Vijana wa Dar na Vibegi mgongoni

Vijana wa Dar na Vibegi mgongoni

Nakushauri na wewe vaa begi.

Ili u neutralize hiyo hali.

Ngumu sana kuwazuia watu kubeba mabegi.

Kwasababu kila mmoja ana mtindo wake wa maisha.

Wengine wanavaa mabegi kwa sababu za msingi ambazo haziepukiki.

Ushauri wako to some extent ni mgumu sana kutekelezeka.
Mkuu mwalimu wako wa mwandiko kiboko. Au huo ni ushairi? Au ndio mistari? Nahisi labda ghani maana hata kifasihi maandishi yana dhima...
 
Begi langu ndo ofisi na shule pia sina haja ya kuweka ma wallet mfukoni kila kitu ndani ya begi tupia mgongoni safar ya kusaka pesa ishaanza.
 
Kama dar ndo imeingia hiyo fashion ya kubeba kibegi watakuwa wameiga RCHUGGA, maana huko ndiyo swaga, but kwa chugga huwa tunaweka skafu na sweta na kamwamvuli kadogo dogo kwani hali ya hewa inabadilika badilika kila mara.
 
idawa wewe ni wa mwaka gani kwani?
Sie miaka ya nyuma 1979 baada ya vita tulikuwa na vibegi flani vyenye kamba mbili na tulibeba mgongoni, na ukibeba ulionekana mshua na upo juu sana!.

Sasa kushangaa vijana wenzako wakihusika kutumia nafasi yao ya ujana kufanya kile kilicho kwenye chati kwa sasa me NAMSHANGAA anaye_washangaa hao vijana.

But yote kwa yote ndio muda wao huo kama wakati wako ulikuwa wa kuvaa bugasi basi kizazi hiki ni cha mabegi mgongoni.
 
Hata huku Ufipani naona 'masharo' wanabeba mabegi mgongoni. Mtu yupo kijijini, anakwenda kijiweni umbali wa pua na mdomo. Ila siku nzima yupo na begi mgongoni utadhani kobe na ngao yake. Begi kubwa ila ndani kuna chaja ya simu na earphone.
Usharo ni mzigo!
 
Hahahahah!!!!!! jamani leo nilitumwa nikalipe bill ya maji tulipokuwa foleni kuNa kama wanaume wa 5 ivi wotE wana mabag mgongoni,,,, sasa ilipofika zamu ya aliekuwa mbele yangu akawa anatafuta kile kikaratasi kwenye bag lake ili alipe bahati mbaya zipu ikajiachia bila kiwango hadi vitu vikamwagika kilicho shtua masikio ya watu ni mlio wa kioo na kasha la makeup limepasuka pale chini kuja kumtazama aliedondosha ni mwanaume,,, watu tukaishiwa POZI mbaya zaidi kaacha maunga ya makeup kwenye tiles pale ofsin kwa watu,,,,, SIKU ZOTE huwaga najua mnabebaga LAPTOP kumbe ndo hayo!!!!!!!!!! DUNIA imeisha.......
 
Top secret.jpg
Top secret.jpg
 
Ungelisema Mwanaume (1) usitujumlishe.... labda alitaka kupeleka zawadi kwa sista wake au lover wake?
 
Huku vijijini wala hayo mambo hatujui. Huku kikwapa ka beberu la mbuzi. Ukisimamia show ....mhh
 
Back
Top Bottom