na Mkapa tuambiane sera za kuwasaidia Wana-Arumeru

Kwani Mkapa aliposema kuwa Vicenti sio mwanafamili wa ukoo wa Nyerere alikuwa anasaidiaje maisha ya wananchi? Je, Mkapa kumsema ndio kutangaza sera za kuwasaidia wana arumeru kama unavyotaka tuamini? Uongo wa mkubwa kama Mkapa ni wa ovyo kuliko maji taka ya Vicenti.
 
Keil,

Hizi habari zimenipita sana mwenzio kushoto. Nafikiri kwa sababu ya kukaa sana Sikonge tangu nilipomaliza JKT. Mengi yanayotokea Dar kwa kweli ni kusoma hapa JF, kwenye mitandao au nikiongea na Mtanzania.

Hii habari sijawahi kuisikia kabisa na kwa kweli imenishangaza mno. Nakumbuka kuangalia mazishi ya Nyerere kwenye BBC na CNN na kumuona hadi Mama Clinton akija Tanzania. Sikutegemea kuwa Mkapa atakuwa mkatili namna hiyo na mtu aliyeweka pesa mbele hadi kumtanguliza Mwalimu wake na mtu aliyemuweka madarakani.

Nakubaliana na wewe kuwa Dr. Slaa au Mbowe au Zitto, wampige STOP huyu V. Nyerere na hii habari asiiongelee tena. Kama sumu kashatema na mengine acha yaanze kushuka kwa gravitation force.

Ngoja nilale na asubuhi ntaamkia hapa kuifuatilia zaidi kama haitafutwa.

[Lali/dilagi mpola kwenuko ]
kwa kweli hii habari inaumiza sana na inatonesha vidonda ni bora waiache itafika muda wake kama BWM alikukuwa anapina maji na unga basi chaguao ni lake akoroge uji au asonge ugali ameona uzito wa maji na unga
 
Ikumbukwe, baada ya masaa machache ya kutangazwa kwa kifo cha baba wa taifa, kuna mwimbaji alitoa albamu ya nyimbo za maombelezo zilizoimbwa kwa ustadi wa hali ya juu. Hivi walijuwaje kwamba baba wa taifa angeaga dunia??????
 
Hili suala la Mkapa kuhusika na kifo cha Mwalimu halikuanzishwa na VN, nakumbuka wakati ule Mwalimu bado anaugua kule London siku moja mmoja wa binti zake alipokuwa anahojiwa na BBC alieleza kuwa tangu baba yake aanze kuugua Rais Mkapa hakujali ugonjwa wake licha ya kuwa alitaarifiwa juu ya ugonjwa. Siku moja wakati Mwalimu ameshazidiwa na ameshaota mkanda wa jeshi ndiyo Mkapa akaenda kumuona, alipofika Butiama alipomsalimia Mwalimu aligoma hata kujibu salamu yake, alimuuliza swali moja tu kuwa Ben ndiyo leo umejua kuwa naumwa? Kwa aibu Ben alijitetea kuwa alikuwa na kazi nyingi, Mwalimu akamwambia asante sana. Baada ya hapo Ben akajibaraguza kuwa anampeleka London kwa matibabu ,Mwalimu alikataa kata kata kwenda London, akamwambia wacha nife tu. Ni baada ya kubembelezwa na binti zake ndipo akakubali kwenda London lakini kwa shingo upande.Siku mbili baada ya maelezo hayo ya binti wa Mwalimu Mzee Kingunge akaenda London kwenda kudhiti utoaji wa taarifa za hali ya afya ya Mwalimu, wote wana familia walipigwa marufuku kuongea na vyombo vya habari juu ya hali ya baba wa taifa. Kama hakukuwa na njama ovu juu ya afya ya mwalimu kilichokuwa kinafichwa ni nini?
 
