Viganja Mashavuni Mwangu

Viganja Mashavuni Mwangu

[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] hatimae umekuja
Angalia mbaya wako asije kurudisha lokapu tena
Atajua mwenyewe nishazoea ban zake
 
SEHEMU YA 60

Watoto wao ndiyo walikuwa furaha yao, kila walipokuwa wakiwaangalia, mioyo yao ilijisikia faraja na kuona kwamba Mungu aliwabariki kwa kuwapa watoto hao waliokuwa na sura nzuri kupita kawaida.
Kila siku ilikuwa ni lazima kwa Naseku kuwapeleka watoto wake shuleni kwa gari lake, hakutaka kumwamini mtu na kitendo hicho kilionekana kuwa sahihi kwa kuwa kilimfanya kuwa karibu na watoto wake.
Walter na Walker waliendelea kukua, walikuwa watoto wenye furaha tele kiasi kwamba mpaka watu wengine walikuwa wakishangaa kwani walijua kwamba wangekuwa kwenye huzuni tele kutokana na hali ya kuungana lakini ndiyo kwanza kila siku walikuwa watoto wa kucheka tu.

Siku zikaendelea kukatika, watoto Catherine na Jackline waliendelea kuwa pamoja nayo, kwenye kila hatua waliyokuwa wakikua, walikuwa pamoja huku ukaribu wao ukiongezeka kila siku.

Baada ya miaka minne, wakaanza kusoma darasa la kwanza katika shule hiyohiyo. Ilikuwa ni furaha kwao, walisoma kwa bidii, walipendwa kila kona, kwa darasani, hawakuwa na akili nyingi lakini kila siku walionekana kupenda sana kusoma.

Watu waliwapenda kwa kuwa walikuwa na sura nzuri. Katika kipindi hichohicho cha darasa la kwanza ndipo walimu wakagundua kwamba mapacha hao walikuwa na vipaji vikubwa mno.

Walter alikuwa na uwezo mkubwa wa kuimba, kila alipokuwa akiambiwa aimbe wimbo wowote ule, sauti yake iliwashangaza watu wengine, wakabaki wakishangaa, hawakuamini kama duniani kulikuwa na mtoto aliyekuwa na sauti kali ya kuimba kama ilivyokuwa kwa Walter.
Kwa Walker, hakuwa muimbaji, yeye alikuwa na uwezo wa kuchora.

Tangu alipokuwa chekechea, hakukuwa na kitu alichokipenda kama kuchora, alijua kuchora sana zaidi ya watoto wengine.

Vipaji vyao havikujificha, kwa kuwa vilikuwa vimeonekana, walichokifanya Cassian na mkewe ni kuwaendeleza katika vipaji hivyohivyo walivyokuwa navyo. Kwa Walter, akatafutiwa mwalimu wa kwaya kwa ajili ya kumfundisha namna ya kuimba na kupangilia sauti yake.
 
SEHEMU YA 61

Uwezo wake ulikuwa mkubwa mno, kila alipokuwa, maisha yake yalikuwa ni kuimba tu.

Kanisani alikuwa gumzo, japokuwa alikuwa na miaka saba lakini kila mmoja alipenda kusikia namna alivyokuwa akiimba, aliwafurahisha watu wengi kiasi kwamba kanisani hapo akawa muimbaji kiongozi, kwenye kila ibada ya kusifu na kuabudu, alikuwa akichaguliwa yeye.

Wakati Walter akiwa muimbaji, Walker hakuwa na uwezo wowote wa kuimba, yeye alikuwa mchoraji, alikuwa na uwezo mkubwa wa kuchora kiasi kwamba mpaka watu wengine walikuwa wakishangaa.

Walter alikuwa mzungumzaji, alipenda sana kuongea, alikuwa na uwezo wa kuongea maneno mengi kwa wakati mmoja lakini Walker alikuwa mkimya, hakuwa mzungumzaji, mpole ambaye muda wote alionekana kuwa siriazi kupita kawaida.

“Who do you want to be?” (unataka kuwa nani?) aliuliza Cassian huku akiwaangalia watoto wake.

“A Pop star like Michael Jackson,” (niwe staa wa Pop kama Michael Jackson) alijibu Walter harakaharaka.
“What about you?” (vipi kuhusu wewe?) aliuliza Cassian huku akimwangalia Walker.

“I want to be a greatest picture artist ever in the world,” (nataka kuwa mchoraji bora kuliko wote waliowahi kutokea katika dunia hii) alisema Walker huku akimwangalia baba yake.

Waliishi katika ndoto, kila siku ilikuwa ni lazima kufanya mazoezi kwa kile walichokuwa wakitaka kuwa. Bado vipaji walivyokuwa navyo viliwashangaza watu wengi, hawakuamini kama kungekuwa na watoto waliokuwa na uwezo mkubwa kwa vile walivyokuwa nacho kama wao.

Kwenye mashindano mbalimbali shuleni, walipewa zawadi nyingi, waandishi wa habari waliposikia kuhusu wao, wakaanza kuwatafuta kwa lengo la kuzungumza nao na kuandika mengi kuhusu watoto hao.

Kuwapata halikuwa jambo jepesi, kila walipokwenda shuleni hapo, walikataliwa kuonana nao kwani ulinzi wao ulikuwa mkubwa kutokanma na heshima kubwa aliyokuwanayo baba yao.

Waandishi hao hawakukoma, kila kona walipokuwa waliendelea kusikia sifa za watoto hao, walikuwa wakiwashangaza kila mtu aliyekuwa akisikia kuhusu wao, juu ya vipaji vikubwa walivyokuwa navyo.
 
SEHEMU YA 62

Kwa mwaka mzima walikuwa wakiwatafuta lakini hawakuweza kuwaona.

Walipofikisha umri wa miaka kumi, baba yao akawafungulia chaneli katika Mtandao wa Youtube kwa ajili ya kuionyesha dunia kwamba kulikuwa na watoto waliokuwa na vipaji vya hatari ambao walikuwa wameungana.

Kwa kutumia pesa zake, akaanza kuitangaza chaneli hiyo, watu wengi wakaiona na kuangalia vipaji vya watoto hao.

Kila mmoja aliyekuwa akiangalia alishangaa, hakuamini kama katika dunia hii kungekuwa na watoto waliokuwa na uwezo kama Walter na Walker.

Wakaanza kupata umaarufu wakiwa wadogo kabisa. Katika kila kona ya dunia walikuwa wakizungumziwa wao tu. Watu wengi wakataka kufahamu mahali walipokuwa, walitaka kujionea kwa macho yao uwezo mkubwa waliokuwa nao watoto hao.

Waandishi kutoka BBC, CNN na vituo vingine vya habari vya kimataifa vikasafiri mpaka nchini Tanzania kwa lengo la kuonana na watoto hao. Halikuwa jambo jepesa kuwapata, walikuwa watoto wa ndani tu na hata walipokuwa shuleni, ilikuwa vigumu mno kuwaona.

Waandishi hao wakatumia majina ya vituo vyao, kitu cha kwanza kabisa kilikuwa ni kumtafuta Cassian, hakuwa mwepesi kuonana na watu hasa alipokuwa ofisini kwake, waandishi hao walihangaika kwa muda wa wiki nzima ndipo wakakutana naye na kuanza kufanya naye mahojiano.

Walimwambia wazi jinsi walivyokuwa wakishangazwa na vipaji walivyokuwanavyo watoto hao, kila mtu alishangaa, haikuwa Afrika tu bali dunia nzima ilikuwa ikistaajabu kwa kile kilichokuwa kikiendelea.

Moyo wa Cassian ukajisikia faraja, watoto wake wakawa maarufu, hilo ndilo alilitaka kwa kipindi kirefu, alijua kwamba walikuwa wameungana, alijua kwamba kama wangeendelea kuishi hivyo tu ilikuwa ni lazima kukata tamaa na kujiona kwamba hakukuwa na tumaini jingine na wakati mwingine hata kumlaumu Mungu na ndiyo maana alikuwa akipambana kuhakikisha kwamba wanakuwa na furaha hata kama wanakuwa kwenye hali ya kuungana.

