Shunie
JF-Expert Member
- Aug 14, 2016
- 152,999
- 453,892
Nyemo ChilonganiSEHEMU YA 01
Cassian alikuwa kimya, macho yake yalikuwa yakiangalia baharini huku mawazo yake yakiwa mbali kabisa. Moyo wake ulichoka, maumivu aliyokuwa akiyasikia moyoni mwake hayakuweza kuelezeka.
Alikuwa bilionea mkubwa, mwenye makampuni mengi, migodi ya dhahabu na kila kitu ambacho kingemfanya kustahili kuitwa bilionea. Alimshukuru Mungu kwa utajiri aliokuwa nao lakini tatizo lilikuwa moja tu, hakuwa na mtoto.
Hilo lilikuwa pigo kubwa katika maisha yake, wakati mwingine alikuwa akimuuliza Mungu juu ya kilichokuwa kimetokea. Kwa nini alimpa utajiri mkubwa na kumnyima mtoto? Utajiri ungekuwa na maana gani kama tu hakuwa na mtoto ambaye angekuja kuurithi baada ya yeye kufa?
Hakuwa na furaha hata kidogo, kila siku moyo wake ulichoma kama moto kiasi kwamba alimuonea aibu mkewe, hata kukutana naye wakati mwingine aliogopa kutokana na tatizo lililokuwa mwilini mwake.
Hapo ufukweni mawazo yake yalikuwa mbali kabisa. Alitulia ndani ya gari huku akionekana kuwa na mawazo lukuki, alikaa garini kwa dakika kadhaa ndipo akaamua kutoka na kuanza kutembea. Kwa jinsi alivyokuwa akiwaza mpaka wakati mwingine machozi yalikuwa yakimtiririka mashavuni mwake.
Aligombana na dada zake kwa sababu hakuwa na mtoto. Kipindi cha kwanza ndugu hao walifikiri kwamba mwanamke aliyekuwa akiishi naye ndiye alikuwa na matatizo lakini baada ya kupima katika hospitali tatu, zote zilionyesha yeye ndiye alikuwa na matatizo.
Hakutaka kuwaambia ndugu zake ukweli, alikuwa tayari kugombana nao na hata kuchukiana maisha yake yote lakini si kuwaambia ukweli kwamba tatizo la kutokupata mtoto lilisababishwa na yeye na si mpenzi wake kama walivyokuwa wakihisi.
“Kwa nini wanamuonea? Kwa nini hawataki kuniuliza ili wajue ukweli kwamba Evelyne hana tatizo?” alijiuliza huku machozi yakimtiririka mashavuni mwake.
Hayo ndiyo yalikuwa maisha yake ya kila siku. Moyo wake ulimuuma mno, hakuona thamani ya utajiri, bila kuwa na mtoto maisha yake yangekuwa hivyohivyo mpaka kifo chake na mali kubaki kwa ndugu zake.