VIDEO: Tundu Lissu amjibu Mama Samia Suluhu kuhusu uhakika wa CCM kuunda Serikali

The Palm Tree

JF-Expert Member
Apr 13, 2013
7,951
12,535
Siku chache zilizopita mgombea mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM na makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan alinukuliwa ktk moja ya mikutano yake ya kampeni akisema..

Hata kama kura hazitatosha mwaka huu, wao (i.e CCM) wana uhakika wa kuunda serikali na kuendelea kutawala kwa miaka mingine mitano tena (2020 - 2025)..

Katika video hii, Mgombea Urais kwa tiketi ya CHADEMA, Mh. Tundu Lissu akaipata hiyo. Na hapa ndilo jibu lake kwa Mama Samia Suluhu..

Kabla hajamjibu Mama Samia, Tundu Lissu anaanza kwa kulilalamikia Jeshi la polisi mkoa wa Dodoma kwa kuutelekeza msafara wa mgombea huyu wa Urais alipokuwa anatoka Kongwa kuja hapa Dodoma..

Haikuleweka mara moja sababu za RPC wa Dodoma na OCD wake wa wilaya ya Dodoma kutelekeza jukumu lao hili muhimu la ulinzi na usalama wa mgombea huyu wa Urais kama wanavyotakiwa kufanya na sheria za nchi na hususani sheria na kanuni za uchaguzi mkuu wa 2020..

Je, kulikuwa na jambo baya lililopangwa kutendeka jana hiyo mfano ajali dhidi ya Tundu Lissu na hivyo polisi kutoa mwanya kutekelezwa kwa kujiondoa kuongoza na kuulinda msafara wake?


 
Back
Top Bottom