Vijembe na maaskofu halafu ushinde vita sahau!

Vijembe na maaskofu halafu ushinde vita sahau!

mi nadhani magu angetumia busara tu kujibu hoja za viongozi wa kiroho mbona ata enzi za manabii na mitume waliandika waraka kwa tawala za kifalme, Amani aliandika waraka uliowafanya wayahudi wa haha biblia inasema hadi walishindwa kula na kunywa. ...mbona hakukua na neno baya wala kejeli kwene waraka wa viongozi wa dini, I think magu atambue dini kwanza siasa baadae tawala nying za kifalme zilidondoka kwa sababu ya kukebehi na kudharau yasemwayo na viongozi wa kiroho. ......Afadhali basi ata angekaa kimya kuliko kujibu vile as if hana dini wala hajawai sikia neno la biblia kuhusu waraka wakiroho. .........shida ya raisi ni moja tu kashatengeneza mentality yakutokukosolewa imagine huo waraka ungesifia si angewaita ikulu maaskofu. ....ila wanasiasa bhnaa
 
Jana Gentamycin alitoa ushauri ashauriwe mapema asome hotuba atakayoandikiwa ili asiropoke, lakini wapi!! Kaanza tu huyo! Kaibuka na njaa za Maaskofu kukosa sadaka. Yaani Muumini uliyebatizwa na unakomunika unapokwenda kanisani unadiriki kumwambia askofu wako analilia sadaka? Mungu usikubali watu kwa madaraka yao waendelee kukashfu watumishi wako, TENDA SASA!
Maaskofu hawa tuwajuao haswa wa KKT ambao hugombania madaraka mpk kupelekana kortini na mpk wkt mwingine serikali kuingilia kati kusuruhisha migogoro yao?
Leo mnataka kuwapa u-mungu?
Hebu acheni kbsaa utani.
 
Yeye ana utakatifu gani si bora Maaskofu wamesema machache? Wangetaka kumwaga kila kitu pangekalika? Huyu aliyekabidhi kimada nyumba ya serikali na juzi kazaa na mke wa mtu ndo wa kumsifia udhu?
Una ushahidi au unaropoka tu kisa umetaitiwa ndg?
 
Watu mnaodhani mkuu atapata shida eti kwa kudharau habari ya maaskofu mnajidanganya bule.maaskofu ni watu na si lazima waaminike kama MUNGU.wanaweza kutumika pia kuharibu amani ya nchi.mmesahau pia kabla ya uchaguzi walisema tuombe MUNGU.hawa hawa.so ina maana yale maombi yao hayakua na nguvu?ya kwamba aliyekuja siyo kwa matokeo ya maombi yao?mimi ni mkristo tena mkristo sahihi..nasema hawa maaskofu wawe wanasiasa badala ya kuponya kiroho.wanaodhani nchi itayumba kwa sababu ya maaskofu wetu wa namna hii naamini haitatokea hivyo na Rais huyu tutamuona anakatiza mpaka mwisho wake.jambo la wakati tu.

JAH RASTAFARI MORNING AFRICA
 
Hivi si juzi tu (siku ya Pasaka) aliongea ndani ya kanisa kwa upole pale St. Joseph, Dar, sasa iweje tena leo anawarushia mawe?
 
Wapo miamba waliokuwa na ushawishi,ubabe namafunzo ya kijeshi lkn waliishia pabaya kutokana na kukosa hekima na busara! Tusikilizane na kuheshimiana huo ndiyo msingi wa maendeleo endelevu.
 
je hao maaskofu wamekosa nao busara ya kuomba kikao naye na kuyazungumza kuliko kila siku kutunishiana misuli kwenye majukwaa ya kanisa na majukwaa ya siasa??
Umesahau wewe, viongozi wa dini waliomba wakutane nae tangu 2016 ameshupaza shingo. Lakini amini maneno yangu, Mungu anapouangusha ufalme kwanza huufitinisha!!
 
Umesahau wewe, viongozi wa dini waliomba wakutane nae tangu 2016 ameshupaza shingo. Lakini amini maneno yangu, Mungu anapouangusha ufalme kwanza huufitinisha!!
Rais ni taasisi.
Wasubiri tu ombi lao litajibiwa
 
Watu mnaodhani mkuu atapata shida eti kwa kudharau habari ya maaskofu mnajidanganya bule.maaskofu ni watu na si lazima waaminike kama MUNGU.wanaweza kutumika pia kuharibu amani ya nchi.mmesahau pia kabla ya uchaguzi walisema tuombe MUNGU.hawa hawa.so ina maana yale maombi yao hayakua na nguvu?ya kwamba aliyekuja siyo kwa matokeo ya maombi yao?mimi ni mkristo tena mkristo sahihi..nasema hawa maaskofu wawe wanasiasa badala ya kuponya kiroho.wanaodhani nchi itayumba kwa sababu ya maaskofu wetu wa namna hii naamini haitatokea hivyo na Rais huyu tutamuona anakatiza mpaka mwisho wake.jambo la wakati tu.

JAH RASTAFARI MORNING AFRICA
Nina wasiwasi kama huu ushauri wako ni wa kumtakia heri kiongozi wetu mpendwa.

Huenda sasa kuna mapandikizi kwa ajili ya kusifia na kuipotosha kweli ili nchi izidi kupotea. MSIFANYE HIVYO TAFADHALI
 
Hivi kuna mtu timamu anayemwelewa huyo ajiitaye jiwe ukitoa hawa wanaolipwa kusifia?
 
Rais ni taasisi.
Wasubiri tu ombi lao litajibiwa
Sasa ulikuwa unaandika nini? Angalieni wote mnaiga jinsi anavyo overlook!! Akikosea yeye na nyie washereheshaji wake wote mnafuata mkumbo.
 
Sina hakika lakina dhamira yangu inanituma niseme haya; unaweza ukawa ni "jiwe", pamoja na nguvu zote za kimamlaka lakini kuna wakati busara lazima kiongozi ikuongoze.

Nchi yetu haina dini, lakini watu wake wana dini zao na ndo maana wanapoapishwa wanashika vitabu vya dini kubwa mbili nchini....kutumia nafasi tulizonazo kuanza kuwapiga vijembe viongozi wetu wa kiroho haijakaa sawa na haiwezi kukuacha salama. Waraka wao haukumtaja mtu wala siamini kama ulilenga kumkomoa mtu bali ni sauti ya kiroho inayotaka kuponya taifa.

Unawatu hao watu ni waumini wao...yaani akisema mwanasiasa jambo fulani na kiongozi wa kiroho akasema jambo hilo kwa kinyume chake basi muumini atafuata ya kiongozi wa kiroho... tusicheze na IMANI za watu tunaweza jibu hoja zao bila kuleta mvutano na mfarakano na tukaeleweka.....kubishana na viongozi wetu wa kiroho ni kumkosea mungu!
NAsubiri nione gwajima kwanza akipata laana kwa kumnanihii pengo then nitajipanga kuona kwa magufuli, otherwise, mtabaki kudanganyana tu laana laaana. Au laana hizo za kanisa zinachagua viumbe?
 
Nina wasiwasi kama huu ushauri wako ni wa kumtakia heri kiongozi wetu mpendwa.

Huenda sasa kuna mapandikizi kwa ajili ya kusifia na kuipotosha kweli ili nchi izidi kupotea. MSIFANYE HIVYO TAFADHALI
Wewe ni MUNGU mpaka kweli uijue peke yako?unadhani mawazo yako hayawezi kua potofu?uhalisia unaonekana.mwaka juzi tulisema nini,mwaka jana tulisema nini,na leo watu wanapinga walichokiwazia kiwepo.acha tusonge mbele


JAH RASTAFARI MORNING AFRICA
 
Ashinde mara ngapi? Ingia ofisi ya uma leo kisha toa rushwa kienyeji kama zamani uone kama utampata mtu
 
Kwahiyo maaskofu wanapenda vita? Mimi nilifikiri maaskofu ndo wazuri ktk kusamehe na kukuombea ili utulize vita. sisi maandiko ndo yanatufundisha hivyo, lakini kama kazi ya maaskofu ni kufanya vita ili ufeli basi hao maaskofu ni noma. Ngoja ninukuu vifungu.

1 Yohana 4
1 Wapenzi wangu, msimsadiki kila mtu asemaye kwamba ana Roho wa Mungu, bali chunguzeni kwa makini kama huyo mtu anaongozwa na Roho wa Mungu au la, Maana manabii wengi wa uongo wamezuka ulimwenguni.

2 Peter 2:1-22
But false prophets also arose among the people, just as there will be false teachers among you, who will secretly bring in destructive heresies, even denying the Master who bought them, bringing upon themselves swift destruction. And many will follow their sensuality, and because of them the way of truth will be blasphemed. And in their greed they will exploit you with false words. Their condemnation from long ago is not idle, and their destruction is not asleep. For if God did not spare angels when they sinned, but cast them into hell and committed them to chains of gloomy darkness to be kept until the judgment; if he did not spare the ancient world, but preserved Noah, a herald of righteousness, with seven others, when he brought a flood upon the world of the ungodly; ...

Kwa maana yakwamba maaskofu wapenda vita na malumbano na kondoo wao, yatatufanya wenda waaumini waanze kuangalia hivyo hivyo vifungu kwa makini zaidi.
Soma maandiko vizuri, viongozi wa dini kwa miaka yote ya uhai wa ulimwengu, walifanya kazi kubwa ya kufundisha, kuonya na kushauri watawala, tena wazi wazi, walitumia nafasi zao kuhakikisha kwamba jamii wanazoishi zinakuwa na kuheshimiana!
Viongozi watawala walipokaidi walikutana na mapigo ya ghadhabu ya Mungu.

Musa baada ya kumsihi sana farao awaache wana wa Israel wakamtumikie Mungu wao, alikaidi mara kadhaa mpaka alipokutana na pigo takatifu kutoka kwa Mungu, baada ya pigo hilo alinyoosha mikono na kuwaruhusu waisrael kuondoka, Farao alijiona mkosaji kuwaacha waisrael waende, akaamuru majeshi yake yenye nguvu kuwafuata ili warudi Misri, tunajua kilichofuata? Majeshi ya Farao yenye nguvu, yaliishia katika bahari ya shamu, hawakuonekana tena!!!
Tusicheze na Mungu kwa kuwa na majeshi na silaha nzito za kijeshi, Mungu akighadhibika, hivyo vyote havitafaa kitu kutuacha salama.
Nasisitiza, nchi yetu ni nzuri sana, ni tamu mno, lakini taratiibu tunaiharibu kwa sababu ya viburi, jeuri na dhulma., Mungu wetu akichoshwa na matendo haya, hakika tutajuta!!!
 
Back
Top Bottom