Vijembe na maaskofu halafu ushinde vita sahau!

Vijembe na maaskofu halafu ushinde vita sahau!

Sina hakika lakina dhamira yangu inanituma niseme haya; unaweza ukawa ni "jiwe", pamoja na nguvu zote za kimamlaka lakini kuna wakati busara lazima kiongozi ikuongoze.

Nchi yetu haina dini, lakini watu wake wana dini zao na ndo maana wanapoapishwa wanashika vitabu vya dini kubwa mbili nchini....kutumia nafasi tulizonazo kuanza kuwapiga vijembe viongozi wetu wa kiroho haijakaa sawa na haiwezi kukuacha salama. Waraka wao haukumtaja mtu wala siamini kama ulilenga kumkomoa mtu bali ni sauti ya kiroho inayotaka kuponya taifa.

Unawatu hao watu ni waumini wao...yaani akisema mwanasiasa jambo fulani na kiongozi wa kiroho akasema jambo hilo kwa kinyume chake basi muumini atafuata ya kiongozi wa kiroho... tusicheze na IMANI za watu tunaweza jibu hoja zao bila kuleta mvutano na mfarakano na tukaeleweka.....kubishana na viongozi wetu wa kiroho ni kumkosea mungu!

Maaskofu wanakuwa na NGUVU PALE WANAPOONGEA UJUMBE WA MUNGU. ASKOFU WA KANISA KATOLIKI KASOMA PHILOSOPHY NA THEOLOGY. na Bado kwa kupata huu UTUMISHI tunajtegemea COMMON SENSE yake itakuwa above normal. UJUMBE WA ASKOFU UKIWA SPECIFIC ITs just means anadata. Na kama anadata za KUMUHUSU MTU MMOJA Specific then ile COMMON sense inapaswa kumtuma kwenda direkt kwa MUHUsika. Leo mnafanya mnawaelewa maaskofu. Mlishawatukana sana humu. Kwenu ujumbe Wa Maaskofu unamuhusu MTU MMOja BASI UJUMBE HUO SIO WA MUNGU. UJUMBE wa MUNGU HUMGUSA KILA MTU. sasa cha ajabu Watu mnageuza ujumbe kama hotuba ya KISIASA ni dalili kubwa ya KUFELI NIA ILIYOKUSUDIWA. TAFAKARINI.
 
Mungu anatupenda sote, hata kambare anatupenda na kutuongoza. Isikie sauti yako ya ndani
 
je hao maaskofu wamekosa nao busara ya kuomba kikao naye na kuyazungumza kuliko kila siku kutunishiana misuli kwenye majukwaa ya kanisa na majukwaa ya siasa??
Haukumbuki alishasema yeye ni mtu anayejiamini na ukitaka kumpangia kitu ndiyo umeharibu kabisa
 
Kwa hiyo mkuu Pascal Mayalla,huyo anenwaye hana busara?
Hapa tunazungumza vitu viwili tofauti, wewe unamzungumzia mtu anayenenwa, mimi si zungumzii mtu, nazungumzia kitu kinachoitwa busara

Ili busara iweze kutumika, hatua ya kwanza ni kwa hiyo busara yenyewe, kwanza iwepo, ikiishakuwepo, ndipo sasa itumike!. Ikitokea busara yenyewe haipo, atumie busara gani, kutoka wapi?'

Jee Aachwe Aseme Tuu, By "Taking The Bitter With The Sweet", Or Atumie Busara?!.

Paskali
 
Kwahiyo maaskofu wanapenda vita? Mimi nilifikiri maaskofu ndo wazuri ktk kusamehe na kukuombea ili utulize vita. sisi maandiko ndo yanatufundisha hivyo, lakini kama kazi ya maaskofu ni kufanya vita ili ufeli basi hao maaskofu ni noma. Ngoja ninukuu vifungu.

1 Yohana 4
1 Wapenzi wangu, msimsadiki kila mtu asemaye kwamba ana Roho wa Mungu, bali chunguzeni kwa makini kama huyo mtu anaongozwa na Roho wa Mungu au la, Maana manabii wengi wa uongo wamezuka ulimwenguni.

2 Peter 2:1-22
But false prophets also arose among the people, just as there will be false teachers among you, who will secretly bring in destructive heresies, even denying the Master who bought them, bringing upon themselves swift destruction. And many will follow their sensuality, and because of them the way of truth will be blasphemed. And in their greed they will exploit you with false words. Their condemnation from long ago is not idle, and their destruction is not asleep. For if God did not spare angels when they sinned, but cast them into hell and committed them to chains of gloomy darkness to be kept until the judgment; if he did not spare the ancient world, but preserved Noah, a herald of righteousness, with seven others, when he brought a flood upon the world of the ungodly; ...

Kwa maana yakwamba maaskofu wapenda vita na malumbano na kondoo wao, yatatufanya wenda waaumini waanze kuangalia hivyo hivyo vifungu kwa makini zaidi.
Ni makosa sana kuwaita maaskofu wote kwa umoja wao kuwa hawana roho ya Mungu, hawaongozwi na roho wa Mungu na ni manabii wa uongo kwa sababu tu wametoa waraka unaowasha masokioni mwenu.

Basi kwa kuwa umejipambanua na biblia.
Nenda katika kitabu cha Samuel 1 and 2.
Some jinsi Nabii Samuel alivyomshauri Mfalme Sauli...maneno ya Samweli yakawa machungu masikioni pa mfalme...akamfanya kuwa adui na akamwinda amuangamize...akidai kuwa maonyo yake na maono yake hayajatoka kwa Mungu na hayapendi.
Hali ilikuwa mbaya hadi Sauli aliua makuhani wengi sana waliompokea Samweli na kumpa chakula.

Naamini unafahamu vyema yaliyomkuta Sauli na ufalme wake baada ya hapo.

Katika biblia hakuna aliyekuwa mkosoaji na mkemeaji mkubwa wa wafalme na watawala kama viongozi wa dini. Na wakisema ukweli walichukiwa sana na hata kuuawa na watawala...lkn hilo huwa haliwatushi wala kuwarudisha nyuma. Wako tayari kupata mateso na hata kifo kwa kusimamia kauli yao na matendo yao.

Sio mara ya kwanza viongozi hasa kutoa nyaraka zao...hawajawahi tukanwa ila leo tu ndio mnawaona manabii wa uongo.
Kweli madaraka hulevya.

Ngoja niwaonye...jana mliwakimbilia hawa hawa mnaowaita manabii wa uongo wawaombee....leo mnawatukana...kesho mnaenda tena wawaombee... inaingia akilini kweli????
 
je hao maaskofu wamekosa nao busara ya kuomba kikao naye na kuyazungumza kuliko kila siku kutunishiana misuli kwenye majukwaa ya kanisa na majukwaa ya siasa??
Mimi nakumbuka viongozi wa dini waliwahi kutaka kuonana nalo enzi za UKUTA wa CHADEMA, nadhani walishaonana !
 
Sina hakika lakina dhamira yangu inanituma niseme haya; unaweza ukawa ni "jiwe", pamoja na nguvu zote za kimamlaka lakini kuna wakati busara lazima kiongozi ikuongoze.

Nchi yetu haina dini, lakini watu wake wana dini zao na ndo maana wanapoapishwa wanashika vitabu vya dini kubwa mbili nchini....kutumia nafasi tulizonazo kuanza kuwapiga vijembe viongozi wetu wa kiroho haijakaa sawa na haiwezi kukuacha salama. Waraka wao haukumtaja mtu wala siamini kama ulilenga kumkomoa mtu bali ni sauti ya kiroho inayotaka kuponya taifa.

