Faida za kufanya maombi

Faida za kufanya maombi

Mwl Mwakujonga

JF-Expert Member
Joined
Jun 29, 2023
Posts
356
Reaction score
707
Tukiwa katika mazungumzo na rafiki yangu juu ya umuhimu wa kufanya maombi ya mara kwa mara hata kama hakuna tatizo, kwa sababu shetani yuko kazini kila siku kuwatafuta watu haweze kuwadhuru.

Rafiki yangu anaeleza siku moja wakati yuko kazini mmoja wa watoto wake ambao anawafundisha alikuwa anamwomba kumwombea, kwani alikuwa ajisikii vizuri, kwa kuwa alikuwa anakazi nyingi alimwambia yeye na mwenzake wanatakiwa kuwa wanafanya mambi wenyewe kwa sababu yeye hayuko pamoja nao siku zote wanatakiwa kujitegemea kwa maombi.

Maneno hayo alitoa kama hutani kwa sababu alikuwa anashughuli nyingi , anasema siku hiyo alikuwa anakwenda msibani na alipokuwa msimbani alijiskia moyoni mwake kuna udhuni kubwa ndani yake kiasi kwamba hakawa anajiskia vibaya, alijaribu kumwomba Mungu kwa ajili ya hali ile imwache ili akimaliza shughuli za mazishi aweze kuomba lakini hali hile haikumwacha hadi jioni.

akiwa amerudi nyumbani akapigiwa simu yule rafiki yake amegongwa na gari na kufariki , anasema alihisi moyo kufa ganzi alikuwa na maomivu yasiyo koma, anasema siku ile haikuwa nzuri kwake kwani alijiona ana hatia ya damu ya mtu.

binafsi nilijiskia hudhuni lakini nikawaza mambo yafuatayo:-

Yule mtoto alikuwa na wazazi wake, je wazazi wake walikuwa wanaomba kwa ajili ya mwanao? kama walikuwa hawaombi kwanini hawakumwombea mtoto wao? ile kwamba mtoto amerudi nyumbani salama leo sio guarantee kesho atakuwa salama.

Mzazi/Mlezi Muombee mtoto wako , kila siku ya Mungu haujui kesho yake itakuwaje, Musa akasema huso wako husipotuchukua kutoka hapa hatutoki mahali hapa, Musa alijua kutembea bila huwepo wa Mungu ni hatari kwa maisha yake ndio maana hakukubali kuondoka mbele za Bwana hadi walipotengeneza

hakikisha kila siku unasema neno kwa ajili ya Mtoto wako hata kama ni maneno Mawili tu, sema kwa ajili yake

Baba katika Jina la Yesu Kristo na Mweka Wakfu mtoto wangu huyu siku ya leo umlinde na Kumtunza aingiapo na kutokapo katika jina la Yesu Kristo, utashindwa na aya maombi?​
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom