SoC02 Vijana wamepokeaje michezo ya kubahatisha (betting) ?

Stories of Change - 2022 Competition

muhin

Member
Jul 16, 2021
7
6
Mkeka au Mikeka "ni kauli zinazotamkwa kutoka kwa vijana wengi kwenye kila kona ya nchi yetu haswa vijana wa kiume ukilinganisha na wale vijana wa kike ,kwa hakika vijana ni miongoni mwa nyenzo muhimu inayotegemewa na kila taifa kwa ajili kusukuma maendeleo ya taifa husika , kwa hiyo basi vijana hutegemewa katika sekta kama vile uchumi,elimu,michezo,afya na nyinginezo ili kuleta mabadiliko chanya.

Vijana pia ni kundi linalondamwa na matatizo mengi ambayo hugawanyika kwenye makundi tofauti tofauti moja ya matatizo hayo husababishwa na kibaiologia(kimwili) sababu ni vichocheo vya homoni kwa wao kuwa juu , matatizo hayo ni kama vile anasa , starehe ambazo si salama , ulevi , uhuni wa kijinga , matumizi ya madawa ya kulevya na nyinginezo hivyo kwa hali kama hiyo serikali hutumia nguvu ya ziada kuwalinda vijana kutokana na matatizo yanayowakumbuka ili kunusuru uchumi wa taifa husika.

Kulingana na hali ya kiuchumi kutokua sawa kwa vijana wengi katika nchi zetu zinazoendelea vijana hujaribu kutumia njia mbadala ili kujikwamua kiuchumi miongoni mwa njia hizo ni hii michezo ya kubahatisha ( betting ) ambayo ukirudi nyuma kidogo mpaka mwaka 1985 kulikua na bahati nasibu ya taifa pekee , Miaka ilivyozidi kwenda kutokana na mabadiliko ya sheria za kiuchumi katika nchi yetu iliruhusu sekta iyo kujiendesha mpaka kufikia mwaka 2003 ilitengenezwa bodi ya michezo ya kubahatisha ambayo itasimamia na kuratibu michezo hiyo.

Pia mabadiko ya teknologia yanachangia ukuaji wa sekta hii ya michezo ya kubahatisha , hivyo wachezaji hubashiri michezo kama vile mpira wa miguu, ndondi au ngumi , mbio za farasi , mashine za kubahatisha (dubu) na nyinginezo.

Jinsi vijana walivyopokea michezo ya kubahatisha na jamii kwa ujumla .
Baadhi ya vijana wamepokea michezo ya kubahatisha kama njia mbadala ya ajira au kazi au biashara ambayo itawasaidia kupata mahitaji muhimu ya kimaisha hivyo basi vijana hutumia nguvu , akili , muda kwenye kujihusisha na michezo ya kubahatisha kwa lengo la kupata pesa huku wakiwa mbali kwenye kutafuta ajira , kazi au hata biashara.

Wakati vijana wakijifunga kibwebwe kwenye bahati nasibu wamesahau jambo kuwa makampuni yanayoendesha bahati nasibu yenyewe yapo kwa ajili ya biashara na kama ilivyo kote duniani hakuna mfanyabiashara mwenye lengo la kutopata faida.

Kwa ajili hiyo makampuni ya bahati nasibu yenyewe yanaingiza kiasi kikubwa cha pesa na kuwazawadia kichache kwa watu wachache tu.

Kwa ajili hiyo makampuni yenyewe yanafanya biashara lakini vijana tulio wengi tunaacha kufanya kazi au biashara na kuweka nguvu kwenye michezo ya kubahatisha huku tukisahau kuwa yenyewe makampuni yanafanya biashara.

Kwa upande mwengine michezo hii huathiri kisaikologia kwa kuongeza ulaibu kwa wachezaji na kujiona muda wowote wanaweza kuwa mamilionea kwa sababu maneno yanayotumika kuwafanya watu wacheze ni maneno ya kutia hamasa , kwa namna iyo vijana hujihusisha na kubashiri kwa siku , wiki , mwezi na hata muda mrefu kwa kubashiri licha ya kufanya kazi au kutafuta kazi au hata biashara.

Vijana walio wengi pindi wanapokuwa walaibu wa michezo ya kubahatisha husahau malengo yao hivyo kuleta matatizo mapya katika jamii kama vile matatizo ya msongo wa mawazo na mengineyo.

Kwa hali ilivyo kuna haja ya nguvu iongezeke kwa ajili ya kuwaelimisha vijana haswa kwa kuambiwa kua bahati nasibu si ajira , kazi au biashara bali ni kama lilivyo jina lake ni bahati nasibu unaweza ukacheza hata idadi ambayo haihesabiki na usiibuke kuwa mshindi.

Pia nafikiri hawa vijana wadogo wanaokua kuanzia miaka 10 -15 wapewe elimu za kutosha mashuleni juu ya kupambana kwenye maisha na si kusubiri mteremko eti uweke buku upate milioni 500 ni jambo ambalo litawafanya wasiweke kipaumbele kwenye masomo sababu wakijua pesa mtaani zinapatikana kwa urahisi.
Kwa upande wa serikali licha ya kuwa wanapata kodi kutoka kwenye makampuni hayo ya kubashiri ni vyema serikali iweke mikakati na sheria ndogondogo mfano sehemu za kubashiri zianze kufunguliwa saa 8 mchana ili vijana wajue namna ya kutafuta riziki kwa upande mwengine.

Kwa kumalizia siishuku vibaya sekta hii ya bahati nasibu kua haijaweka mikakati ya kulinda vijana haswa huku mitaani tunapoishi bali ongezeko la vijana wanaojihusisha na hili na kuacha kupambana juu ya kazi , biashara au ajira huongezeka kila baada ya siku.

Hivyo wadau , serikali na taasisi zingine zishauri njia mbadala itakayoweza kutumika ili kutatua changamoto hii inayotukabili kwenye jamii .

Rejea.
Mwananchi.(2018-04-12)."Historia ya bahati nasibu nchini".
 
Back
Top Bottom