Vijana wanakufa kwa ajali za bodaboda kila siku. Serikali haina taarifa au kwakuwa wahanga ni familia za kimaskini?

Serikali inatakiwa ifanye nini mkuu? Izuie vijana kuendesha boda boda?
Uwezo wa kuwadhibiti wafate sheria wanao hasa kwa hizi barabara kubwa.

Daladala ni vichwa maji zaidi ya bodaboda ila kwa kiasi fulani wanadhibitiwa na trafiki wa mchongo na walau ajali za rejareja hazipo sana, ukiskia ajali ya daladala (kwa dar) basi inakua imetokea alfajiri sana au usiku, muda ambao vazi jeupe hawapo. Chuma mbovu mbovu zipo road ila pamoja na huo ubovu wake zinafata sheria kinamna fulani.

Boda hana helment, kavaa viyebo sijui vindala au yuko peku, kabeba abiria hana helment, anakatiza hovyo kwenye mataa bila kuruhusiwa ila hamna wa kumzuia.

Wanachoogopa boda ni kupakia mishikaki na hii ni kwasababu jamaa zao kijiweni wanawasakama maana ukipakia mshkaki unawakosesha mkate, kwahiyo wanaogopana wao kwa wao na wanafata sheria za kijiwe sio za nchi.
 
serikali ilifanya kazi yake kuonyesha fursa na kuisapoti boda ikawa kazi watu wakaingia huko tatizo ni kukosa misingi na sheria zenye kuwabana kuanzia kwenye mafunzo mpka kuwa boda kamili... mbali na hapo hao maboda boda wenyewe hawajielewi hawajitambui na hawajali maisha yao huwezi endesha pikipiki kwa kasi huna kofia ngumu huna koti hujavaa viatu chombo chenyewe hakiko salama mambo yote hayo ni dereva anatakiwa awe makini ndipo serikali isimamie swala la mafunzo leseni vituo na haki za hao boda boda....

kwakua ccm wanajua ni msaada wao kipindi cha uchagizi basi hawawagusi wakijua watalipwa fadhila ila tunatengeneza janga baya sana...

leo unaweza tembea na pikipiki umewasha taa kila boda utakayelishana nae anakuambia zima taa hiyo unajiuliza anajua anachoongea au ndio kaamua kua boda hajapitia madesa kidogo
 
Sina mambo mengi

Hali ni ngumu, kila siku unasikia misiba huku na kule.
Nazungumzia hii misiba ya bodaboda, serikali iko kimya kama hamna kinachoendelea.
Je, serikali haina taarifa ya misiba hii ya bodaboda au haijali kwakuwa wahanga ni familia maskini?
Yaani juzi tu barabara ya Dar Arusha,semi,iliwatupa kando ya barabara,wakaanguka,abiria na dereva wa boda,kilichowasaidia walianguka kwenye nyasi nyingi,lakini wangeanguka kwenye lami,wangepasuka vichwa,Mungu ni mkuu.
 
Sina mambo mengi

Hali ni ngumu, kila siku unasikia misiba huku na kule.
Nazungumzia hii misiba ya bodaboda, serikali iko kimya kama hamna kinachoendelea.
Je, serikali haina taarifa ya misiba hii ya bodaboda au haijali kwakuwa wahanga ni familia maskini?
Serikali ya wapumbavu ccm inaamini bodaboda ndio muajiri mkuu nchi hii ,so haiwezi pinga shughuli hatarishi kama hiyo

Sent from my Nokia 6.2 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom