Vijana wa Dar na Vibegi mgongoni

Vijana wa Dar na Vibegi mgongoni

kama si kazini basi ujue Naenda kwa demu wangu na husitake Kujua kuna nini kwenye Begi langu

Jigo
 
damn,mi lazima nibebe beg coz kuna skaftini ndani,pakti ya sigara na kibiriti,body spray,cap,powerbank,na jacket in case of weather,na vingi vidogovidogo.
 
Doh Unaonyesha hali ya kukosa kazi na kuanza kushuhulika na mambo yasiyokuhusu .... yaani Begi la mtu lipo mgengoni kwake ww limekuwasha nn ... haya ni maajabu saana na kukosa kazi.. sidhani kama ni jambo linalojuhusu saana na kuhitaji ww kulihoji , as long hakuombi msaada wa kulibeba pale anapochoka ,,.. mwishoe utkuja kuiliza kwann watu wanava mashrti
 
Hatamimi zamani nilikuwa napinga sana matumizi ya begi kazini na nilikuwa naona aibu na kuteseka na doc kwenye mabahasha. Kiukweli begi linakuweka huru sana maana unaweka kila kitu unahitaji kwa matumizi yako unapokuwa nje ya nyumbani. Mfano mi mi huwa naweka doc za kazini kiasi naweza endelea na kazi hata nikiwa nje ya ofisi, pia napata fursa ya kujaza chupa ya chai, bite,na vinywaji kwa ajili ya matumizi yangu niwapo ofisini pamoja na electronic devices. Begi limenisaidia sana kubana matumizi maana shemeji yako akisha nifungashia kwenye begi mi kazi yangu ni kutafuta nauli tu basi. Halafu nikirudi toka kazizi nikiona chochote cha kuwabebea wanangu hiwa sijisikii vibaya maaana naliamini begi langu. Nikiwa na begi langu mgongoni hata lijae vipi mwili unakuwa balanced kuliko ambavyo ningebebe mikononi mifuko ya rambo. Huwezi ona umuhimu wa begi kama umetokea kishumundu au nanjilinji.
 
Acheni ushamba wa kujibebesha mizigo kama punda eti fashion.Mijitu mizima ovyo kabisa bwana.Mbona mimi ni kijana lakini upuuzi huo umenipitia mbali.Mtakuwa mnabeba kwa ajili ya wizi tu.
Kama mimi mwenyewe kwa mapenzi yangu,naamua kubeba begi langu lenye vitu vyangu na kutembea nalo,kwanini wewe uingilie kwa kunitaka nisivae hali ya kuwa sijakubebesha wewe?.

Kipi kinachokusumbua mtu anapoamua kuvaa begi lake alilonunua kwa pesa zake na kutembea nalo?.

Kwanini unipangie jinsi ya kutumia mali yangu hali ya kuwa mimi sijakupangia wala kuingilia maisha yako?.
 
Bila shaka kipindi hicho walikuwa wakibeba kama fasheni. Je leo bado wanayabeba mgongoni mabegi kama hayo ya enzi hizo?
 
Jamaa yangu mmoja alienda Ulaya akakaa kama miaka mitano bila kurudi Tz. Aliporudi likizo siku moja nikamuona amebeba m-backpack wake mkuuubwa na mzito (kama wale wanaobeba watalii) mgongoni huku amevaa pensi lake anakataa mitaa ya Samora huku anaangalia kwa kushangaa shangaa kama watalii wanavyofanya.
Ha ha ha ha ha ha ha ha mbavu zangu [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Sioni kama kuna tatizo mtu kuweka vitu vyake kwenye kibegi hata kama siyo laptop maana vinakuwa safe. Ila kuna wengine hasa hawa vijana wanao tafuta kazi za ajira hasa maeneo ya Posta, mara nyingi kunakuwa na bahasha za A4 humo kumejaa CV, Mihogo ya kukaanga na maji ya Kandoro yale ya 1.5 ltr.
 
Ulipekua begi la watu ukajua kama hajaweka kitu? Huo ni umbeya. Wapo watu mjini wanaishi kuangalia maisha ya watu na kukosoa only
Cz kuna watu wangu wakaribu washaniambia wamezoea sana begi hata km halina kitu anabeba tuu
 
Tunabebaga upupu njoo utukabe mkuu utupole vibegi vyetu
 
Back
Top Bottom