Betting yachangia billioni 170 katika pato la taifa kwa mwaka 2022/2023

Cannabis

JF-Expert Member
Jan 20, 2014
8,943
25,284
Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT) imetimiza miaka 20 tangu kuanzishwa kwake July 01, 2003 ambapo imesema ndani ya miaka hiyo imefanikiwa kuchangia pato la Taifa kufikia Tsh. bilioni 170.43 kwa mwaka, kuongeza ajira kwa vijana na kuvutia uwekezaji wa kampuni 67 za kitaifa na kimataifa.

“Uwepo wa sekta rasmi na pia chombo cha usimamizi ambayo ni GBT imewezesha Sekta ya Michezo ya Kubahatisha kuratibiwa na kudhibitiwa kikamilifu ili kuwalinda Washiriki, Michezo hii inachagiza burudani, inachochea ushindani/ ukuaji wa biashara nchini, na kuzuia athari katika Jamii kiwemo uwezekano wa watoto kujihusisha na michezo ya kubahatisha”

“Mchango wa Sekta katika mfuko mkuu wa Serikali umekuwa ukiongezeka kila mwaka, mfano, mwaka 2006/07 mapato ya kodi yalikuwa ni Tsh 2.8 bilioni mapato hayo yameongezeka hadi Tsh. 170.4 bilioni Mwaka 2022/2023”

“Sekta imekuwa ikichangia 5% ya kodi itokanayo na michezo ya Kubashiri Matokeo (Sports Betting) katika kukuza michezo nchini”
 
Back
Top Bottom