Viganja Mashavuni Mwangu

Viganja Mashavuni Mwangu

Sehemu ya 121

Yeye na mumewe, Cassian walikuwa na mtoto mwingine, Esta ambaye kipindi hicho alikuwa chuo kikuu lakini bado tu hawakuonekana kufurahia kabisa, walikuwa wakimuomba Mungu ili kila kitu walichokuwa wakipitia watoto wao hao yaishe ili waishi maisha ya amani na furaha kama ilivyokuwa zamani.
Machozi hayakuacha kutiririka mashavuni mwake, kila siku viganja vyake vilikuwa mashavuni akifuta machozi yaliyokuwa yakitiririka kila alipokuwa akiwaangalia watoto wake waliokuwa kwenye matatizo makubwa.
Walker hakuacha kulia, mpenzi wake aliyafumbua macho yake lakini hakuwa na furaha hata kidogo, alisahauliwa, msichana huyo hakukumbuka kitu chochote kile na kila alipokuwa akiwaangalia, alibaki akishangaa.
Hawakuacha kufika hospitalini hapo, Patricia aliendelea kuwa kitandani na hata pale alipopata nafuu, alichukuliwa na kuwekwa kwenye kiti cha walemavu kwani hakuwa na uwezo wa kufanya kitu chochote kile katika kiti kile alichokuwepo.
Walker na Walter ndiyo waliokuwa na kazi ya kumpeleka huku na kule, walihuzunika, wakati mwingine walikuwa wakilia, kwa Walker, alitumia nafasi hiyo kuzungumza naye maneno mengi na hata kumkumbusha yaliyopita lakini msichana huyo hakuwa akikumbuka kitu chochote kile.
“Mimi nilikuwa nasoma?” aliuliza Patricia huku akishangaa.
“Ndiyo! Ulikuwa nchini Ufaransa ukiishi na wazazi wako. Unakumbuka?’ aliuliza Walker huku akimwangalia msichana huyo.
“Hapana! Sikuwahi kuishi Ufaransa hata siku moja.”
“Unamkumbuka Annie?”
“Ndiye nani?”
“Rafiki yako chuoni!”
“Kwani mimi nimewahi kusoma?”
“Ndiyo! Tena ulikuwa na akili sana darasani,” alisema Walker.
Hakukumbuka kitu chochote kile, kila kitu alichokuwa akiambiwa kilionekana kuwa kipya katika maisha yake. Walker na mwenzake walijaribu kumkumbusha kila kitu kilichotokea lakini hakukumbuka kabisa.
Wazazi wake nao walikuwa wakilia tu, waliumia, hawakuamini kama binti yao angepitia maisha kama aliyokuwa akipitia. Ubongo ulicheza na uti wa mgongo kuvunjika, yalikuwa ni matatizo makubwa yaliyowafanya kulia kila siku.
 
Sehemu ya 122

Siku zikaendelea kukatika, baada ya miezi tisa, Walker na Walter wakaanza kujisikia hali ya tofauti vichwani mwao. Walikuwa wakipata maumivu makali ya kichwa kiasi kwamba wakati mwingine walihisi kama walibeba vitu vizito na kupoteza fahamu.
Lilikuwa tatizo kubwa lililowatesa kupita kawaida, Naseku na mumewe walishangaa, watoto wao hawakuwahi kupata tatizo kaka hilo, hawakujua kilichokuwa kimetokea hivyo kuwachukua na kuwapeleka hospitalini.
“Tatizo limeanza lini?” aliuliza daktari huku akiwaangalia.
“Ni ghafla sana, hatujui tatizo nini!” alijibu Cassian huku akimwangalia daktari.
Kilichofanyika ni vipimo, wakaangalia vichwani mwao, walihisi kwamba inawezekana fuvu la kichwa lilikuwa limepata majeraha hivyo kuangalia. Huko hawakugundua kitu, iliwashangaza, hakukuwa na tatizo lolote lile sasa kwa nini walikuwa wakizimia mara kwa mara.
Kilichofuata kilikuwa ni kuangalia mishipa na misuli yao pale ilipokuwa ikiwaunganisha vichwani. Hapo ndipo wakagundua kwamba walikuwa wameharibu mishipa na misuli kwa kuwa tu walikuwa wakitumia nguvu kubwa mno katika kufikiria na kulia hivyo mishipa mingi kulegea na kutanuka hali iliyoonyesha kwamba hali ingekuwa mbaya zaidi katika maisha yao kama hali hiyo ingeendelea.
“Tatizo kubwa ni nini?” aliuliza Cassian, Naseku hakuzungumza chochote kile, kazi yake ilikuwa ni kulia tu.
“Misuli na mishipa yao ina tatizo hasa katika sehemu hii waliyoungana, kuna tatizo kubwa la kuvimba na kusinyaa,” alijibu daktari huku akiwaangalia wazazi hao.
Lilikuwa pigo kubwa kwao, kitendo cha kufikiria sana na kuhuzunika ndicho kilikuwa sababu kubwa ya wao kuwa katika hali hiyo. Wakalazwa hosipitalini. Kila mtu duniani akajua kile kilichotokea, watu wengi wakaanza kutuma salamu zao za pole kwa mapacha hao ambao walilazwa katika chumba maalumu huku madaktari wakiendelea kuwahudumia.
 
