Vijana wa Dar na Vibegi mgongoni

Vijana wa Dar na Vibegi mgongoni

Limbukeni wapo wengi sana ila sio wote wengine waneweka laptop, document, material kwa wanafunzi na wafanyakazi kama waandishi wa habari hakuna hata haja ya kuifanya topic hii ishu ya vibegi mgogngoni, Hata ikiwa fashion au mtu kaweka deki mbovu ni utashi wake inahusu...!
Naunga mkono hoja mkuu hii haituhusu
 
wengine hubeba viroba/makonyag na maji ya uhai au kilmanjaro

Speculation za hivi ndio huwa tunazipenda sie wabeba rasket ili tupuuziwe uhalisia na uzito wa tunavyobeba.Ni jambo zuri sana nikikuona unanifikiria nimebeba konyagi na kumbe begi imejaa experia z,htc one,lumias,ipads,na bahasha ndogo ya kaki iliyotuna,napeleka mzigo dukani au kwingineko.Huku mitaani kwetu nyakati za jioni utakuta teenagers wengi na hivyo virasket,ukifuatilia utakuta vimebeba viatu vya mpira,jezi,kamba za kurukia,maji ya kunywa,perfumes etc na akifika uwanjani,vitu vyote muhimu kama wallet,simu anaweka humo.akimaliza kucheza anavua nguo zenye jasho,anajimwagia maji eneo la karibu,anatoa kitaulo anajifuta vizuri,anavaa nguo nyingine,anatoa perfume anajipulizia,huyoo,ukimwona njiani yuko nadhifu kuliko nyinyi enzi zenu mnapita barabarani mkirudi na nguo zile zile za mazoezi ili watu wajue mnacheza soka au kupiga tizi,kumbe mnaleta karaha tu jezi zimejaa udongo mgongoni,jasho, kikwapa,kiatu na soksi harufu mbaya kama za jalala la machinjioni,wenyewe mlikuwa mnaning'iniza shingoni ili mtaani wajue mcheza soka kumbe unapollute environment tu,bure kabisa nyie,mijisifa tu imewajaa,ndio maana mnahoji nonsense tu hapa.
 
hii iko personal wapendwa mim pia ni mpenzi wa begi za mgongoni japokuwa wadada wengi hubeba handbag. kwa begi langu naweka vitu vingi tu hata kama sio vingi hivyo bt ni vile begi inanipa sapoti sana..
so haijalishi nimebebea nin
 
Mkuu nimempenda kwa kuwa muwazi kwenye comment yako, japo wengine wanakua wakali hadi kutetea upuuzi.
Sio wote wanabeba hivyo vibegi wanamaana sawa.

Ni kweli siyo watu wote tunaobeba au wanaobeba hivi vibegi tuna maana sawa...ila kiukweli wengi wanaobeba hivi vibegi wanakuwa na hivyo vitu nilivyoviorodhesha pale juu...sasa kwa kuondoa usumbufu mtu anaamua kubeba hicho kibegi ili aweke vitu vyake vyote vya muhimu sehemu moja. Kwani mfuko wa suruari haiwezi kuingiza hivyo vitu vyote.
 
Ni kweli kabisa...Kipindi nipo DSM siku ya Jmosi huwa natoka na Begi tupu naelekea K/Koo maana najua nikirudi nimejaza chochote...

Hii inategea mtu na mtu na lengo la mtu kubeba begi..

Mkuu Mimi hata wiki mbili hazijapita nililazimika kununua begi, ingawa siyo haya kuweka mgongoni maana hayaendani na mavazi ninayopenda Mimi kuvaa, sababu ya kununua nilienda zangu manzese shida kwenda kutafuta soksi Za mtumba, Ila nikakutana na nguo Za watoto nikasawishika kununua pamoja na mahitaji mengine nikajikuta nina rambo mbili zimetuna. Nikalazimika kununua begi ingawa nyumbani ninalo, kwa hiyo sioni shida mtu kubeba begi maana Sawa na mtu kubeba leso huwezi jua jasho litakupata saa ngapi.
 
You are know everybody at Dar es Salaam is pretend is big boss and is have laptop. I am not know why. Every bigman is have laptop. how can people know you have hidden laptop ? It simply carry a bag. wear nice cloth. be smart and you pass as respectful person. You are not carry bag they know you are daladala conductor or you not have many money. Simple trick it use.

Mkuu hii english ni kwamba unatania au upo serious?
 
Abuhuna. It understand me it not understand ? I am not know why people it not know simple english. If I am write english of inside it will say what ? I am know even deep english of countryside england. Very tough..And if you hear I am speak through the nose deep slang ???

Mkuu hiki sio kiingereza, hiki ni kimaasai, au kilatini
CC Nyani Ngabu
 
Last edited by a moderator:
Acheni ushamba hilo beg ni personal package ,unaweza weka ipad,gadgets yoyote ile ,vitabu hata condom because its safe

Definetly ... Kama mimi nabeba charge ya sim ya laptop na some time nabeba laptop yangu.. Je huu ni ushamba?
Ambaye anaona kuwa ni ushamba basi hajui kinachoendelea ..
""Kila mtu kazaliwa ili awe yeye"" by TANMO
 
Last edited by a moderator:
Abuhuna. It understand me it not understand ? I am not know why people it not know simple english. If I am write english of inside it will say what ? I am know even deep english of countryside england. Very tough..And if you hear I am speak through the nose deep slang ???

Hahahahaaaaaaaa aiseeeee.... nalala nikiwa na furahaaa..
 
Definetly ... Kama mimi nabeba charge ya sim ya laptop na some time nabeba laptop yangu.. Je huu ni ushamba?
Ambaye anaona kuwa ni ushamba basi hajui kinachoendelea ..
""Kila mtu kazaliwa ili awe yeye"" by TANMO

Kwa mfano mie nabebaga briefcase na uwa naweka kitana changu tu....
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom