Ndagullachrles
Member
- Jun 20, 2023
- 54
- 51
Wadau wa sekta ya utalii katika mikoa ya Kilimanjaro na Arusha,wamepaza sauti wakitaka mchakato wa mradi wa ujenzi wa kiberenge ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro usitishwe .
Kwamba mradi huo ambao utahusisha viberenge 40 katika Njia za Machame na remosho umegubikwa na changamoto nyingi na unahatarisha ajira za waongaza wageni(Guides) na wabeba mizigo(portres)wanaokadiriwa kufikia 19,000.
Ikumbukwe kuwa,Februari 16 mwaka jana,kilifanyika kikao cha wataalamu,kilichofanyika katika Jiji la Arusha na kikiongozwa na aliyekwua waziri wa maliasili na Utalii,Damas Ndumbaro na kuhusisha wadau wote wa kekta ya utalii kwa ajili ya kujadili mradi huo .
Kikao cha pili ambacho kilikujwa kifanyika mkoani Kilimanjaro machi nane kwa amelekekezo ya Mheshimiwa Ndumbaro,haukufanyika .
Vyama vya Guides,portes,Tiga,KILI-MERU,MKPS na TPO hawa ni wadau wakubwa sana wa sekta ya utalii katika milima ya Meru na Kilimanjaro ambao wameainisha athari za kiuchumi na kimazingira ednapo mradi huo utatekelezwa.
Moja ya athari hizo ni serikali kupoteza mapato ya mabilioni ya fedha hasa ikizingatiwa kuwa viwango watakavyotozwa watalii watakaotumia kiberenge ni vya chini ikilinganishwa na viwango vinavyotozwa kwa sasa kwa kila mgeni anayepanda mlima kwa maana ya Park Fees.
Kwa sasa mgeni anayepanda mlima kilimanjaro analipa dola za kimarekani 887,hii ni fedha inayolipwa moja kwa moja serikalini,lakini kama mradi huo utatekelezwa,mgeni atalipa dola za kimarekani 140 kwa siku na park fees ya dola 20 tu.
"Kwa hali ya kawaida,hapo serikali inajiandaa kupata hasara na siyo faida hata kama wataweza kupanda watalii 20 kwa siku (ambao watalipa dola 4,000)na wakati kama wakipanda watalii 50 kwa siku kwa njia ya kawaida serikali itakusanya UDS 44,350 kwa siku",anasema mdau mmoja wa utalii.
Katika andiko lake la kurasa tisa,mdau huyu anasema kwa takwimu zilizopo kwa mwaka wastani wa watalii 50 elfu wanapanda mlima kilimanjaro na kuingiza zaidi ya Bilioni tisa wakati watalii watakaotumia kiberenge kama watapanda watalii 250,000 kwa mwaka wataingiza mapato ya Bilioni tano tu.
ATHARI YA JAIRA KWA VIJANA
Kwa kawaida mgeni mmoja anaongozwa na mwongoza wageni mmoja(guide),mpishi mmoja na wabeba mizigo watatu hivyo mtalii mmoja anakuwa na watu watano.
Kwa hebabu hiyo kama watalii 50 elfu watapanda mlima Kilimanjaro basi watazalisha ajira ya vijana 200,000 na mpaka sasa kwa mujibu wa vyama vya porters na Guides,mlima kilimanjaro unao porters 16,640 na Guide 3,000 na kufanya jumla yao kufikia 19,640,hili ni jeshi kubwa sana.
WIZARA WANASEMAJE
Catherine Mbena,kamishana mwandamizi anayehusika na masuala ya habari Shirika la hifadhi za Taifa (Tanapa),amekataa kuzungumzia jambo hilo akisema liko ngazi ya wizara na kushauri watafutwe watu wa wizara ya maliasili na utalii.
Lakini Mkurugenzi wa Utalii wizara ya maliasili na Utalii,Theresa Mugobi naye akasema hawezi kulizungumzia suala hilo kwa kile alichodai kwanza suala la kiberenge halijui na pili yeye siyo msemaji wa wiraza.
"Mimi naripoti wa katibu Mkuu na kwa waziri,kama jambo hilo halijatoka huko mimi nalizungumzia kama nani,kwa ufupi mimi sina mamlaka ya kulizungumzia hilo,naomba sana kaka yangu",amesema kwa njia ya simu.
je unajua athari za kimazingira kama mradi huu utatekelezwa, na je wataalumu wa mazingira wanasemaje
tukutane kesho hapa hapa