dikteta2020
JF-Expert Member
- Aug 14, 2018
- 595
- 3,990
Hawa ni wachambuzi wa kisasa nchini Kenya wakishangazwa na namna Tanzania ilipo bado kwenye ukoloni japo ni wa watu weusi.
Alichokiongea kina mantiki sijui kama umemsikiliza lakiniKenya kuna ukabila hatuwezi iga
Mimi sina chama ila katiba hii ya Tanzania ni bora kuliko zote Africa
Ukizungumzia ubaguzi wa kikabila pia usisahau hapa kwetu kuna mgombea anayehutubia kikabila, anayehubiri ubaguzi wa kuleta maendeleo kwa majimbo yenye vyama vya upinzani.Siasa za Kenya ni za ubaguzi wa kikabila.
Kenya wapambane kwanza waondoe hili kabla ya wao kukosoa wengine.
Wataambiwa mawakala wa mabeberuHawa ni wachambuzi wa kisasa nchini Kenya wakishangazwa na namna Tanzania ilipo bado kwenye ukoloni japo ni wa watu weusi.
View attachment 1590849
Umesoma katiba ya Kenya? Huwezi kuilinganisha na ya Tz. Ni nzuri mno!
Tanzania hatuna ukabila bwashee.Ukizungumzia ubaguzi wa kikabila pia usisahau hapa kwetu kuna mgombea anayehutubia kikabila ,anayehubiri ubaguzi wa kuleta maendeleo kwa majimbo yenye vyama vya upinzani
Tufikiri kwa ndani zaidi. Kweli tunadhani kuwa tume ya uchaguzi iliyoteuliwa na mmoja wa mgombea inaweza kuwa huru? Inaweza kumtangaza mgombea mwingine kuwa mshindi hata kama kashinda kihalali? Inaweza isimbebe kweli anayewalipa mshara?Hawa ni wachambuzi wa kisasa nchini Kenya wakishangazwa na namna Tanzania ilipo bado kwenye ukoloni japo ni wa watu weusi.
View attachment 1590849
Siasa za Kenya ni za ubaguzi wa kikabila.
Kenya wapambane kwanza waondoe hili kabla ya wao kukosoa wengine.
Rudi kwenye mada mkuu.Pale Kenya sasa hivi ni kama hamna mkubwa! Kila mtu ni kambare! Wamejaa ukabila, hayo ndio waliyoendelea hakuna kingine.
Fikiria uchaguzi bado miaka 2 lakini ofisi ya rais Kenyata ina mgogoro wa kugombea madaraka ya 2022