Unawatu hao watu ni waumini wao...yaani akisema mwanasiasa jambo fulani na kiongozi wa kiroho akasema jambo hilo kwa kinyume chake basi muumini atafuata ya kiongozi wa kiroho... tusicheze na IMANI za watu tunaweza jibu hoja zao bila kuleta mvutano na mfarakano na tukaeleweka.....kubishana na viongozi wetu wa kiroho ni kumkosea mungu!
Amina
 
Nawashangaeni nyie mnaotapatapa,

Lowassa aliwatumia na urais akaukosa,pamoja na kuwarundikia pesa za nyingi sana.
Mkuu, kuhusu Magufuli, hicho kikundi cha maaskofu wachache walioamua kutumia kinga ya dini kufanya siasa watashindwa vibaya sana,na watabaki na aibu kubwa huku wakiomba poo !

Kwanza fahamu, maaskofu wamegawanyika,hawana umoja mpaka sasa,wapo wanaomkubali Magufuli mia mia,na wengine ni kikundi chako kinachompinga kwa kutetea maslahi yao,ukiona huo mgawanyiko fahamu wamefeli,na kwa taarifa yako mziki wameukubali,sema nyinyi ndo mnaukuza kuwapaisha
Na wewe umeamua kuwa JIWE??
 
Anawajua walivyo ndiyo maana alisema aliyosema. Hata sisi waumini tunawajua baadhi yao na tunapambana kuwaondoa. Kazi kubwa ipo kwa wakatoliki tu kwa sababu maaskofu wao mwenye mamlaka ya kuwatoa ni papa tu
 
Jiwe kazidi kudata baada ya kujikuta ibada aliyokwenda kuabudu ikiongozwa na kaimu Paroko. Anahisi maaskofu hawataki kumuona na hii inazidi kumtesa.
 
kati ya marais wa hovyo ambao ccm imewahi kuliachia taifa huyu ni namba moja, hapa kwakweli tanzania tulilambishwa mavi.rais gani anaishi kwa majingu wakat wote kuhangaika na.vitu vidogo vidogo
 
hawa maaskofu ambao wengi ni mafisadi bora niwe mpagani tu,nakumbuka jinsi gani viongozi wa dini walivyochochea mauaji ya kimbari Rwanda.Binadamu ni binadamu tu
Hata upagani ni dini mkuu na inafika point katika jamii lazima mtambulike na upagani wenu!
 
kati ya marais wa hovyo ambao ccm imewahi kuliachia taifa huyu ni namba moja, hapa kwakweli tanzania tulilambishwa mavi.rais gani anaishi kwa majingu wakat wote kuhangaika na.vitu vidogo vidogo
Matamko yake mengi ni ya kuropoka tu! Laana za damu za watu alizozitanguliza mbele ya haki ndiyo zinazomuuandama, ila kwa vile ameanza kumzihaki M/Mungu, nafikili mwisho wa jiwe umekaribia"Kuwa chizi siyo lazima uvue nguo! "
 
Nawashangaeni nyie mnaotapatapa,

Lowassa aliwatumia na urais akaukosa,pamoja na kuwarundikia pesa za nyingi sana.
Mkuu, kuhusu Magufuli, hicho kikundi cha maaskofu wachache walioamua kutumia kinga ya dini kufanya siasa watashindwa vibaya sana,na watabaki na aibu kubwa huku wakiomba poo !

Kwanza fahamu, maaskofu wamegawanyika,hawana umoja mpaka sasa,wapo wanaomkubali Magufuli mia mia,na wengine ni kikundi chako kinachompinga kwa kutetea maslahi yao,ukiona huo mgawanyiko fahamu wamefeli,na kwa taarifa yako mziki wameukubali,sema nyinyi ndo mnaukuza kuwapaisha
Nafikiri anayewajibu jukwaani ndo anawapaisha na kwa nini uhusishe CHADEMA kwenye hoja kama hii?
 
Back
Top Bottom