“Wana miaka mingapi?” aliuliza mwandishi wa BBC.
“Miaka kumi ila mwaka huu katikati watakuwa na miaka kumi na moja,” alisema Cassian.
“Na una watoto hawa tu?”
 
SEHEMU YA 63

“Ndiyo! Ila mama yao ni mjauzito. Natumaini kupata mtoto mwingine mwaka huu,” alijibu Cassian.

Alikuwa akiulizwa maswali mengi kuhusu Walker na Walter, baada ya kumalizana naye wakataka kuwaona watoto hao na kufanya nao mahojiano kitu ambacho hakikuwa na tatizo lolote lile.

Wakaondoka na kuelekea nyumbani huko, walitakiwa kuwasubiri mpaka watakaporudi kutoka shuleni.

Hilo halikuwa tatizo, walisafiri kutoka nchini Marekani, Uingereza mpaka Tanzania kwa ajili ya watoto hao tu, hivyo wakawasubiri, na baada ya saa mbili, watoto hao wakafika nyumbani na kuanza kuwahoji baadhi ya maswali huku wakiwaonyeshea jinsi vipaji vyao vilivyokuwa hatari.

Dunia ikazidi kuwatambua, waliendelea kujulikana kila kona. Wazungu hawakutaka watoto hao wakae Tanzania, walichokifanya ni kuandaa matamasha na hivyo kuwaomab wazazi hao ruhusa ya watoto hao kushiriki katika matamasha mbalimbali yaliyokuwa yakifanyika humo.

Pesa zikazidi kuongezeka katika akaunti ya Cassian, akawaongezea pesa watoto wake, nao, wakaanza kupata utajiri mkubwa, kwenye kila tamasha walilokuwa wakihudhuria, watu walikuwa wakilipia sana kwa ajili ya kuona miujiza waliyokuwa nao watoto hao.

Mbali na kupokea pesa za waandaaji wa matamasha, pia wamiliki wa YouTube wakaanza kuwalipa pesa nyingi kwani chaneli yao ilikuwa ikitazamwa na watu wengi, mpaka kufika idadi ya watu bilioni moja, idadi ambayo ilikuwa ikiwafukuzia Justin Bielber kwa video yake ya wimbo wa Sorry na Adele kwa wimbo wake wa Helo.

They have received cheque of twenty milion dollars from YouTube,” (wamepokea cheki ya dola milioni ishirini kutoka Youtube) alisema jamaa mmoja aliyekuwa akiangalia kwenye mtandao kuhusu watoto hao.

“Sure?” (kweli?)
“Yeah! Check this out,” (ndiyo! Angalia hii)
Kwa kuwa walikuwa wakiishi sana katika nchini za huko, baba yake, Cassian akaamua kuwaanzisha masomo katika shule ya St. Monica iliyokuwa Washington nchini Marekani, shule ambayo ilikuwa ikikuza sana vipaji vya watoto waliokuwa mahali hapo.
 
