Shunie
JF-Expert Member
- Aug 14, 2016
- 157,400
- 465,166
- Thread starter
- #341
Sehemu ya 112
Patricia hakutaka kubaki mahali hapo, alichokifanya ni kuchukua teksi na kuanza kuondoka mahali hapo huku akionekana kuwa na furaha tele.
Wakati gari likiwa limeingia katika Barabara ya St. Louis IV, ghafla honi nyingi zikaanza kusikika, dereva alikuwa amejisahau kuzembe kabisa, hakuangalia vizuri taa zilizokuwa zikiwaka na hivyo kuingia katika barabara hiyo iliyokuwa ikiruhusu magari yaliyokuwa yakikimbia kuanzia kasi ya 100 mpaka 150. Ni mlio mmoja mkubwa ndiyo uliosikika mahali hapo.
“Puuuuuuuu!” Teksi ile ikagongwa, ikaruka angani, ikabingirika mara tano, watu wakashika vichwa, ilipotua chini, damu tu ndizo zilizokuwa zikionekana kwenye lami. Patricia akatulia kwenye kiti kama alivyokuwa huku akitokwa na damu mfululizo.
*** Hakukuwa na siku ambayo Walker alikuwa na hamu ya kuzungumza na Patricia kama siku hiyo. Wakati wakiwa kwenye mkutano kwa ajili ya kusaini mkataba huo ambao ungewafanya kuwa majaji katika Shindano la American Got Talent, kichwa chake kilikuwa kikimfikiria msichana huyo mrembo.
Wakati mwingine alitamani asimame na kuondoka, aliona kila kitu kikiendelea taratibu sana, alitamani yeye ndiye angekuwa msimamizi wa mkutano huo mdogo ambao angeamua ni muda gani walitakiwa kuondoka humo ndani.
Muda ulizidi kwenda mbele, baada ya dakika kadhaa, akapokea notification ya CNN ambayo ilimwambia kwamba kulikuwa na ajali mbaya iliyokuwa imetokea katika Barabara ya St. Louis.
Hilo wala halikumtisha, kwake, lilionekana kuwa jambo la kawaida akaendelea kukaa kwenye kikao mpaka kilipokwisha ambapo kitu cha kwanza kabisa akachukua simu yake na kumpigia Patricia ambaye alimwambia atangulie hotelini.
Simu ikaanza kuita pasipo kupokelewa, hilo halikumtia hofu sana kwani alihisi kwamba msichana huyo alikuwa bafuni akioga hivyo kusubiri zaidi na baada ya dakika kadhaa kumpigia tena.
Majibu hayakubadilika, yaliendelea kuwa vilevile kwamba simu haikupokelewa.
Hilo likaanza kumtia hofu, akaanza kuhisi kwamba kulikuwa na kitu kilichokuwa kikiendelea huko alipokuwa.
Alichokifanya ni kupiga simu katika hoteli aliyomuwekea chumba kwa lengo la kusikia kama msichana huyo alikuwa amefika humo au la.