Viganja Mashavuni Mwangu

Viganja Mashavuni Mwangu

Sehemu ya 127

Madaktari hawakuacha kuhangaika, walifanya kila liwezekanalo kuokoa maisha ya mapacha hao.

Kila mtu aliwatumainia, wao ndiyo ulikuwa msaada wa mwisho waliokuwanao kipindi hicho, yaani wao ndiyo waliokuwa wameshililia uhai wa mapacha hao, wao ndyo wangeamua kama watu hao walitakiwa kufa au kuendelea kuishi.

Hawakuwa na mategemeo yoyote ya mapacha hao kupona, damu zilizokuwa zikiwatoka baada ya mishipa kuchanika ziliendelea kusambaa miilini mwao na hivyo kuwafanya kuwa kwenye hali mbaya zaidi.

Ilipofika tarehe 2/09/2016 majira ya saa 2:36 usiku ndiyo muda ambao Walter na Walker wakafariki dunia katika kitanda walichokuwepo.

Hiyo ilikuwa habari ya mshtuko, madaktari ambao walilitambua hilo wakaishiwa nguvu, hawakujua ni kwa namna gani wangeweza kuwaambia wazazi wao juu ya kile kilichokuwa kimetokea kwani kwa kipindi chote ambacho watoto hao walikuwa mahututi nyuso zao zilionekana kuwa kwenye maumivu makali, ingekuwaje kama wangewaambia kuwa walifariki dunia?

“Tutaitoaje miili hii na wakati wazazi wao wapo hapo nje?” aliuliza daktari mmoja.

“Labda tukawatoe!”
“Tukawatoe? Tutaanzaje?”
“Subiri! Nakwenda kuwachukua na kuwaambia twende kwa daktari kuongea nao. Wakati nimetoka nao, nyie watoeni haraka sana muwapeleke katika chumba maalumu kwanza,” alisema daktari mwingine.

“Sawa.”
Wakakubaliana, hakukuwa na muda wa kupoteza, hapohapo daktari yule akatoka, akaanza kuzungumza nao na kuwaambia kwamba walitakiwa kuzungumza nao katika ofisi yake hivyo awafuate. “Wanaendeleaje?’ aliuliza Naseku huku akimwangalia daktari.

“Wanaendelea salama! Twendeni,” alisema daktari.
Wakasimama na kuanza kuondoka, walipiga hatua fupifupi huku kila mmoja akiwa na mawazo tele.

Daktari alikuwa akiwaza ni kwa namna gani angeweza kuwaambia wazazi hao kile kilichokuwa kikiendelea kwani kwa jinsi walivyokuwa wakionekana, hawakuwa radhi kupokea taarifa kwamba watoto wao walikuwa wamefariki dunia.

Wakaondoka katika korido ile, haraka sana madaktari wale waliokuwa wamebaki ndani ya chumba kile walipoona wameondoka, wakaanza kuitoa miili ile iliyokuwa kitandani na kuipeleka katika chumba kingine.
 
Sehemu ya 128

Wakati Naseku na mumewe akipiga hatua, akajipekua, hakuwa na simu, alikuwa ameisahau pale alipokuwa amekaa kwani aliondoka kwa kushtukiza sana.

Hakutaka kuendelea na safari ya kuelekea huko, akamwambia mumewe kwamba alisahau simu na hivyo kuirudia.

Alipofika katika korido ile, macho yake yakatua katika kitanda kikubwa kilichokuwa kikitolewa katika chumba kilekile walichokuwa watoto wake huku kikiwa kimefunikwa na shuka kubwa la kijani.

Moyo wa Naseku ukapiga paaa! Hakuamini alichokuwa akikiona, madaktari walipomuona, wakashikwa na hofu na kujua kwamba ile siri waliyokuwa wameitunza ilibumburuka.

Haraka sana Naseku akaanza kupiga hatua za harakaharaka kuelekea kule wapokuwa wale madaktari, tayari akili yake ilimwambia kwamba wale walikuwa watoto wake, na kama walikuwa wamefunikwa shuka la kijani ilimaanisha kwamba walifariki dunia.

Hata kabla hajafika, madaktari wakamzuia, hakutakiwa kuangalia kile kilichokuwa kimefunikwa, hapo ndipo akaanza kulia.

Alilia kama mtoto, alipiga kelele kiasi kwamba watu wengine wakafika kuona nini kilikuwa kikiendelea. Alilia kwa ajili ya watoto wake, alilia kwa kuwa walikuwa watu muhimu sana katika maisha yake.

“Walter...Walker...kwa nini mmekufa? Kwa nini mmetuacha...mbona hamkusema kama mtakufa...nitaishi vipi mimi....nitaishi vipi bila nyie wananngu?” alilia Naseku kama mtoto huku madaktari wakiwa wamemzuia pande zote, hakuchukua muda mrefu, akaanguka kama mzigo, akapoteza fahamu na hakujua ni kitu gani kiliendelea baada ya hapo.
***

Hali haikuweza kubadilika kwa Patricia, aliendelea kuwa vilevile kama alivyokuwa. Hakuweza kukumbuka kitu chochote kile, kila alipokuwa akitembelewa na watu alikuwa akiwashangaa, hakujua walikuwa wakina nani na wakati mwingine alijiuliza sababu ya kuwa hospitalini hapo lakini akakosa jibu.

Wazazi wake waliendelea kuhuzunika, hakukuwa na kipindi kigumu walichokuwa wakipitia kama kipindi hicho.

Hakukuwa na kilichobadilika, mbaya zaidi wakati wakiendelea kumsubiri binti yao arudiwe katika hali ya kawaida, wakasikia kwamba Walter na Walker walikuwa wamefariki dunia.
 