Sehemu ya 123

Hakukuwa na mtu aliyeruhusiwa kuingia ndani ya chumba hicho zaidi ya manesi na madaktari ambao walikuwa kwa ajili ya kuwatibu tu. Siku ziliendelea kukatika huku wakiwa humo. Tatizo lile likaanza kukua na mwisho wa siku kuanza kutoka damu katika masikio yao na madaktari walipowapima, wakaonekana kuwa na tatizo jingine kabisa, mishipa na misuli iliyokuwa imevimba ilianza kuchanika.
“Nini?” aliuliza daktari mmoja huku akionekana kuchanganyikiwa.
“Ndiyo hivyo! Tatizo kubwa ni kuungana kwao, haya mengi hujitokeza mara chache sana, ni wawili kati ya watu elfu kumi. Chanzo kikubwa kabisa ni kuungana kwao,” alisema daktari ambaye alikuwa ametoka kuwachukua vipimo.
Ilikuwa taarifa mbaya ambayo hawakujua ni kwa namna gani walitakiwa kuwaambia wazazi wao. Pale katika kichwa ambapo waliungana kulipitia mishipa mingi ya damu na misuli kiasi kwamba hata ilipokuwa imevimba, ilikuwa rahisi kuchanika kwa kuwa tu ilikuwa imebanana sana na tena ilikuwa mingi kupita kawaida.
“Watakufa! Kama kweli tatizo limefikia hapa, watakufa,” alisema daktari mmoja huku akiwaangalia wenzake, kidogo akaonekana kukata tamaa, hakukuwa na mgonjwa aliyekuwa akichanika mishipa na misuli halafu akapona.
**** Edmund aliendelea kukaa kwenye mti mpaka asubuhi. Mwili wake ulichoka, hakulala usiku mzima, alikuwa na hofu kwa kuona kwamba angekamatwa na polisi. Akateremka na kuanza kupiga hatua kuelekea barabarani.
Siku hiyo hali ilionekana kuwa tofauti, kila alipokuwa akipita, hakukuwa na watu wengi kama ilivyokuwa siku nyingine hasa katika nchi hizo zilizokuwa zikitawaliwa na Malkia Elizabeth.
Alitembea kwa mwendo wa taratibu, uso wake ulikuwa chini, mawazo mengi yalimtawala na hakutaka kabisa kugundulika alionekana kuwa mnyonge kupita kawaida, alijuta, hakujua kama kuna siku angekuja kuishi katika maisha aliyokuwa akiishi kipindi hicho.
Alitembea mpaka alipofika katika kituo cha daladala ambapo hapo akatulia. Akaanza kuyafikiria maisha yake yaliyopita, japokuwa yalikuwa kwa kipindi kifupi sana hasa baada ya kutaka kuwaua mapacha walioungana lakini aliona kama ulikuwa mwaka mzima kwa jinsi alivyokuwa.
 