siku zote watoto wa nje awaaminiani so si o kosa lake mpwa msamehe..kwanza ajiulize kw anini babake alizini nje ya ndoa ndio akamzaa afadhali vicent alizaliwa wakati wazazi awajaoana so naweza kusema yawezekana nikosa la baba kukimbilia nyumba ndogo na si kumtungia mtoto jina..uwezi sema mtoto wa nje wakati ujaoa ...ukiwa umeoa na ukaza mtoto na binti mwingine hapo naweza sema serikali wanadai mtoto wanje ..lakini kama babako alikula njama na mamako kukuzaa na baadae kwa tamaa ya babako akakataa kumuoa mamayako na kukimbilia vidosho wa mjini na kuoa weewe sio mtoto nje...nenda serikalini ukaulize usije nyimwa mafao ya babako kwa k utotambua ....mwenzio anachapa lapa kujibishana na Rais aliemuuua babake wewe baki na himitizo la mtoto wa nje...Hakika nimeamini damu inanena jamani

USIMUUE MTU USITOE MIMBA KWA MABINTI NAWAAMBIA SOMENI BAIBO DAMU INAONGEA ILE ...KILICHOFANYIKA KWA VICENT NI DAMU YA BABAKE IMEMUUMA NA SASA INANEA KUPITIA MJUKUU WAKE AMBAE LEO WALIOMUU WANADAI SI MTOTO WA LA WA FAMILIA ...MUNGU LAZIMA ANENE KWA HILI WATNZANIA TUWE MACHO KUMBE YANAYOMTOKEA MWAKYEMBE YALIANZA KIPINDI CHA MKAPA SASA SIJUI MPAKA WANAAMALIZA WATAWAMALIZA WANGAPI JAMANI

Mkuu umenipa darasa hapo! thanx!
 
Mtanzania,

Mimi nadhani tuanze kwanza na mbunge wetu wa Kyela, yeye anasema amepewa sumu, jee ni kweli au?

Mkuu Rufiji,
Wapi Dr. Mwakyembe kasema amepewa sumu? Binafsi sijamsikia wala sijasoma popote pale aliposema amepewa sumu.

Akishasema mwenyewe basi wakati huo tutajadili zaidi. Hata kyela wananchi wake wanasubiri awaambie nini kinaendelea.
 
Ni nani alikuwa waziri wa afya chini ya utawala wa Kikwete?

Lakini aliyesema alidai kuwa ni Mkapa ndio aliyempa uwaziri. Lakini jee ina maana aliyekuwa Daktari wa Nyerere hakuwa na sifa za kuwa Waziri wa Afya?
 
Mkuu Keil, asante sana kwa hii, nawashauri wanaChadema wenye mapenzi ya kweli, waikate hii post, waipaste, waiprint na kuitumia kama msahafu wa kampeni!.

Kwa vile Vincent ni mtoto wa baba mdogo, CCM watamtumia mtoto halisi wa Nyerere preferably Madaraka au Makongoro ku caunter attack hii kauli ya Vincent huku CCM wakiwachagiza wazee wa familia ya Nyerere kina Chifu Wanzagi kutoa karipio kali la kutaka Nyerere aachwe apumzike kwa amani hivyo kuutumia kisingizio hicho kum disown Vincent na kum ex-communicate asizingumze lolote kumhusu Nyerere na hayo aliyozungumza ni ya kwake binafsi na sio ya kina Nyerere.

Nashauri concetration ya Chadema iachane na siasa za maji taka, ijikite kwenye issues!. Siasa hizi za maji taka na vijembe, zina hold water maeneo yenye uswahili kama ukanda wa pwani, Kanda ya Kaskazini ni issues tuu sio mipasho wala uswahili!.

Ule msimamo wangu uchaguzi Arumeru ilishaisha, bado uko pale pale!. Na kwamba kinachoendelea sasa ni kutimiza tuu matakwa ya katiba na kufiatwa tuu kwa taratibu, sheria na kanuni za uchaguzi ili kuhalalisha matokeo!.

Baba, nawewe umekosea sana tu! Nyerere hakuwa wa Familia ya nyerere tu alikuwa ni wataifa zima na sometimes Africa nzima hao unaowataja wakitaka mbinafsisha itakuwa ni makosa makubwa....ebu wajaribu tuwacheke!
Nyerere ni wakila mtu na kila mtu anahaki ya kuhoji kifo chake!
Acheni usanii!
 
Kwa hiyo Mkapa wa CCM kusema Mwal Nyerere hakuwahi kumtajia kwamba kuna mtoto anaitwa Vincent Nyerere ndio sera za CCM?

Ukweli ni wazi kwamba Nyerere alipinga sana suala la kubinafsisha kila siku. Na hata alikataa NBC kubinafsishwa, akisema kama mabenki ya nje wanasema NBC ni kubwa sana hawewazi kuwekeza ikiwapo waondoke. Nyerere alikataa kubinafsisha hata akasema kuna siku mtakuja kubinafsisha hata magereza. Aliwauliza watu kwamba hivi mtanzania anaweza kwenda Uingereza hata aikiwa na hela akakubaliwa kupewa ardhi au shirika la UK? Na tunajua Mkapa alisimamia kwa kila nguvu kubinafsisha kila kitu. Mfano mzuri ni suala la kubinafsisha NBC, akafikia hata kukosana na wabunge waliopinga. Sasa itaingia akilini kwa kila mtu kwamba Mkapa alimwona Nyerere kama kikwazo kikubwa katika uraisi wake - hivyo si wazo la mbali kwamba inawezekana kabisa alidiriki kum"Mwakyembe".

Ubinafsishaji wa aina ya Mkapa ulimuudhi Nyerere kupita kiasi, na ikawa wazi Nyerere asingekubali Mkapa kuendelea kuwa raisi awamu ya pili.

Na kila mtu anajua baada ya kifo cha Nyerere Mkapa alibadilika isivyo kawaida!!! Akawa fisadi wa kutupwa.

Mkapa alifikia hatua ya "kuzawadiwa" hoteli kule Afrika kusini na Kampuni aliyoisaidia kupata shirika kubwa sana la umma hapa Tanzania, na akamuomba Mandela awe mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa hiyo hoteli Mandela akamtolea nje kwa maneno ya kejeli sana.

Nyie hamumfahamu Mkapa nawaambia mie. Yaani afadhali hata Mwinyi ambaye tunamsamehe kwa kuwa maovu mengi yaliyofanyika ikulu akiwa raisi yeye alikuwa akishinizwa kwa kuwa alikuwa "weak character" . Lakini sio Mkapa. Mkapa alihusika yeye mwenyewe moja kwa moja.

Kwanza Mkapa anamsema Vincent juu ya uzao wake kwa ukoo wa Nyerere, yeye je? Mkapa anataka tuseme ya "watoto" wake kweli? Aibu tupu zimejaa tukianza kwenda nyanja hizo. Tutasema na yale yasiyosemeka kwa utaratibu wa desturi zetu - ohooo!!! Msione kina Cameron wanasema tuhalalishe mambo fulani. Wanajua mengi.

Naukumbuka mfano mzuri aliyoutoa marehemu JKN akipinga ubinafsishaji. Akatolea mfano kuwa hapa Tanzania tuna mabondiy wazuri sana, enzi hizo Matumla (snake boy) anavuma sana. Akaelezea kuwa huwezi mumpambanisha Matumla na Tyson. Kwanza wapo uzito tofauti na Tyson alikuwa bingwa wa Dunia kipindi kile. Lakini licha ya mifano kama hii ya kuwasema viongozi wetu ili wabadili misimamo yao hawakusikia. Leo hii tunazalisha Gold nyingi inayostabilize currency za wenzetu wakati shilingi yetu ikiendelea kuporomoka kila kukicha.
 
Back
Top Bottom