Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete na Mbowe, hawa ndio walezi wakuu wa kisiasa wa Edward Lowassa

fazili

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
13,819
18,554
Miamba hii mitano ndio inayohusika kwa kiasi kikubwa zaidi na mwanzo hadi mwisho wa maisha ya kisiasa ya Edward Lowassa.

Edward Lowassa alianza maisha ya siasa katika mikono ya Mwalimu Nyerere akiwa kijana mdogo miaka ya 60's. Mwaka 1988 Lowassa alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha ampapo alifanya kazi nzuri chini ya serikali ya rais Mwinyi.

Tunajua tangu miaka ya 90 Lowassa alishika nafasi mbalimbali za juu za uongozi kama waziri chini ya rais Mkapa na baadaye kuwa waziri mkuu chini ya rais Kikwete kuanzia mwaka 2005.

Edward Lowassa alifikia kipeo cha juu kabisa cha maisha yake kisiasa alipojiunga na CHADEMA na kuamua kugombea urais mwaka 2015. CHADEMA chini ya uongozi wa Freeman Mbowe wamehusika sana kumfanya Lowassa ajulikane zaidi ndani na nje ya nchi. Kama alivyowahi kusema mwenyewe, Lowassa anasema ni ndani ya CHADEMA tu aliweza kugombea nafasi hiyo kubwa zaidi ya kisiasa nchini na kuweza kukusanya umati mkubwa wa washabiki.

Hongera walezi wa Lowassa kisiasa, hongera Mbowe kwa kuwa mlezi wa Lowassana kumfikisha kwenye ndoto yake ya kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania. Ni matumaini yangu kuwa upo kwenye right track, songa mbele na mapambano kazi yako inaonekana.
 
Miamba hii mitano ndio inayohusika kwa kiasi kikubwa zaidi na mwanzo hadi mwisho wa maisha ya kisiasa ya Edward Lowassa.

Edward Lowassa alianza maisha ya siasa katika mikono ya Mwalimu Nyerere akiwa kijana mdogo miaka ya 60's. Mwaka 1988 Lowassa alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha ampapo alifanya kazi nzuri chini ya serikali ya rais Mwinyi.

Tunajua tangu miaka ya 90 Lowassa alishika nafasi mbalimbali za juu za uongozi kama waziri chini ya rais Mkapa na baadaye kuwa waziri mkuu chini ya rais Kikwete.

Edward Lowassa alifikia kipeo cha juu kabisa cha maisha yake kisiasa alipojiunga na CHADEMA na kuamua kugombea urais. CHADEMA chini ya uongozi wa Freeman Mbowe wamehusika sana kumfanya Lowassa ajulikane zaidi ndani na nje ya nchi. Kama alivyowahi kusema mwenyewe, Lowassa anasema ni ndani ya CHADEMA tu aliweza kugombea nafasi hiyo kubwa zaidi ya kisiasa nchini na kuweza kukusanya umati mkubwa wa washabiki.

Hongera walezi wa Lowassa kisiasa, hongera Mbowe kwa kuwa mlezi wa Lowassa. Ni matumaini yangu kuwa upo kwenye right track, songa mbele na mapambano kazi yako inaonekana.
Umeeleza kwa kifupi na vyema sana kwa jicho la ziada
 
Bangi bhana...

Mbowe huyu huyu kengeza au mwingine?

Unamjua Lowasa wewe...

Yaani Mbowe awe mlezi wa Lowasa kisiasa?

Maanina wallah...

Kikwete mwenyewe japo ni jabali la siasa za Tanzania kamwe hakua mlezi wa Lowasa kisiasa.

Mnamuoverate sana Marehemu.

Mbowe alimkaribisha CDM akiwa mwenyekiti na kumpa nafasi ya kugombea Urais, tafsiri yake bila Mbowe asingepata nafasi pale CDM.

Bila JK EL asingekuwa PM maana chaguo la wazee pale Lumumba lilikuwa Pinda at the 1st place, JK akakaza shingo akampa swaiba wake UPM mpaka yalipoharibiki ndio akarudi Kwa option ya Pinda.

Marehemu Six ndio anayeyajua mengi kati ya EL na JK na labda RA.
 
Ahahahahaha! Sisi Wahaya tunasemaga "okunywa enjai etaire" ( kuvuta bangi ambayo haijakomaa) ni kubaya sana! Jamaa eti Mbowe kumtengeneza Mzee Lowassa! Ahahahahaha!!!
 
Marehemu Six ndio anayeyajua mengi kati ya EL na JK na labda RA.
Kwa taarifa yako mzee Sita alikua anautaka u PM na hakuupata...

Mbowe hakua na chaguo hiyo 2015 zaidi ya kumkaribisha Lowasa ili apate wabunge wengi...

