Mkuu, CV ya Mtanzania inajulikana sana hapa JF na hata jina lake, anapoishi, kisomo chake na kazi alizofanya na anayoendelea kufanya sasa.
Mgongo wa shule, mhhhhh wewe mgeni basi maana shule alimaliza miaka ya 90 mwishoni na siyo UK. Ukitaka kujua zaidi, basi uliza nani aligombea ubunge na Mwakyembe mwaka 2010 na anaishi UK.
Mtanzania, nakubaliana na wewe kabisa kwa unayoyasema. Ila kwa watu kama Nyerere kama kweli alitakiwa kuondoshwa basi kuna mkono wa watu wengi na si Mkapa peke yake. Lazima kuna nguvu Mkapa aliamini itamsaidia kama mambo yakianza kuvuja. Hadi sasa tunajua kuwa UK pia walifaidi na kuwepo kwa Mkapa kwa mambo kama Radar ya jeshi na madudu mengine mengi ambayo mie si mtaalamu sana hapa.
Jana nilikuwa naangalia jinsi Osama bin Laden alivyouawa. Jinsi mpango mzima ulivyokuwa na nikashangaa sana kwamba kwa miaka 8, Bush hakuweza kabisa kumkamata Osama. Kabla ya uchaguzi wa pili, siku tatu kabla, zikatoka Video za Osama kuhusu uchaguzi wa USA kuwa "wakimchagua Bush, atashambulia USA." Kila mdadisi wa mambo akajua kuwa Bush na Osama family ni marafiki. Watu wakachukia na kumpigia kura za hasira Bush. Mie kwa upande naamini maneno ya VN yanaweza kuwa ya kweli kwa kuangalia siasa za UK/USA kwa miaka mingi zilivyokuwa na upande mwingine naamini kuwa JKN alikufa Natural Death. Nyerere alikuwa kikwazo kwao kuja Tanzania kujichotea mali.
Ila ukiangalia madudu aliyoyafanya Mkapa baada ya kifo cha Nyerere na kukumbuka tabia za Nyerere na ukali wake, unapata sana shida kuamini kama Mkapa hakuhusika kuharakisha kifo cha Nyerere ili aweze kumaliza miradi yake mapema. Ukisoma ile thread ya mwaka jana ya somebody SHIMBO ambayo watu walijadili bila kumtaja Mkapa, unazidi kupata wasiwasi. Vyovyote vile ilivyokuwa, kifo cha NYERERE ilikuwa neema kubwa sana kwa Mkapa na Watanzania fulani. Nina imani kuna siku siri zitafumuka kutoka hukohuko UK kama ambavyo wengi walipinga ununuzi wa Rada ya jeshi kuwa ulikuwa halali. Hata serikali yenyewe ya UK walidai hivyo na yule Mama wa UK (jina limenitoka) ikapelekea ajiuzulu na kugombana na PM Tony Blair. Leo hii tunajua ukweli kuwa Tony Blair alituibia.
Mkapa alifanya makosa kuja na Personal Attack kwa kijana mdogo kama VN. Nafikiri hili ndiyo lilikuwa kosa kubwa sana kwake. Hawa vijana hata wakiropoka huwa wanasamehewa. Ingelifaa aseme Nchemba Mwigulu au Nape na si Mkapa. Ila mie nachosema,VN na Chadema waachane nayo maana kama ni sumu imeshatosha na kuendelea ni kutia chumvi utakaoharibu radha.
Mkuu nakubaliana nawe kuhusu hizo sheria za UK,japo uwepo wa mtu huko tena mgeni si lazima kujua sheria zao zinazofanya kazi,nina hakika hata wewe utakua mmoja wa wale foreigners ambao mnaishi kwa mgongo wa shule huku mkipigania mkono kwenda kinywani,either kwa u kitchen porter,warehousing au care,maana ndio kazi zetu sisi foreigners huko,bahati nzuri Mungu alinifumbua mapema nikaukimbia huo utumwa mambo leo!point yangu ni kua unajua system za wenzetu zinazofanya kazi,kama Julius ndio alikua kikwazo cha raia wa magharibi kuja kujichotea mali huku na wakaamua kumtumia Benja kuweza kummaliza huyo babu ulitegemea siri hizo ungepewa mtu kama wewe??nafikiri kumbukumbu zako utakua umezikita zaidi kwy kifo cha former KGB ALEXANDER LITVINENKO ambae alikua poisoned na KGB na alifia Uk na uchunguzi wa ugonjwa wake uliusisha mpaka M16(S.I.S) na kupigiwa kelele sana na serikali ya Uk,ila lazima uelewe kifo cha huyo jamaha wa KGB kilifuatiliwa sana na Waingereza kwa kua ni mtu waliyekua wanamtumia kwa manufaa yao wenyewe dhidi ya Russia!kwa hiyo mkuu kujifanya kua kwa kua uko Uk ndio ujue sheria zao zote na sìri zao huo ni uongo uliotukuka,sheria nyingi utakazokua unazijua wewe ni za home office kule Croydon kwa kua ndizo zinazokugusa moja kwa moja!