Sehemu ya 124

Wakati akiwa hapo, watoto wanne wakaletwa mahali hapo huku wakiwa wamevaa sare za shule na kusubiri hapo huku wakiwa na wanawake watu wazima wawili. Walimsalimia lakini mawazo ya Edmund hayakuwa hapo kabisa, alikuwa akifikiria mbali, maisha yake yalimchanganya kupita kawaida.
Hawakutaka kushughulika naye, wakasubiri gari la shule ambalo lilifika hapo baada ya dakika kadhaa na kuwaingiza watoto wale na kuondoka. Edmund hakusimama, bado kichwa chake kilikuwa kimechanganyikiwa, hakujua ni kitu gani alitakiwa kufanya, alikuwa na njaa, mwili ulichoka na hakujua ni kwa jinsi gani angeweza kula.
Wakati akiwa amekaa mahali hapo, kwa mbali akaliona lile gari la wanafunzi likaanza kurudi mahali hapo. Hakuliona, kichwa chake kilikuwa mbali kabisa, gari lile likasimama karibu naye, polisi wawili waliokuwa na bunduki mikononi mwao wakateremka na kumuweka chini ya ulinzi kwa kutaka aweke mikono yake kichwani.
Hakufanya hivyo, alikuwa akibubujikwa na machozi mfululizo na muda wote alihisi kama alikuwa akienda kufa kwa jinsi maisha aliyokuwa amepitia yalivyomchanganya.
Alibaki akiwa kama mtu aliyeganda, hakutingishika, kichwa alikiinamisha kidogo na hakuonekana kujua kitu chochote kilichokuwa kikiendelea. Kama kuzunguka huku na kule, alifanya hivyo kwa kipindi kirefu sana, akachoka, ilikuwa ni bora kukamatwa na polisi akapumzike lakini si kuendelea kuzurura kama alivyokuwa akifanya.
 
Sehemu ya 125 “Hands on your head,” (mikono kichwani mwako) alisema polisi mmoja huku akiwa amemnyooshea bastola lakini Edmund hakufanya hivyo.
Wakamsogelea na kumfunga pingu, hakufanya kitu chochote zaidi ya kulia, moyo wake ulibadilika na kuumia mno, hakuyapenda maisha yake, aliyachukia na kitu pekee alichokuwa akikihitaji kilikuwa ni kupumzika tu.
Kitendo cha kukamatwa, watu wakaanza kujaa na kutaka kujua kilichokuwa kimeendelea, dereva wa gari lile la wanafunzi ambaye ndiye aliyetoa taarifa kwa polisi hao baada ya kumuona katika kituo hicho akaambiwa kwamba gari hilo lilihitajika kumpeleka Edmund mpaka kituoni jambo ambalo halikushindikana kabisa.
Akachukuliwa, akapakizwa ndani ya gari huku akilia. Hakuzungumza kitu chochote kile, alikuwa kimya, watu waliogundua kwamba yule alikuwa Edmund, wakapigiana simu na kuwaambia wenzao kwamba hatimaye Edmund alikuwa amekamatwa, ili kuonyesha ushahidi, mpaka picha wakawatumia.
“Una uhakika ni yeye?” aliuliza jamaa mmoja kwenye simu.
“Ngoja nikutumie picha uone!”
.

.
.

Je, nini kitaendelea?
 