SEHEMU YA 64

Hapo, kulikuwa na waimbaji wengi lakini kitu cha ajabu kabisa kila mmoja alikuwa akimshangaa Walter, alikuwa akiimba kiasi kwamba wengine wakampa jina la malaika, waliamini kwamba sauti yake ilikuwa nzuri hata ya hao malaika waliokuwa na kazi kubwa ya kumsifu na kumwabudu Mungu.
Kwa Walker kila mtu alikuwa akishangaa, alikuwa mchoraji mkubwa, alijua kuchora picha za kila aina, kila mtu aliyekuwa akiziangalia picha zake alikuwa akipigwa na butwaa, alikuwa hatari katika uchoraji wake.
Waliishi nchini Marekani, wazazi wao walikuwa wakienda kuwaangalia mara kwa mara. Na baada ya miezi kadhaa baba yao akawaambia kwamba mama yao alijifungua salama mtoto wa kike na kuamua kumpa jina la Ester.
“Is this the one?” (ndiye huyu?) aliuliza Walter huku akiangalia picha ya Ester.
“Yes! She is!” (Ndiyo! Ndiye yeye)
“We look alike,” (tumefanana sana) alisema Walker huku naye akiiangalia picha hiyo.
Miaka saba baadaye, walikuwa watu maarufu kuliko wote nchini Marekani. Majina yao yaliongoza kutafutwa katika tovuti ya Google kitu kilichomaanisha kwamba kwenye kila kona watu walikuwa wakitaka kufahamu mambo mengi kuhusu hao.
Katika kipindi hicho ndipo wakakumbuka kitu. Kipindi walichokuwa wadogo kulikuwa na wasichana wawili waliokuwa marafiki zao sana nchini Tanzania, wasichana hao walikuwa Catherine na Jackline.
Hawakujua mahali walipokuwa, waliondoka nchini Tanzania zamani sana na hawakujua kama wasichana hao walikuwa hai au walikufa.
Walichokikumbuka ni kwamba mmoja alikuwa mtoto wa balozi wa Uingereza nchini Tanzania na mwingine mtoto wa balozi wa Marekani nchini Tanzania hivyo kuanza kuwatafuta katika mitandao ya kijamii.
“I’ve got her,” (nimempata) alisema Walker huku akiiangalia kompyuta yake, alikuwa amempata rafiki yake wa utotoni, Rosemary.
“How about Jackline? Did you find her?” (vipi kuhusu Jackline? Umempata?) aliuliza Walter huku akiwa na hamu ya kujua mahali alipokuwa msichana huyo.
“Give me one sec,” (nipe sekunde moja)
 
SEHEMU YA 65

Haraka sana Walker akaanza kuangalia kwenye tovuti ile, alikuwa akimtafuta msichana huyo kwa kumsaidia ndugu yake huyo. Alichukua dakika zaidi ya tano kuangalia kila kona, kila alipoona jina lililofanana na la rafiki wa ndugu yake, alikuwa akiliangalia kuona kama alikuwa yeye au la.
“I’ve found her!” (nimempata) alisema Walker huku akimwangalia ndugu yake, japokuwa alikuwa akimwambia habari nzuri, uso wake ulionyesha kuwa na shaka kupita kawaida.
“Let me see,” (acha nione) alisema Walter na kisha kuanza kuangalia, alitaka kujua sababu iliyomfanya ndugu yake kuwa katika hali hiyo.
Haraka sana akaichukua iPad aliyokuwa nayo ndugu yake na kuanza kuangalia. Kile alichokiona hakuonekana kuamini, aliliona jina la msichana huyo, picha yake lakini habari ambayo ilimshangaza ni kwamba msichana huyo alikuwa amepata ajali mbaya ya gari alipokuwa akielekea chuoni Oxford nchini Uingereza.
Walter hakuamini alichokuwa akikiangalia, akahisi kama kitu chenye ncha kali kikiwa kimeuchoma moyo wake, baada ya sekunde kadhaa, machozi yakaanza kumtiririka mashavuni mwake.
Hakutaka kukubali, hakutaka kuona rafiki yake huyo akiteseka kitandani na wakati yeye alikuwa hai. Alichokifanya ni kumwambia Walker kwamba ilikuwa ni lazima kusafiri na kuelekea nchini Uingereza kwa ajili ya kumuona msichana ambaye alihisi kumpenda kwa penzi la dhati moyoni mwake.
Wakawasiliana na wazazi wao na kuwaambia kwamba ilikuwa ni lazima kusafiri kuelekea nchini Uingereza kwa ajili ya kumuona msichana huyo aliyekuwa hoi kitandani.
“Hamuwezi kwenda peke yenu! Nisubirini!” alisema Cassian kwenye simu.
“Utachelewa baba!” alisema Walter.
“Siwezi kuchelewa, nakuja baada ya siku mbili.”
“Sawa.”
Moyo wa Walter ukakosa amani, muda mwingi alikuwa akimfikiria msichana huyo. Alimpenda kutoka moyoni mwake, alijua kwamba kilikuwa kimepita kipindi kirefu sana lakini bado moyo wake ulikuwa kwa msichana huyo aliyekuwa hajitambui kitandani.
 