Lengo la Mbowe siku zote ni pesa za Ruzuku so kumpata mtu kama Lowasa ilikua deal asiloweza kilikataa....
 
Bangi bhana...

Mbowe huyu huyu kengeza au mwingine?

Unamjua Lowasa wewe...

Yaani Mbowe awe mlezi wa Lowasa kisiasa?

Maanina wallah...

Kikwete mwenyewe japo ni jabali la siasa za Tanzania kamwe hakua mlezi wa Lowasa kisiasa.
Mbowe alimshauri Lowassa mambo mengi ikiwa ni pamoja na kugombea urais kwa ticket ya CHADEMA. Mbowe alimwezesha Lowassa kutimiza ndoto yake ya muda mrefu aliyoshindwa kuitimiza ndani ya CCM; ni ndoto ya kugombea urais wa Tanzania. Mbowe alimwingiza Lowassa kwenye siasa kakamavu za upinzani ambazo Lowassa kamwe hakuwahi kuzifanya na Lowassa yeye kwa kinywa chake mwenyewe alimshukuru Mbowe kwa dhati kabisa kwamba amekuwa mtu muhimu sana katika maisha yake ya kisiasa, na kwamba bila Mbowe yeye Lowassa asingegombea urais wa Tanzania. Mbowe alimwacha Lowassa arudi alikotoka bila kejeli wala manung'uniko yoyote.
 
Duh haya sawa.
 
Kwa taarifa yako mzee Sita alikua anautaka u PM na hakuupata...

Mbowe hakua na chaguo hiyo 2015 zaidi ya kumkaribisha Lowasa ili apate wabunge wengi...

Lengo la Mbowe siku zote ni pesa za Ruzuku so kumpata mtu kama Lowasa ilikua deal asiloweza kilikataa....
Sawa tufanye win win situation.

Mbowe apate wabunge wengi na ela ya ruzuku na Lowasa apate nafasi ya kukusanya umati nchi nzima na kuwa maarufu .
 
Lowasa apate nafasi ya kukusanya umati nchi nzima na kuwa maarufu .
Bila shaka hukumjua Lowasa...

Chadema hamjawahi kukusanya watu wengi kwenye mikutano kabla ya Lowasa...

Umaarufu wa Lowasa ulianza tangu 1995 anaenda kuchukua fomu ya uraisi kwa style ya pekee..

Jifunzeni historia kabla hamjaanza kuongopea watu...

Ukiniuliza kati ya Chadema na Lowasa nani amempa mwenzake umaarufu takujibu Lowasa bila kusita ...
 
Mpaka Mbowe nae ni mlezi wa siasa wa Lowassa? Ama kweli ukifa yanaongelewa mengi ya uzushi...

Mbowe alikuwa anapiga disco bilicanas wakati Tayari Lowass waziri ..Leo kageuka mlezi wa siasa wa Lowassa?
Hawa jamaa wanajipakulia minyama tu...

Wanajua kila mtu nyumbu humu...
 
Mpaka Mbowe nae ni mlezi wa siasa wa Lowassa? Ama kweli ukifa yanaongelewa mengi ya uzushi...

Mbowe alikuwa anapiga disco bilicanas wakati Tayari Lowass waziri ..Leo kageuka mlezi wa siasa wa Lowassa?
Kuna wajinga wajinga wengi sana hapa JF.
Mbowe mlezi wa siasa wa Lowassa kweli?
 
Bangi bhana...

Mbowe huyu huyu kengeza au mwingine?

Unamjua Lowasa wewe...

Yaani Mbowe awe mlezi wa Lowasa kisiasa?

Maanina wallah...

Kikwete mwenyewe japo ni jabali la siasa za Tanzania kamwe hakua mlezi wa Lowasa kisiasa.
Eti Mbowe awe mlezi Lowasss wewe kweli ni pimbi mwenye Phd
 
Mnamuoverate sana Marehemu.

Mbowe alimkaribisha CDM akiwa mwenyekiti na kumpa nafasi ya kugombea Urais, tafsiri yake bila Mbowe asingepata nafasi pale CDM.

Bila JK EL asingekuwa PM maana chaguo la wazee pale Lumumba lilikuwa Pinda at the 1st place, JK akakaza shingo akampa swaiba wake UPM mpaka yalipoharibiki ndio akarudi Kwa option ya Pinda.

Marehemu Six ndio anayeyajua mengi kati ya EL na JK na labda RA.
Mlezi wa Lowassa kisiasa ni wakoloni bila wakoloni Nyerere asingekuwa Rais, bila Nyerere mwinyi asingekuwa Rais, bila mwinyi mkapa asingekuwa Rais bila mkapa asingekuwa Rais bila mkapa kikwete asingekuwa Rais ..,..sioni kama hoja yako ina mashiko
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom