Vijana wa Dar na Vibegi mgongoni

Vijana wa Dar na Vibegi mgongoni

Kaka hilo liko wazi! Dar es Salaam ulitokea mtindo ambao wengi hawawezi kuamini lakini watu wengi yameshawakuta sana! Kwamba ukiwa na beg lenye komputa mpakato( laptop) umelishika mkononi wanakuja watu wako ndani ya gari wanakushika mkono halafu gari linawashwa kwa kasi, sasa ili kukwepa kuumia lazima mkono uachie na jamaa wanachukua laptop kiulaini! Sasa ili kujipunguza na kasheshe hizo watu wakabuni kuweka mgongoni na kwa kiasi kikubwa imesaidia sana, sasa wengine imekua fashion lakini chimbuko lake kubwa lilikuwa hilo!

Kweli kabisa mkuu,hasa ule mtaa wa shaban Robert wanachuo wa IFM waliipata fresh mida ya saa 2 ivi usiku..
 
Inategea wala si ushamba, Dar ni mji wa watu wa kila aina wewe ukishangaa hilo Mimi nitakushangaa wewe, sababu Za mtu kubeba begi ni zake mwenyewe. Kwanza haivunji maadiri yeyote, mwingine anabeba begi kuwekea chochote ambacho anaweza kununua huko mtaani, badala ya kubebea mfuko wa Rambo.
 
Mbona wasichana wanatembea na pochi? Humo tunaweka vitu vidogovidogo ikitokea dharula
 
Wanasema ni swaga,mi nawashangaa wanaotembea njiani wamevaa headphones zile kubwa masikioni na begi mgongoni kama zile za wacheza mpira wa mamtoni.
Wanaiga sana

Jamaa yangu mmoja alienda Ulaya akakaa kama miaka mitano bila kurudi Tz. Aliporudi likizo siku moja nikamuona amebeba m-backpack wake mkuuubwa na mzito (kama wale wanaobeba watalii) mgongoni huku amevaa pensi lake anakataa mitaa ya Samora huku anaangalia kwa kushangaa shangaa kama watalii wanavyofanya.
 
Mkuu nimecheka hadi machozi.
 
ujana ujanja ujanja tu mjini hahaha wengine huweka kinote book akikutana na mtu anaye mjua anaomba namba ya simu anaandika kwenye note book maskini hata simu hana.
 
Kaka hilo liko wazi! Dar es Salaam ulitokea mtindo ambao wengi hawawezi kuamini lakini watu wengi yameshawakuta sana! Kwamba ukiwa na beg lenye komputa mpakato( laptop) umelishika mkononi wanakuja watu wako ndani ya gari wanakushika mkono halafu gari linawashwa kwa kasi, sasa ili kukwepa kuumia lazima mkono uachie na jamaa wanachukua laptop kiulaini! Sasa ili kujipunguza na kasheshe hizo watu wakabuni kuweka mgongoni na kwa kiasi kikubwa imesaidia sana, sasa wengine imekua fashion lakini chimbuko lake kubwa lilikuwa hilo!

Mkuu Asante umejaribu kuleta ufafanuzi kuhusu hili, sasa vipi hawa wanaotembea na Vibegi tena havina kitu ndani tuwaite vipi kama sio ulimbukeni.
 
Ushamba ni kuzurura na begi kutwa nzima na ndani hamna kitu, wengi wao hawajui kwa nini wanatembea na Vibegi mgongoni.

mkuu hivi mtu ajitwishe mbegi cku nzima pasipo sababu yeyote? ila nnachojua mie mjini mishe nyingi ukijaribu wafatilia sana hao vijana mizunguko yao mwisho wa cku utachoka mwenyewe, ukilikuta tupu ujue keshatua mzigo.
 
Back
Top Bottom