SEHEMU YA 66

Aliona baba yake akichelewa kuja, alichokuwa akikihitaji ni kumuona msichana huyo tu. Baada ya siku alizoahidi baba yake kutimia, wakaondoka nchini Marekani na kwenda Uingereza ambapo huko wakapelekwa moja kwa mja mpaka katika Hospitali ya Queen Elizabeth kwa lengo la kumuona msichana huyo.
Walipofika hospitalini, umati mkubwa wa watu ulikuwa ukiwashangaa, wengine wakawasogelea kwa lengo la kupiga nao picha. Walikuwa maarufu, walipendwa na kila mmoja alitamani sana kuwa nao karibu kwani vipaji walivyokuwa navyo vilimshangaza kila mmoja.
Hawakuwa na haja ya kujitambulisha walikuwa wakina nani bali walikuwa na haja ya kuuliza mahali alipolazwa msichana huyo. Kwa kuwa ulikuwa muda wa kuona wagonjwa, walipoambiwa mahali alipokuwa, haraka sana wakaondoka na kuelekea huko.
Wakafungua mlango na kuingia ndani. Msichana Jackline alikuwa kitandani, alikuwa kimya, pembeni yake walikuwa wazazi wake, kwa jinsi walivyoonekana tu walikuwa wamekata tamaa, hawakuamini kama binti yao angeweza kuzinduka na kusimama tena.
Kila walipomwangalia, waliona kabisa huo ndiyo ungekuwa mwisho wake kitandani pale. Walter aliumia mno, alimwangalia Jackline huku akihisi akichomwa na kitu chenye ncha kali, hapohapo machozi yakaanza kumtoka. Mbali na wazazi wa Jackline waliokuwa chumbani humo, pia pembeni yao kulikuwa na kijana mwingine, huyu aliitwa Edmund, kijana aliyekuwa mpenzi wa Jackline aliyekuwa kitandani.

Je, nini kitaendelea?
 
SEHEMU YA 67

Walikuwa na umri mdogo lakini walionekana kuwa na mapenzi ya dhati, kila siku walikuwa pamoja huku mtoto Catherine akijitahidi kumuonyeshea Walter kwamba kweli alikuwa akimuhitaji kama rafiki katika maisha yake.

Siku ziliendelea kukatika, wakaendelea kukua zaidi na zaidi, ukaribu ule ukaongezeka kiasi kwamba Catherine akawa haoni wala hasikii kwa Walter, kila siku ilikuwa ni lazima awe mtu wa kwanza kuzungumza naye shuleni wakati anaingia na awe mtu wa mwisho kuzungumza naye wakati akiondoka.

Ilikuwa hivyo, wazazi waliendelea kuwashangaa, haikuwa rahisi kuona watoto waliokuwa wakipendana kiasi hicho, walishindwa kuwatenganisha na kwa jinsi walivyokuwa wakiwaona walivyopendana, walihisi kabisa hapo baadaye kungekuwa na ugumu mkubwa kuwatenganisha.

Siku zikaendelea kukatika, baada ya miaka mitano, baba yake, Bwana Gordon Smith akamaliza muda wake wa kuwa balozi wa Uingereza nchini Tanzania hivyo kurudi na familia yake nchini huko.

Hilo likawa pigo kubwa kwa Catherine, siku za kwanza zilikuwa ni ngumu sana kwake, alikuwa akilia kila wakati, alikosa furaha na muda mwingi alikuwa mtu wa huzuni tele.

Wazazi wake wakajaribu kumletea marafiki wengi wa kukaa naye lakini hakubadilika, bado kichwa chake na moyo wake ulimfikiria mtu mmoja tu, Walter aliyekuwa nchini Tanzania.

