Vifurushi vya Vodacom vyarejea

Vifurushi vya Vodacom vyarejea

Nimejiweka Zantel ni burudani kabisa raha mustarehe.
1500=1.5 gb-160 mnts-500 sms per 7 dys.
1000=1 gd 7 dys.
10,000=10 gb 30 dys.
We we we we wewewewewe! Tena komea hapohapo hao wajinga wezi sana tena nitumie nafasi hii kuwatahadharisha ndugu zangu

Epukeni kuunga vifurushi vya mara kwa mara Zantel... mtakuja kunishukuru
 
We we we we wewewewewe! Tena komea hapohapo hao wajinga wezi sana tena nitumie nafasi hii kuwatahadharisha ndugu zangu

Epukeni kuunga vifurushi vya mara kwa mara Zantel... mtakuja kunishukuru
Nilijua napigwa mwenyewe, kumbe tuko wengi.
 
Daa naona wanaangalia sura au matumizi ases mimi mbona hawajanipa
Screenshot_2021-04-16-18-33-20.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakuu wasalam !nimeona mabadiliko kwenye vifurushi hususan internet kwa shilling elf 3000 unapata gb3 week nzima awali nilikuwa napata gb 1.2 kwa week
Hii inaweza kuwa nafuu kwangu mimi

Sijui kwako *149*03# Zama ujionee
Mbona hakuna mabadiliko
 
Ila kwa mtu mwenye matumizi makubwa ni bora ununue 50gb kwa 50k, kwa mwezi ipo kwenye Jimwage Data...

Mi natembea na hiyo angalau kuna unafuu, voda inabaki kuwa internet bora kabisa kwenye speed pamoja na kwamba ni ghali..

Mi ndo maana sihami boda, kwa mwezi nikitumia 100k kwenye data sio mbaya.
 
Nasikia TTCL GB 1.2 1000 wiki nzima. Kweli nyumbani kumenoga.
TTCL ni viazi mbatata, nilidhani wangekuwa juu kwa huduma hasa kwa speed ya net maana nadhani wana privilege kwa kuwa ni govt owned wana ahueni ya baadhi ya costs.
Mkonga wa mawasiliano wanamiliki wao hata kama in direct.
 
Nimejiweka Zantel ni burudani kabisa raha mustarehe.
1500=1.5 gb-160 mnts-500 sms per 7 dys.
1000=1 gd 7 dys.
10,000=10 gb 30 dys.
Sipendi kuweka mambo yangu humu kwahiyo sitatoa ushahidi tofauti na maelezo (japo ninao ushahidi wa kutosha)

Tangu nisajili laini nimekuwa nikiunga bando kwa easypesa tu, ni mara chache sana (nadhani mbili au tatu tu) kuweka vocha kutokana na kutokuwepo kwa vocha za Zantel huku nilipo na hata zikiwepo bei inakuwa juu maradufu

Februari mwaka huu tarehe fulani nikaweka vocha na kuunga kifurushi kisha salio likabakia, baada ya muda fulani walipoona situmii ile vocha mara pap napata notifications kucheki nakuta sms mbili dabo ya kwanza hongera kwa kujiunga na *¥$&?(natajiwa lihuduma hata silijui) na ya pili umefanikiwa kujitoa kwenye *¥$&?

Muda huo nilikuwa nahangaika kuunga kifurushi kingine maana niliona kile nilichonacho kimebakia kidogo, basi kila nikiunga naambiwa sina salio la kutosha kucheki salio kweli halitoshi aisee nikalipuka kwa hasira nikawapigia na hapo ndipo nilipoamini ile kauli ya mitandao ni wezi wanatuibia halafu wana majibu ya kukaririsha, kama mtu asiyependa bugdha ndo kwanza anaachilia mbali kufuatilia

Eti kajidai kucheki anasema hakuna tatizo hakuna hela iliyokatwa mara nilipombananisha anasema umejiunga na huduma flani kumbana zaidi ndo akanifanya nicheke badala ya kukasirika. Ananambia eti hiyo huduma ulijiungaga tangu mwezi wa 10 mwaka uliopita ila kwakuwa leo ndo umeweka vocha basi ndomana umekatwa leo gharama za huduma

Nikazidi kumthibitishia kuwa sijajiunga akasema eti huenda mtu ameniunga nikamkazia zaidi kwamba simu yangu haijawahi kutumiwa na mtu jamaa akawa amekomalia tu hapohapo eti huenda tu kuna siku labda nilibonyeza hata kwa bahati mbaya wakati wa kuongea au hata ikiwa mfukoni. Nikamuuliza vipi na swala la kujitoa nalo maana sms yapili inaonesha nimejitoa jamaa akakosa la kujibu

Habari hiyo ndefu sana ngoja tuikate tu maana hata hapo ilipoanzia siyo mwanzo

Hiyo part one na tuiache sasa twende kwenye part two

Juzi nimeunga bando halafu sikulitumia kutokana na maswala ya chaji sasa Leo hii naingia jamiiforums data haifanyi kazi kila nikiingia kwenye app yoyote ya kuhitaji internet mambo hayaendi nikasema ngoja niangalie salio nakuta sms hakuna data hakuna hata zile dakika tano tano za Zantel hakuna (huku sina mtu wa Zantel wa kumpigia) na wakati huo mimi naunga mara kwa mara vifurushi vya 'bao bila kikomo' sms100 dk5Z-Z na gb1. Basi nikaunga kifurushi kingine kisha nikawatwangia tena huduma kwa wateja

Eti anasema hapa nikiangalia una dk za Zantel na sms kadha wa kadha na data unazo mb za kutosha kabisa (anataja mb zile nilizounga muda huo). Nikamkomalia akasema subiri nicheki zaidi. Mara kurudi anasema sasa kifurushi chako inaonesha kimeshaisha kwakuwa aina ya kifurushi hicho kinadumu ndani ya siku tatu tu nikamuuliza haya ndo mabadiliko mliyotuahidi sasa mbona hayapo wazi akajibu eti niwe mvumilivu kwa muda huu maana kuna mabadiliko mengi yanajitokeza

Nilipombana zaidi kwamba kama ni hivyo mbona dakika umenitajia hapo inaonesha mpaka za juzi bado zipo na sms inakuwaje data pekee ndo imeexpire halafu kwanini wewe uone vingine huko na mimi nikiangalia salio niletewe vingine? Hakuwa na cha kujibu cha maana

Mpaka hapo nikagundua kuwa

1. Tumepigwa changa kuhusu vifurushi kurejeshwa kama zamani. Either TCRA au Mitandao kuna anayerudisha gharama za hasara alizokula

2. Mitandao wanajivunia kwamba hatuwezi kuwafanya lolote/ kuwashtaki kwakuwa hela wanayokata au kuiba ni ndogo kwa mtu mmoja mmoja

3. Huduma kwa wateja imewekwa options nyingi na za kuzunguka sana ili kuepuka au kuepusha wao kupatikana kiurahisi (mfano chagua 1 kwa Kiingereza- ila ukiingia unakuta huduma ni vilevile kwa Kiswahili)

4. Jamaa wanakuibia halafu ukiwapigia mbinu zao ni tatu

-upigwe kalenda, ngoja kidogo mpaka ukate tamaa na mara nyingine simu isipokelewe au ikatwe kabisa

-ubambikiziwe (kwamba umejiunga) lihuduma ambalo hata hulijui ilimradi tu ionekane umekatwa kihalali

-haiwezi wala haitaweza kutokea ukarudishiwa hela uliyoibiwa (sijawahi kusikia mtu amerudishiwa pesa zaidi ya kuombwa radhi tu) ukiwabananisha maswali au ukija juu kidogo mara nyingine wanakata simu
 
Wakuu wasalam !nimeona mabadiliko kwenye vifurushi hususan internet kwa shilling elf 3000 unapata gb3 week nzima awali nilikuwa napata gb 1.2 kwa week
Hii inaweza kuwa nafuu kwangu mimi

Sijui kwako *149*03# Zama ujionee
Nilitaka kununua kifurushi cha internet (Vodacom) jioni hii, nikakuta bado ni Sh3,000 kwa GB1.2. Nikaghaili na kununua kifurushi cha internet (Airtel) cha wiki cha Sh2,000 kwa GB1.
 
Back
Top Bottom