Vijembe na maaskofu halafu ushinde vita sahau!

Vijembe na maaskofu halafu ushinde vita sahau!

DR. MWAKABANJE

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2012
Posts
1,986
Reaction score
3,151
Sina hakika lakina dhamira yangu inanituma niseme haya; unaweza ukawa ni "jiwe", pamoja na nguvu zote za kimamlaka lakini kuna wakati busara lazima kiongozi ikuongoze.

Nchi yetu haina dini, lakini watu wake wana dini zao na ndo maana wanapoapishwa wanashika vitabu vya dini kubwa mbili nchini....kutumia nafasi tulizonazo kuanza kuwapiga vijembe viongozi wetu wa kiroho haijakaa sawa na haiwezi kukuacha salama. Waraka wao haukumtaja mtu wala siamini kama ulilenga kumkomoa mtu bali ni sauti ya kiroho inayotaka kuponya taifa.

Unawatu hao watu ni waumini wao...yaani akisema mwanasiasa jambo fulani na kiongozi wa kiroho akasema jambo hilo kwa kinyume chake basi muumini atafuata ya kiongozi wa kiroho... tusicheze na IMANI za watu tunaweza jibu hoja zao bila kuleta mvutano na mfarakano na tukaeleweka.....kubishana na viongozi wetu wa kiroho ni kumkosea mungu!
 
Siasa na mamlaka vinamlevya mtu hadi haoni kinachoweza mzuia hapa duniani..
Haya ni mamlaka ya kidunia,uliyepewa na wananchi (wote tutakufa tutaiacha dunia)..hatudumu milele..kumbuka uliwaomba wakuombee,unaenda kanisani...
Usishupaze shingo,mamlaka yasikukoseshe wewe na muumba wako,kuna kitu unatakiwa kukujua sema bila unyenyekevu hauwez sikia..
Jitathmin.
 
Sina hakika lakina dhamira yangu inanituma niseme haya; unaweza ukawa ni "jiwe", pamoja na nguvu zote za kimamlaka lakini kuna wakati busara lazima kiongozi ikuongoze.

Nchi yetu haina dini, lakini watu wake wana dini zao na ndo maana wanapoapishwa wanashika vitabu vya dini kubwa mbili nchini....kutumia nafasi tulizonazo kuanza kuwapiga vijembe viongozi wetu wa kiroho haijakaa sawa na haiwezi kukuacha salama. Waraka wao haukumtaja mtu wala siamini kama ulilenga kumkomoa mtu bali ni sauti ya kiroho inayotaka kuponya taifa.

Unawatu hao watu ni waumini wao...yaani akisema mwanasiasa jambo fulani na kiongozi wa kiroho akasema jambo hilo kwa kinyume chake basi muumini atafuata ya kiongozi wa kiroho... tusicheze na IMANI za watu tunaweza jibu hoja zao bila kuleta mvutano na mfarakano na tukaeleweka.....kubishana na viongozi wetu wa kiroho ni kumkosea mungu!
Alaaniwe aliyelisukumiza hili jiwe mpaka likaingia white house.
 
Sasa anashindwa nini kuwakaribisha Ikulu ili wazungumze mustakabali wa nchi kiunagaubaga badala ya kuonyesha dharau kuhusu waraka zao na kuongea uongo kwenye majukwaa?

je hao maaskofu wamekosa nao busara ya kuomba kikao naye na kuyazungumza kuliko kila siku kutunishiana misuli kwenye majukwaa ya kanisa na majukwaa ya siasa??
 
Yaani kitendo tu cha maaskofu kukaa pamoja, wakajadili na kuandika hizo nyaraka mbili kutoka KKKT na RC/TEC kinaashiria waliona kuna tatizo mahali...busara ilikuwa ni kukutana nao na siyo kushindana nao.
Mungu ibariki Tanzania.
 
Acha uzushi sasa hawa wa kwetu wanajitahidi ili kuondoa mauaji haya kukithiri nchini. Na ndityo kuna mafisadi katika dini lakini wi wengi kama unavyotaka kutuaminisha. Mbona huyo dhalimu yeye ni jizi na fisadi la kutupa?

upload_2017-6-13_14-5-10-jpeg.732623

hawa maaskofu ambao wengi ni mafisadi bora niwe mpagani tu,nakumbuka jinsi gani viongozi wa dini walivyochochea mauaji ya kimbari Rwanda.Binadamu ni binadamu tu
 
Back
Top Bottom