Vijana lazima wawe washiriki hai na wanufaika muhimu katika miradi ya Ukanda Mmoja, Njia Moja

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,036
VCG111402385791.jpg


Wataalamu waliohudhuria Kongamano la Mkutano wa Mtandao wa majadiliano kuhusu Ukanda Mmoja, Njia Moja wamesema kuwa pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja, ambalo linalenga kuharakisha ukuaji wa pamoja na maendeleo endelevu duniani kote kupitia uratibu imara wa sera, muunganisho, biashara isiyo na vizuizi, ushirikiano wa kifedha na uhusiano kati ya watu na watu, linapaswa kuhakikisha vijana wanakuwa washiriki hai na wanufaika muhimu.

Katika nchi nyingi za Afrika zilizojiunga na Ukanda Mmoja, Njia Moja, vijana wanachukua asilimia kubwa ya idadi ya watu na ni kundi muhimu ndani ya jamii zao. Hivyo wataalamu hao wanaona kuwa kama pendekezo hili linataka kufikia matarajio yake ya kuwa mkakati wa maendeleo na ushirikiano wa kimataifa wa muda mrefu, basi linahitaji vijana kulimiliki na kuliendeleza katika siku zijazo.

Akizungumza kwenye kongamano hilo Mkurugenzi wa kituo cha Utafiti cha Afrika na China (CACS) katika chuo kikuu cha Johannesburg, David Monyae amesema vijana wanahitaji kushirikishwa zaidi na kuwekwa mstari wa mbele kwa kuhakikisha inajengwa miundombinu ya kuwafungulia njia zitakazowaunganishwa pamoja, zitakazowapa fursa za kufanya biashara na kuondoa matabaka kwenye jamii.

“Vijana wanaweza kubeba jukumu muhimu kwa maana hiyo ni lazima tuhakikishe kwamba wako mbele kwenye miradi mbalimbali, kwani tukifanya hivyo sio tu itaondoa shinikizo la ajira, bali pia itawafanya waende mbali zaidi ya pale tunapofikiria.”

Kama alivyosema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kwamba "Vijana ndio huamua kama tutafikia Malengo ya Maendeleo Endelevu ya 2030 au la." Wazo hili kwa bahati nzuri hata Rais Xi Jinping wa China pia analo. Kwa maoni ya rais Xi anaona kuwa "Vijana ni tumaini la nchi na mustakabali wa taifa", hivyo pendekezo hili la Ukanda Mmoja, Njia Moja, pia linajumuisha mawasiliano ya vijana na elimu kwa vijana, zikiwa kama hatua mbili zilizopewa kipaumbele ili kufikia malengo yake makuu.

Takwimu zilizotolewa hivi karibuni na Umoja wa Mataifa na Benki ya Dunia zinaonesha kuwa kwa ujumla, idadi ya watu wenye umri wa miaka 15-24 ambao hawajaajiriwa wala hawafuatilii elimu au mafunzo ni zaidi ya mtu mmoja kati ya kumi katika nchi nyingi za Ukanda Mmoja, Njia Moja. Hivyo kuna kila sababu ya kuwashirikisha zaidi vijana, ikiwa ni pamoja na kuweka miundo mbinu ya elimu na kutoa fursa nyingi za ajira kupitia miradi hii.

Pamoja na hayo yote, ni dhahiri kwamba vijana wakiwezeshwa wanakuwa chachu ya mabadiliko ya kiuchumi na kijamii. Matokeo ya Ukanda Mmoja, Njia Moja katika maendeleo endelevu ya nchi zinazoshiriki yangeimarishwa kwa kiasi kikubwa, huku uwekezaji wake ungeundwa ili kujumuisha au kuchangia katika upanuzi wa rasilimali za afya, kijamii na kiuchumi za vijana.

Hassan Khannenje, ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Kimataifa ya HORN ya Tafiti za Kimkakati, amesema vijana ni injini ya ukuaji wa uchumi kwani wanatoa nguvu katika shughuli za kiuchumi. Pia vijana wanajumuisha idadi kubwa ya watu, sio nchini Kenya tu bali katika bara zima la Afrika. Kwa hiyo kushirikishwa kikamlifu kwenye miradi hii ya Ukanda Mmoja, Njia Moja, na kuelewa thamani yake sio kwa siku za sasa tu, bali hata kwa mustakabali wa mataifa yao, hili ni jambo muhimu sana.

“Katika utekelezaji wa miradi hii ya Ukanda Mmoja, Njia Moja vijana lazima wapewe kipaumbele na kupatiwa fursa kamili.

Ili kusonga mbele bila ya kizuizi, umakini mkubwa zaidi unahitaji kutolewa katika kuwasaidia vijana kuwa washiriki hai zaidi na wanufaika wa miradi ya Ukanda Mmoja, Njia Moja, kwa sababu vijana ni wastahimilivu na wana afya njema, na kuwahusisha kikamilifu ndio msingi wa utulivu na ustawi wa nchi yoyote.
 
Back
Top Bottom