Sehemu ya 129

Ilikuwa ni habari mbaya, ilikuwa ni zaidi ya kuchomwa na msumali wa moto mioyoni mwao, hawakuamini kile kilichokuwa kimetokea kwani mbali na pacha mmoja kutoka kimapenzi na binti yao, walikuwa wakiwapenda kupita kawaia.

Dunia ikashtuka, hakukuwa na aliyeamini kwamba mapacha hao walikuwa wamefariki dunia, kila mtu alikuwa akilia, wengi wakaelekea hospitalini hapo na kuweka mashada ya maua na picha mbalimbali katika eneo ambalo waliruhusiwa kufanya hivyo.

Hakukuwa na mtu aliyeamini kama wasingeweza kuwaona watu hao tena, vile vipaji vya kipekee walivyokuwanavyo wasingeweza kuviona au kusikia tena.

Watu maarufu wakatuma salamu za rambirambi katika mitandao ya kijamii na wengine kwenda huko na kuwatia moyo wazazi wao waliokuwa watu wa kulia kila wakati, tena mpaka muda huo, Naseku alikuwa amepoteza fahamu zaidi ya mara nne, yote ilikuwa ni kwa sababu ya kuumizwa na msiba mzito aliokuwa ameupata.

Baada ya siku mbili, mapacha hao wakapelekwa katika Kanisa la St. John lililokuwa haohapo New York na kuagwa sura ya mwisho kabla ya kupelekwa nchini Tanzania tayari kwa maziko.

“Hivi ni kweli wamekufa?” aliuliza mwanamke mmoja, macho yake yalikuwa yamevimba huku mashavu yakiwa yamelowanishwa kwa machozi.

“Yaani siamini! Kweli mapacha hawa wamekufa?” aliuliza mwanamke mwingine, naye hakuwa ameamini kile kilichokuwa kimetokea.

Siku iliyofuatwa taratibu za kuwasafirisha mapacha hao zikafanyika na hivyo kupelekwa nchini Tanzania. Ndani ya ndege ilikuwa ni huzuni tele, kila wakati Naseku alipokuwa akiliona jeneza la watoto wake alikuwa akilia kwa uchungu, hakuwa akiamini kwamba mwisho wa kila kitu ungekuwa namna ile.

Zaidi ya watu elfu kumi na tano walikuwa wamekusanyika katika Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere kwa ajili ya kuipokea miili hiyo.

Watu wengi waliokuwa mahali hapo walikuwa na fulana zilizokuwa na picha za mapacha hao huku wengine wakiwa na maua kama njia mojawapo ya kuomboleza kwa kile kilichotokea.
 
Sehemu ya 130

Ndege ilipotua, watu wakateremka, jeneza likashushwa, watu wakaanza kulia kwa sauti, kila mmoja alitaka kuligusa jeneza hilo ambalo lilipakizwa na kuanza kupelekwa katika uwanja wa taifa ambapo huko watu walitakiwa kuaga na kisha kuelekea kanisani, kufanyiwa ibada na kwenda kuzikwa katika makaburi ya Kinondoni.

Kila kitu kilichotakiwa kufanywa, kilifanywa na ilipofika majira ya saa kumi jioni, tayari msafara ukaanza kuelekea katika makaburi hayo na hivyo mapacha hao kuzikwa huko.

Ilikuwa ni huzuni, mapacha waliokuwa wameipatia Tanzania umaarufu walifariki, kila mmoja alihuzunika, japokuwa walikuwa wameondoka lakini kwenye akaunti yao waliacha utajiri mkubwa ambao wazazi wao wakaamua kutumia asilimia kumi ya utajiri huo kwa ajili ya kuwasaidia watoto waliokuwa kwenye matatizo mbalimbali.

Kwa msichana Patricia, aliendelea kuwa kwenye hali hiyohiyo kwa muda wa miaka mitano. Alikuwa akitibiwa kwa nguvu zote, pingili za mgongo wake ambazo ziliachia zikaanza kurudi na miaka miwili mbele, akafanikiwa kusimama na kuanza kutembea ila kumbukumbu zake hazikuweza kurudi tena.

Ubongo wake ulikuwa kama umeathiriwa, hakujua kilichotokea, hakujua kama aliwahi kuwa na mwanaume aliyekuwa akimpenda kwa moyo wake wote. Wazazi walijitahidi kumpeleka katika hospitali mbalimbali lakini kote huko waliambiwa kwamba binti yao asingeweza kukumbuka kitu chochote mpaka kifo chake.

Maisha yake yakaanza upya, akaanza kutengeneza urafiki na watu wengine, hata alipokuwa akiziona picha za Walter na Walker hakuwa akikumbuka kitu chochote kile, kwake, watu hao walionekana kuwa wageni kabisa ambao aliwaona mara kadhaa walipokuwa wakimfuata hospitalini kumuona.

Naseku hakuwa na furaha, alikuwa mtu wa huzuni, kila alipokuwa akiziona picha za watoto wake, alikuwa akilia, machozi yalitiririka mashavuni mwake na kuyafuta kwa kutumia viganja vyake.

Hakikubadilika kitu, kwa mtoto mmoja waliyekuwa naye, Esta, wakaendelea kumlea na baada ya miaka minne, akaolewa na kufanikiwa kujifungua watoto mapacha wa kiume ambao kwa kuwaenzi ndugu zake, akaamua kuwaita Walter na Walker.

MWISHO.
 
[emoji120] [emoji120] [emoji120]
 
Back
Top Bottom