Pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja” halina lengo la kukandamiza upande wowote

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,036
VCG111255056687.jpg


Mwaka 2013, rais wa China, Xi Jinping, alitoa Pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja” (BRI), ambalo miaka 10 baadaye, limesifiwa sana na jamii ya kimataifa kama ‘mradi wa karne’.

Likiwa na mtandao mkubwa wa usafiri, nishati, na mawasiliano, unaolenga kuunganisha biashara za baharini na nchi kavu, BRI imeendelea kupanuka kutoka Asia mpaka Ulaya, Afrika, Oceania na Latin Amrica.

Kati ya nchi zilizojiunga na Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja, nyingi zinazoteka bara la Afrika. Nchi 52 kati 53 za Afrika zilizoanzisha uhusiano wa kidiplomasia na China zimejiunga na BRI, pamoja na Umoja wa Afrika. Nchi hizo zimeshuhudia maendeleo makubwa katika sekta za ujenzi wa miundombinu, afya, nishati, kilimo na sayansi na teknolojia.

Lakini, palipo na jema, ubaya daima haukosekani. Baadhi ya nchi, hususan za Magharibi, zimekuwa na desturi ya kukosoa uhusiano kati ya China na nchi za Afrika, hususan kutokana na ushirikiano unaoongezeja kati ya pande hizo mbili chini ya mfumo wa Ukanda Mmoja, Njia Moja.

Mara nyingi, uhusiano kati ya China nan chi zaAfrika unaelezwa kwa njia isiyo sahihi, tena kwa mtazamo mbaya nan chi za Magharibi, ambazo zinaitaka Afrika kuwa makini kutokana na nia mbaya ya China kwa bara hilo.

licha ya hayo, watafiti wengi wamepinga madai hayo, huku nchi nyingi za Afrika zikiichukulia China na Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja kwa mtazamo wa tofauti. Kwa Waafrika wengi, ushiriki wa China katika bara hilo kama ulivyodhihirishwa na Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja, umeweza kutimiza mahitaji ya watu wengi wa huko, kuchangia katika kuleta maendeleo, na kusaidia kuongeza ubora wa maisha yao.

Mtafiti kutoka nchini Uganda, Frederick Golloba Mutebi anasema, China haina lengo la kuikandamiza Afrika kama vile nchi za Magharibi zinavyodai, kwa sababu China imekuwa ikitoa misaada inayotakiwa na nchi za Afrika ili kujipatia maendeleo, akitolea mifano ya miradi mikubwa ya miundombinu iliyotekelezwa na China katika nchi mbalimbali za Afrika.

Tangu kuanzishwa kwake, BRI imekuwa na umuhimu mkubwa katika maingiliano, mawasiliano, mageuzi ya kiviwanda, nishati na kuboresha miundombinu katika nchi za Afrika, mambo haya yote yamepewa umuhimu mkubwa katika Ajenda ya Umoja wa Afrika yam waka 2063. Pendekezo hilo pia limedumisha ushirikiano wa kunufaishana ambao umekuwa ukiongoza uhusiano wa kihistoria wa China na nchi za Afrika.

Chini ya mfumo wa BRI, kanda nyingi za ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara zimeanzishwa katika nchi 16 za Afrika. Hatua hii imesaidia kuleta maendeleo kwa biashara nyingi, kutoa nafasi za ajira, na kuvutia uwekezaji wa kigeni. Ndani ya mfumo wa BRI, uwekezaji wa China barani Afrika, katika maeneo ya ujenzi wa miundombinu, biashara na teknolojia ya kidijitali, unalenga kuboresha uwezo wa bara hilo wa kujiendeleza, na si kwa manufaa ya China, kama ambavyo nchi za Magharibi zinadai.

Kwa Afrika, Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja limesaidia kupatikana kwa manufaa mengi katika maeneo mbalimbali, na kuimarisha uhusiano kati ya bara hilo na China.
 
Back
Top Bottom