SEHEMU YA 64

Hapo, kulikuwa na waimbaji wengi lakini kitu cha ajabu kabisa kila mmoja alikuwa akimshangaa Walter, alikuwa akiimba kiasi kwamba wengine wakampa jina la malaika, waliamini kwamba sauti yake ilikuwa nzuri hata ya hao malaika waliokuwa na kazi kubwa ya kumsifu na kumwabudu Mungu.
Kwa Walker kila mtu alikuwa akishangaa, alikuwa mchoraji mkubwa, alijua kuchora picha za kila aina, kila mtu aliyekuwa akiziangalia picha zake alikuwa akipigwa na butwaa, alikuwa hatari katika uchoraji wake.
Waliishi nchini Marekani, wazazi wao walikuwa wakienda kuwaangalia mara kwa mara. Na baada ya miezi kadhaa baba yao akawaambia kwamba mama yao alijifungua salama mtoto wa kike na kuamua kumpa jina la Ester.
“Is this the one?” (ndiye huyu?) aliuliza Walter huku akiangalia picha ya Ester.
“Yes! She is!” (Ndiyo! Ndiye yeye)
“We look alike,” (tumefanana sana) alisema Walker huku naye akiiangalia picha hiyo.
Miaka saba baadaye, walikuwa watu maarufu kuliko wote nchini Marekani. Majina yao yaliongoza kutafutwa katika tovuti ya Google kitu kilichomaanisha kwamba kwenye kila kona watu walikuwa wakitaka kufahamu mambo mengi kuhusu hao.
Katika kipindi hicho ndipo wakakumbuka kitu. Kipindi walichokuwa wadogo kulikuwa na wasichana wawili waliokuwa marafiki zao sana nchini Tanzania, wasichana hao walikuwa Catherine na Jackline.
Hawakujua mahali walipokuwa, waliondoka nchini Tanzania zamani sana na hawakujua kama wasichana hao walikuwa hai au walikufa.
Walichokikumbuka ni kwamba mmoja alikuwa mtoto wa balozi wa Uingereza nchini Tanzania na mwingine mtoto wa balozi wa Marekani nchini Tanzania hivyo kuanza kuwatafuta katika mitandao ya kijamii.
“I’ve got her,” (nimempata) alisema Walker huku akiiangalia kompyuta yake, alikuwa amempata rafiki yake wa utotoni, Rosemary.
“How about Jackline? Did you find her?” (vipi kuhusu Jackline? Umempata?) aliuliza Walter huku akiwa na hamu ya kujua mahali alipokuwa msichana huyo.
“Give me one sec,” (nipe sekunde moja)
Mamaa kumbe nawe umo shogaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sehemu ya 126

Hakukuwa na kitu kilichobadilika, Walter na Walker waliendelea kuwa katika hali ileile, walikuwa kitandani huku wakiwa kwenye hali mbaya. Madaktari walikuwa wakihangaika kuhakikisha wanarudi katika hali zao za kawaida lakini hilo lilishindikana kabisa.

Damu zilizidi kuwatoka, mishipa ilipasuka hali iliyowafanya kuwa katika hali mbaya zaidi. Wazazi wao walikuwa wakilia, hawakuwa wakiamini kama mwisho wa kila kitu ungekuwa namna hiyo.

Vyombo vya habari viliendelea kutangaza kwamba watu hao walikuwa na dalili ndogo sana za kupona na kurudi katika hali kama zamani kwani hakukuwa na mtu ambaye mishipa yake ilipasuka halafu akapona.

Kipindi hicho ni kama dunia ilikuwa kimya, ilikuwa ikiomboleza kwa kile kilichokuwa kikiendelea. Kwenye mitandao ya kijamii, magazetini na hata mitaani watu walikuwa wakiwazungumzia wawili hao na jinsi walivyokuwa na nafasi ndogo ya kuweza kupona na kurudi katika hali zao kama walivyokuwa zamani.

“Wanakufa!” alisema mwanaume mmoja alipokuwa akiziangalia picha za mapacha hao waliokuwa hawajitambui katika kitanda kikubwa walicholalia.

“Ila nina uhakika Mungu atawaponya!” alisema mwanamke aliyekuwa pembeni yake, macho yake yalikuwa mekundu, japokuwa hawakuwa ndugu zake lakini alishindwa kujizuia, alikuwa amelia sana kwa ajili ya watu hao.

Watu wakaendelea kujazana hospitalini walipokuwa, kila mmoja alitaka kujua kile kilichokuwa kikiendelea. Wengi waliokuwa mahali hapo walionekana kukata tamaa, walijua kabisa kwamba baada ya saa chache zijazo wawili hao wangefariki dunia na kwenda kuanza maisha mapya baada ya kifo.

Naseku alilia sana, aliishiwa nguvu na kupoteza fahamu zaidi ya mara tatu, alikuwa na uchungu mno, moyo wake ulimuuma na kila alipokuwa akiwaangalia watoto wake, alisikia kitu chenye ncha kali kikiuchoma moyo wake.

Aliomboleza, mtu pekee aliyekuwa akimfariji kwa kipindi hicho alikuwa mume wake, Cassian. Kila alipokuwa akibembezwa, hakubembelezeka kwani alijua kabisa kwamba huo ndiyo ungekuwa mwisho wa kila kitu, watoto wake wangekufa palepale hospitalini walipokuwa.
 
Back
Top Bottom