Pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia moja” limesaidia kuchochea maendeleo ya Afrika katika mwaka 2023

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,036
1703037801327.png


1703037811767.png


Mwaka 2023 ulikuwa na matukio kadhaa makubwa kwa bara la Afrika, ambayo yaliangazia njia za kuhimiza maendeleo ya nchi moja moja ya Afrika, na hata maendeleo ya bara zima la Afrika. Katika matukio hayo muhimu China ilitajwa mara kadhaa, na pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia moja” lilionekana kuwa moja ya hatua muhimu zenye kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa nchi za Afrika.



Kwenye mkutano wa kundi la BRICS, pamoja na mkutano wa majadiliano kati ya viongozi wa China na nchi za Afrika, iliyofanyika Agosti 2023 nchini Afrika Kusini, na mkutano wa maadhimisho ya miaka 10 ya pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia moja”, ajenda ya maendeleo barani Afrika, na China ikiwa moja ya sehemu muhimu ya ajenda hiyo, ilikuwa na nafasi muhimu kwenye mikutano hiyo.



Kwa muda mrefu sasa hali ya kuwa nyuma kwa maendeleo ya bara la Afrika imekuwa ikitajawa mara kwa mara, lakini udhati wa wadau wa kimataifa katika kubadilisha hali hiyo umekuwa ukitofautiana. Tukiangalia mfano mmoja tunaweza kuona kuwa baadhi ya nchi za magharibi zimekuwa hodari katika kueleza changamoto zinazozikabili nchi za Afrika, bila kutoa msukumo unaohitajika katika kuondoa changamoto hizo. Na hata zikitoa msukumo fulani, huwa unalenga kwenye maswala yanayohimiza ajenda zao, na sio kulenga kusaidia Afrika na waafrika moja kwa moja.



China kwa upande mwingine, kwa kutambua changamoto za kimsingi za Afrika na kwa kujadiliana na nchi za Afrika, inatumia njia mbalimbali za kushughulikia na kutatua changamoto za msingi zinazolikabili bara la Afrika. Changamoto kubwa za Afrika ni kutokuwa na muundo mzuri wa biashara, yaani bado inaendelea kuuza zaidi malighafi na kununua zaidi bidhaa za viwandani, na changamoto nyingine ni nchi za Afrika kutokuwa na kiwango kikubwa cha biashara ya ndani ya nchi za Afrika zenyewe. Kutokana na hali hiyo, Rais Xi Jinping wa China aliahidi kuanzisha “ushirikiano wa aina mpya wa kimkakati kati ya China na Afrika”, lengo likiwa ni kuondoa mzizi wa tatizo hilo.



Kutokana na usugu wa changamoto za maendeleo ya uchumi barani Afrika, ilikuwa vigumu kufikiri ni vipi China inaweza kusaidia kuondoa changamoto hizo. Waingereza wanasema “seeing is believing”, na sasa kuna mengi yanayoonekana, yanayoweza kutajwa kuwa ni utekelezaji wa ahadi ya China kwa nchi za Afrika. Kwenye kubadilisha muundo wa biashara kati ya China na Afrika, tumeweza kushuhudia kuwa kupitia programu mbalimbali uagizaji wa bidhaa kutoka nchi za Afrika kuingia China umekuwa unaongezeka, na idadi ya watalii wa China wanaotembelea nchi za Afrika imekuwa ikiongezeka, na kusaidia hata kurekebisha hatua kwa hatua changamoto ya urari wa biashara.



Pengine la muhimu zaidi ambalo China kupitia pendekezo la “Ukanda mmoja, Njia moja” imeweza kushirikiana na nchi za Afrika kutatua changamoto ya muda mrefu ya mawasiliano ya barabara kati ya nchi za Afrika. Kumekuwa na msukumo mkubwa wa kuwekeza kwenye sekta ya viwanda, ambapo hadi kufikia mwaka 2023 kutakuwa na bustani za viwanda zaidi ya 60 katika nchi mbalimbali za Afrika. Na uwekezaji huo sio tu unahimiza matumizi ya malighafi za nchi wenyeji, bali pia unahimiza usafirishaji nje wa bidhaa zilizokamilika.



Kwa upande wa miundo mbinu kuna reli nyingi ambazo zimejengwa na kampuni za China zikiunganisha miji mbalimbali au hata nchi tofauti. Mfano mzuri ni reli ya SGR ya Kenya ambayo baada ya kukamilika itafika hadi Uganda, na reli inayoendelea kujengwa Tanzania baada ya kukamilika itaunganisha bandari ya Dar es salaam na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Rwanda, Burundi na hata Uganda. Hii ni mbali na barabara na viwanja vya ndege vilivyojengwa na makampuni ya China katika nchi mbalimbali za Afrika.
 
Back
Top Bottom