Baada ya miaka mingine mitano kukatika, Catherine akafanya vizuri katika masomo yake na hivyo kuchaguliwa kusoma katika Chuo Kikuu cha Oford kilichokuwa hapohapo Uingereza.

Bado hakuacha kumfikiria Walter, alimkumbuka mwanaume huyo, alipata marafiki wengi lakini kwa Walter ilikuwa ni tofauti kabisa, alikuwa rafiki aliyejali na kumsikiliza, aliufurahisha moyo wake na muda mwingi alitamani kumuona tena mbele yake, alitamani kumwambia kwamba katika maisha yake yote hakika asingepata rafiki wa kweli kama alivyokuwa yeye.

Wakati kichwa chake kikimfikiria sana ndipo akaamua kumtafuta katika mtandao. Hakupata kazi kumpata kwani mapacha hao walikuwa maarufu mno nchini humo kutokana na vipaji walivyokuwanavyo.
 
SEHEMU YA 68

Moyo wake ukaridhika, alifurahi kumuona Walter, mwanaume aliyekuwa akimpenda kupita kiasi. Alitamani kusafiri kuelekea nchini Tanzania kwa ajili ya kuonana naye lakini masomo yalikuwa yakimbana na kuwa na ratiba ndefu mno.

Siku zikakatika, mwanaume huyo aliendelea kuishi moyoni mwake. Kila siku ilikuwa ni lazima kuingia katika chaneli yao iliokuwa YouTube na kuanza kumwangalia jinsi alivyokuwa akiimba, sauti yake nzuri ilimtetemesha, hakuhisi kama kungekuwa na mtu aliyekuwa na sauti nzuri kama ilivyokuwa kwa mwanaume huyo.

Wakati kichwa chake kikimfikiria Walter ndipo mwanaume mwingine akaanza kujisogeza. Huyu aliitwa Edmund, mwanaume aliyekuwa akisomea masuala ya IT hapo Oxford.

Siku ya kwanza Edmund alipomuona Catherine moyo wake ulitetemeka mno, hakudiriki kuyatoa macho yake kwa msichana huyo, alikuwa mzuri wa sura, alikuwa mrembo mno kiasi kwamba kila alipokuwa akimwangalia, hakuisha hamu kabisa.

Akaanza kujipendekeza, kitu cha kwanza alichokuwa akikihitaji ni kuwa rafiki yake, wazungumze kama marafiki lakini mwisho wa siku amwambie ukweli kwamba alikuwa akimpenda kupita kawaida.

Kwa msichana kama Catherine halikuwa jambo jepesi hata kidogo, alikuwa msichana mgumu kuzoeleka lakini kwa Edmund naye hakuwa mwanaume aliyekuwa na moyo mwepesi wa kukata tamaa.

Aliendelea kumfuatilia msichana huyo huku kila alipokuwa akimuona, alimfuata na kupiga naye stori. Catherine hakuwa akipenda ukaribu na mwanaume huyo lakini kwa kuwa alianza kumng’ang’ania sana mwisho wa siku akajikuta akiwa karibu naye.

Kichwa chake kilifikiria urafiki zaidi lakini kichwa cha Edmund kilifikiria mapenzi zaidi.

Walikuwa karibu kiasi kwamba mpaka watu wengine wakahisi kwamba wawili hao walikuwa wapenzi.

Edmund hakutaka kukaa kimya, alijua kwamba kama wangezoeana zaidi basi suala la kaka na dada lingeingilia kati kitu kilichomfanya kuanza kumchombeza msichana huyo kwa maneno ya hapa na pale.

Siku za kwanza ilikuwa ngumu kwa msichana huyo kuelewa lakini baada ya Edmund kung’ang’ania zaidi, mwisho wa siku akampata msichana huyo na kuanza kuwa wapenzi.

“Edmund!” aliita msichana huyo.
“Unasemaje mpenzi!”
“Naomba nikuombe kitu!”
 
Back
Top Bottom