Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja lasaidia maendeleo ya kilimo barani Afrika

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,036
W020231115164083108609.jpg


Mwaka 2013, rais Xi Jinping wa China alitangaza Pendekezo la ‘Ukanda Mmoja, Njia Moja’ (BRI), ambalo limekuwa na manufaa kwa nchi mbalimbali zinazoendelea haswa nchi za Afrika katika sekta mbalimbali, ambapo thamani ya uwekezaji kati ya China na nchi zilizojiunga na Pendekezo hilo mpaka sasa umefikia dola za kimarekani bilioni 380,

Mpaka sasa, nchi 53 kati ya 54 za bara la Afrika zimejiunga na Pendekezo hilo, na manufaa yake yameonekana kidhahiri. Tangu kuanzishwa kwake, BRI imekuwa na ushirikiano wa kilimo na nchi na mashirika mbalimbali yaliyojiunga na Pendekezo hilo. Kwa nchi za Afrika, kilimo kinachukua nafasi kubwa katika pato la ndani la nchi za bara hilo, huku asilimia karibu 60 ya watu wakijishughulisha na kilimo. Pamoja na kuwa na rasilimali kubwa ya ardhi yenye rutuba, bado nchi za Afrika hazijafaidika na kilimo.

Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja lililotolewa na China, limekuwa mkombozi katika sekta ya kilimo kwenye nchi za Afrika, ambazo zimeshuhudia teknolojia za kisasa za kilimo na miundombinu bora ya kisasa inayowezesha wakulima kufikisha mazao yao kwa watumiaji kwa urahisi zaidi.

Tangu kuanzishwa kwake, ushirikiano wa kilimo kupitia BRI umezingatia hatua za kitaifa na kimataifa zinazolenga kuondokana na vikwazo katika ukuaji wa sekta ya kilimo, na kujenga miundombinu rahisi na migumu. Miundombinu hiyo ni pamoja na mitandao sahihi ya usafirishaji ili kupeleka bidhaa za kilimo katika masoko, kuboresha uratibu wa utafiti katika sayansi ya kilimo, na kuhuisha viwanda vya hifadhi pamoja na umwagiliaji, na pia kuwatambulisha wakulima kilimo cha kisasa na teknolojia zinazounga mkono kilimo cha kisasa, na hivyo kuboresha kilimo endelevu.

Kwa nchi zilizojiunga na Pendekezo la BRI, ushirikiano huo wa kilimo unasukuma mageuzi ya kiuchumi kwa kuimarisha uwezo wa uzalishaji na kuboresha biashara katika sekta ya kilimo, na kwa njia hiyo, kukabiliana na changamoto za dunia ikiwemo umasikini na njaa. Ushirikiano wa kilimo wa BRI unafungua fursa mpya za ukuaji katika mnyororo wa thamani wa kilimo na chakula, na kuwezesha nchi washiriki, hususan nchi zinazoendelea, zikiwemo za Afrika, kuendeleza ukuaji unaotokana na kilimo ili kutimiza malengo ya maendeleo.

Katika nchi nyingi za kipato cha chini ama cha kati ambako nguvukazi kubwa inajishughulisha na kilimo, na ambazo sekta hiyo inachukua asilimia 25 ya pato la jumla la ndani, ushirikiano wa kilimo wa BRI unaohusiana na uhamishaji wa teknolojia za kilimo, uwekezaji katika kilimo, uwekezaji katika miundombinu na kasi ya sera za uratibu, unatoa fursa ya kipekee kwa nchi hizo zinazoendelea kutimiza ukuaji endelevu unaochochewa na kilimo, kuingia katika masoko mapya na makubwa, kusaidia kutoa fursa za ajira, na kuboresha usalama wa chakula.

Tukichukulia mfano wa Burundi, ambayo ilijiunga na Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja mwaka 2018, ikianzia na ushirikiano wa kilimo. Mara baada ya kuanza ushirikiano na China chini ya Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja, ambao unazingatia zaidi ushirikiano uliopo wa kilimo kati ya nchi hizo mbili, katika miaka mitano iliyopita, Burundi imeshuhudia maendeleo makubwa katika sekta ya kilimo na ufugaji nchini humo, hususan kilimo cha mpunga, na hivyo kuboresha kidhahiri usalama wa chakula nchini humo.

Kupitia ushirikiano wa kilimo wa BRI, Burundi imepokea awamu tano za wataalamu wa kilimo kutoka China, ambao wamefanya utafiti na majaribio kadhaa, na kufanikiwa kuchagua na kutambulisha aina nane za mpunga zinazoendana na hali ya hewa na mazingira ya nchi hiyo. Kutokana na juhudi hizo, mavuno hafifu ya mpunga yaliyokuwa yakisababishwa na magonjwa ya mpunga kwa sasa yamekuwa historia.

Nchini Jamhuri ya Kongo, kilimo cha muhogo kimekuwa kikifanyika kwa miongo kadhaa, lakini hakikuwa na tija kwa wakulima, sababu ikiwa ni kukosekana na aina ya muhogo inayoendana na mazingira husika, teknolojia duni za kilimo na pia ukosefu wa viwanda vya utengenezaji wa bidhaa zinazotokana na muhogo.

Baada ya kujiunga na BRI, wataalamu wa China walitambulisha kiwanda cha uzalishaji wa unga wa muhogo katika kituo cha majaribio ya kilimo kilichoko Brazzaville, mji mkuu wa Jamhuri ya Kong, chenye uwezo wa kuzalisha tani 4,000 za unga wa ubora wa juu kwa mwaka. Ndani ya kiwanda hicho, mashine zinafanya kazi ya kusafisha, kumenya, kukata na kusaga muhogo, na kutengeneza unga wa ubora wa juu wa zao hilo.

Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi wa nchini Jamhuri ya Kongo, Paul Valentin Ngobo anasema, kwa sasa hawana tena hofu ya kuwa na muhogo mkavu mvua inaponyesha, kwani uzalishaji unafanyika katika sehemu moja. Pia amesema, bei nzuri ya manunuzi inayotolewa na kampuni hiyo pia imesaidia wakulima wa huko kuongeza kipato chao.

Kwa mifano ya nchi hizo mbili, tunaweza kuona jinsi China imekuwa mstari wa mbele katika kuzisaidia nchi nyingine zinazoendelea, zikiwemo za Afrika, kuboresha sekta ya kilimo, na hivyo kuongeza kipato kwa wakulima na kwa taifa kwa ujumla. Na China imefanya hivyo kupitia njia mbalimbali, ikiwemo kutoa mafunzo kwa wataalamu wa kilimo katika nchi husika, kuhamisha teknolojia za kisasa za kilimo, na utafiti.
 
Back
Top Bottom